Ndomba kuwa mkurugenzi wa Takukuru soon

Maseke ya Meme

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
695
914
Inasemekana muda si mrefu muungwana atafanya mambo hadharani! Ni tetesi kutoka ndani ya jikotayari kwa kupakuliwa.

Stay tuned...................................
 
Inasemekana muda si mrefu muungwana atafanya mambo hadharani! Ni tetesi kutoka ndani ya jikotayari kwa kupakuliwa.

Stay tuned...................................


Thanx!
Who is Ndomba by the way? His/her full name....!
 
Kama ni huyo Col Samuel Ndomba ni mshkaji wa JK tangu walipokuwa pamoja jeshini Monduli.
 
Hatimaye fisadi Hosea aondolewa PCCB. Kafukuzwa, kastaafishwa kwa manufaa ya umma au ni mabadiliko tu ya kawaida? labda atapatiwa nafasi nyingine ya juu?
 
Itakuwa mara ya pili kuwa na mjeshi PCCB, kwani kabla ya Hosea alikuwepo Maj Gen Anatoly Kamazima. Na taasisi nyingi zilishikwa na wajeshi tangu kabla, kama kuna wanaojua sababu watuambie: Col Abihud Nalingigwa (mawasiliano, sasa TCRA), Brig Gen Prof Dr Yadon Kohi (COSTECH), Maj Gen Herman Lupogo (TACAIDS), Brig Gen Muhiddin Kimario (CDA), Brig Gen Augustino Ramadhani (Makamu Mwenyekiti, Tume ya Uchaguzi. sasa Jaji Mkuu), na wengine tajeni. Hii imekaaje? Na je kuna nafuu kuliko zikishikwa na raia? Au huko jeshini hakuna kazi za hawa wakubwa? Ingekuwa vipi kama hawa wakuu wangetumia taaluma zao kuimarisha jeshi kama taasisi inayojimudu ki-rasilimali, kuliko wao kuondoka huko halafu wanabaki kuajiri raia? Majeshi ya wakubwa huku yana viwanda vya zana, taasisi za research zinazojitegemea na tena zinachapisha scientific journals katika fani nyingi, mashule hadi university, vyuo vingine vya viwango mbalimbali, mahospitali makubwa ya rufaa na ya kufundishia madaktari wao, viwanda vya madawa (na utafiti wake), mashamba ya nafaka,, mboga, mifugo, usindikaji wa vyakula (ration) na mambo mengine kibao, askari mtaalamu ana kazi za kutosha jeshini. Na ikitokea dharura hawa jamaa wana uwezo wa kuchukua nafasi zote za raia (wanao watawala, wachumi, wanasheria, wanasayansi wa karibu kila kitu kilichoko uraiani, na wapiganaji wenyewe wa medani) yaani ni kama li-serikali fulani la akiba tena lenye maguvu, lakini limetulia tu! Sijui kama jeshi letu ni hivyo au nao wanasubiri wachomolewe kambini na JK na kupewa ukuu wa wilaya na ukurugenzi wa mashirika!

Na sielewi hawa maafande wakikutana kwenye madaraka ya kiraia vyeo vyao vya kijeshi wanaviweka wapi, yaani sijui wanapeana vipi heshima wao kwa wao. Kwa mfano kuna wakati pale Arusha mkuu wa mkoa alikuwa Captain (na alikuwa anatajwa siku zote kwa cheo chake) na mkuu wa wilaya mojawapo alikuwa Colonel, sasa hawa sijui walikuwa wanasalimianaje wakutanapo! Na si kwamba hawakuwa active jeshini hawa, walikuwa bado active sana tu. Afande Brig Gen Augustine Ramadhani alifanyiwa gwaride la kuagwa jeshini akiwa ameshatumikia tume ya uchaguzi kwa muda mrefu na kufanikisha chaguzi mbili za Mkapa, kwa kushirikiana na mwenyekiti wake Lewis Makame. Muungwana JK alipandishwa cheo kutoka Meja kuwa Lt Col akiwa tayari Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini. Maj Gen Said Said Kalembo alifanyiwa gwaride la kuagwa kwa ule mtindo wao wa kusukumwa gari lake hadi nje ya kambi akiwa tayari keshakuwa mkuu wa mkoa kwa miaka kadhaa.

