NDONDI: Si kingine; NI AIBU, AIBU KWELI!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NDONDI: Si kingine; NI AIBU, AIBU KWELI!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Steve Dii, Oct 27, 2007.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ifuatayo ni tahiriri ya mhariri wa HabariLeo kuhusu timu ya ngumi Tanzania kushindwa kwenda kushiriki kwenye mashindano Amerika.

  Source: HabariLEO.


  Ndugu Mhariri, walau ungetaja ni kiasi gani takribani tungeweza kuwa na upeo mkubwa zaidi katika unayoyasema na kulinganisha na mambo mengine mengi ambayo serikali inapanga na kuyafanya ndani ya miezi minne au mitano!

  Kweli kabisa serikali yetu siyo ya kutegemea katika yote. Wakina Matumula na wenzake wanapopata nafasi na kushinda na kuiletea sifa Tanzania, serikali isijitie kimbelembele basi... (Mbona wanasoka wetu walikaribishwa hadi bungeni na kuchangiwa pesa kibao au ndondi ni mchezo wa vagi tu?!!).

  Vyama gani hivyo?.. vague statement, again where is your credibility as an editor for the nation's newspaper?! Taja angalau chama kimoja na kuonyesha upeo wako, ili msomaji apate uelewo wa mambo unayoongelea. Na nakuomba ujitahidi kuandika vitu kutoka rohoni mwako na si kwa mashinikizo ya viongozi wa serikali. Lusekelo does it well and works under the same roof :)

  Natamani kweli mtu ajitokeze kuwadhamini wanadondi wetu, natamani pia kuona wanashinda mashindano makubwa duniani na kuitangaza Tanzania yetu ila sifa zote zimwendee mdhamini wao na siyo serikali tena.

  Sir/Madam, seems to me that you are confused na hujui la kuwaambia wasomaji wa gazeti. Kuwa na msimamo ndugu, kwa namna fulani unataka kuonyesha umakini na unachokiongelea, lakini kutokana na kubanwa na watu fulani unateleleka ghafla na kupoteza mwelekeo. Miye naamini kabisa kuwa kile ulichotaka kuandika hapo ilikuwa kuikemea serikali...ila ndiyo hivyo tena... umewapisha wababe, labda nisikulaumu sana!!

  SteveD.
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Bongofleva naona wao wamepata udhamini wa serikali kulingana na habari hii kutoka gazeti hilo hilo:

  Source: HabariLEO.

  SteveD.
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Steve kwa upande mwingine timu ya ngumi kutokwenda huko Chicago ni neema kwetu. Kimsingi timu haina maandalizi kabisa na kwa asilimia kubwa walikuwa wanakwenda kushiriki na sio kushindana.

  Ama kuhusu bongofleva hiyo ni danganya toto hakuna msaada wowote zaidi ya ahadi hewa.

  Bado tuna safari ndefu kwenye anga za michezo
   
Loading...