Ufanyaji kazi wa hawa maafande na raia munaufahamu? Kule Mahenge kulikuwa na mkuu wa wilaya Brig Gen Sylvester Hemed, siku moja walikuja wazungu wafadhili wa mradi fulani, wakati wa kumkaribisha atoe hotuba ya kuzindua mradi, wakamtaja ni "Mr Sylvester Hemed", hakuinuka kitini! Na hata viongozi wengine wa wilaya walipowashitua mabosi wa mradi kuwa wamekosea kumtaja mkuu kwa cheo chake, na mhusika kurekebisha kosa hilo, hakukubali hadi alipoombwa radhi hadharani na kutamkiwa kuwa kosa hilo halitarudiwa! Ya Maj Gen James Luhanga nawaachia waliobahatika kumtumikia pale Iringa (natumaini wapo hapa) wayaseme, na ya Maj Gen Tumainieli Kiwelu huko Kagera nasikia sifa nyingi, lakini wakimbizi wa Ngara huko najua wanayo hadithi yao.
 
Nadhani swali la msingi ni je walistaafu kwanza jeshini? Sina tatizo kama former military man kuingia uraiani lakini ni muhimu astaafu jeshini na hivyo asiwe in the active service. Hebru fikiria Jaji Mkuu bado ni Brigedia Jenerali...
 
Nadhani swali la msingi ni je walistaafu kwanza jeshini? Sina tatizo kama former military man kuingia uraiani lakini ni muhimu astaafu jeshini na hivyo asiwe in the active service. Hebru fikiria Jaji Mkuu bado ni Brigedia Jenerali...

Mkuu huyu jaji mkuu aliendesha chaguzi mbili za Mkapa akiwa makamu mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi na hapohapo akiwa Brig Gen wa JWTZ. Alistaafu jeshini baada ya uchaguzi wa 2000. Brig Gen Kohi amekuwa mkurugenzi wa COSTECH miaka yote akiwa askari, actually hata vyeo alipandishwa akiwa hapo, na alipondolewa majuzi na JK tuliambiwa alirudishwa jeshini. Lt Col Fabian Masawe alichukuliwa kutoka JWTZ (kabla alikuwa headmaster wa Jitegemee sekondari, ya JKT) kuwa mkuu wa wilaya, hatujasikia kastaafu.
 
Jamani mie nafikili JK amefikia mahali bora atumie wajeshi wenzake maana anaona raia wanamharibia mpaka sasa jamaa anarekebisha matatizo tu aliyoahidi wakati wa kampeni mengi nayaona bado.
 
Watu na sehemu zao walizo teuliwa ulizotaja ni sawa ila angalia kwa umakini ktk siasa itengulisha kuhusisha siasa na jeshi na ndipo JK akatoka jeshini. Kuhisi nyadhiva za kisiasa Brother Ben aliwatumia sana wanajeshi wastaafu ktk ukuu wa wilaya na mikoa,jaribu kuwa makini na rekodi zako maana kustahafu leo si kuanyiwa sherehe leo leo.
Na wanatumika kwa kuwa jamaa wame practice nidhamu.
Kuhusu nyadhifa zingine zisizo za kisiasa wanashiriki tu sioni tatizo,mimi nimefundishwa na mwanajeshi chuoni alikuwa kitengo cha radar bongo.
 
Unamaanisha Col. Samwel Ndomba RC wa Arusha?

Yah! Col Samuel Ndomba aliyekuwa RC wa Arusha baadaye akaitwa jeshini tena na kuwa Chief of Personnel. Jamaa ni smart na strict na shushushu aliyesomeshwa USSR enzi zake. Ni rafiki mkubwa wa JK tangu akiwa jeshini wakiwa Idara ya Utambuzi jeshini
 
Kithuku,Mwanakijiji,Mutu,Nangisye,

..nakumbuka kabla ya Maj.Gen.Kamazima alikuwepo Col.Maftaha.

..Raisi Kikwete ameingia madarakani kwa kutumia siasa chafu na rushwa. huwezi kumtegemea Kikwete apambane na rushwa, labda ile inayowahusu maadui wake wa kisiasa.

..matatizo yetu hayawezi kuisha hata ateremshwe malaika kuongoza anti-corruption.
 
Watu na sehemu zao walizo teuliwa ulizotaja ni sawa ila angalia kwa umakini ktk siasa itengulisha kuhusisha siasa na jeshi na ndipo JK akatoka jeshini. Kuhisi nyadhiva za kisiasa Brother Ben aliwatumia sana wanajeshi wastaafu ktk ukuu wa wilaya na mikoa,jaribu kuwa makini na rekodi zako maana kustahafu leo si kuanyiwa sherehe leo leo.
Na wanatumika kwa kuwa jamaa wame practice nidhamu.
Kuhusu nyadhifa zingine zisizo za kisiasa wanashiriki tu sioni tatizo,mimi nimefundishwa na mwanajeshi chuoni alikuwa kitengo cha radar bongo.

Kwa hiyo una maoni gani kuhusu kuwachukua askari ambao bado wako kwenye active service jeshini na kuwapa nyadhifa za kisiasa? Nakupa mifano miwili: Brig Gen Dr Johannes Balele mkuu wa mkoa wa Shinyanga, na Col Samwel Ndomba aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye JK alimpandisha cheo kuwa Brig Gen na kumrudisha makao makuu kuwa Mkuu wa Utumishi. Sasa sijui huyu Brig Gen Ndomba hapo kwenye ukuu wa mkoa wa Arusha alikuwa seconded from JWTZ au ni kituo kimojawapo cha kazi za JWTZ? Yale mabadiliko ya 1992 yaliyowataka wanajeshi walioko katika kazi za siasa kustaafu kazi za jeshi bado yanafanya kazi au Rais anayo madaraka yasiyo na kipimo ya kuteua yeyote kwa nafasi yoyote na akitaka anamrudisha jeshini? Maana nakumbuka kipindi kile katika mabadiliko yaliyoleta vyama vingi ndipo akina Brig Gen Moses Nnauye, Col Jakaya Kikwete, Major Sigela Nswima, , Capt John Komba na wengine wengi walipostaafu utumishi wa JWTZ na kubaki na kazi za kisiasa. Hawa wa sasa hivi wa JK (kina Ndomba, Balele, Masawe) naona ni tofauti kabisa, wao wanashika vyote!
 
Hapo panatosha (kwa sasa)sasa tuangalie mipango ijayo ya atakaepewa rungu zito la pccb maana mmmm kama hatawekewa mipaka ya kisiasa kwenye utendaji wake...jamani ni hakika patakuwa hapatoshi................
 
Muhimu kwangu sio ujeshi...tunataka mtu atakayeleta heshima, uadilifu na uchapakazi PCCB. Isiwe tu ni kuendeshwa na wanasiasa. Mara nyingi nimewasikia watu waadilifu, strict......ila wanapokutana na sekeseke la "ufisadi" wanaanza kumomonyoka taratibu........!
 
Muhimu kwangu sio ujeshi...tunataka mtu atakayeleta heshima, uadilifu na uchapakazi PCCB. Isiwe tu ni kuendeshwa na wanasiasa. Mara nyingi nimewasikia watu waadilifu, strict......ila wanapokutana na sekeseke la "ufisadi" wanaanza kumomonyoka taratibu........!

Binafsi bado SIONI umuhimu wa PCCB. Labda nipewe umuhimu wake kwa watanzania wa leo! Failures ni nyingi sana, inawezekana mimi ni 'mpinzani' kwakuwa sioni umuhimu wa chombo hiki kwa taifa letu. Gharama wanazotumia hawa jamaa ni kubwa na mara nyingi wanashindwa kukabiliana na matatizo makubwa yanayolisumbua taifa letu.
 
Kwani katiba tarajali ya ccm imesemaje kuhusu wanajeshi au watu wengine wenye taaluma nyingine pindi waingizwapo kwenye nafasi za kisiasa?. Na kuhusu kazi za rais zimesemwaje?. Mwenye katiba hiyo atudokeze kidogo ili tupate pa kuanzia manake huku nilipo haijaonekana.
 
Nadhani swali la msingi ni je walistaafu kwanza jeshini? Sina tatizo kama former military man kuingia uraiani lakini ni muhimu astaafu jeshini na hivyo asiwe in the active service. Hebru fikiria Jaji Mkuu bado ni Brigedia Jenerali...

sasa inakuaje bado anapanda cheo wakati hayupo jeshini?
 
Back
Top Bottom