Haki.tupu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 254
- 3
Swali la msingi la kujiuliza ni kama Hosea ndo kikwazo cha ufisadi, mimi namchukia kwa kuwa na yeye ameiibia nchi hii sana lakini sina uhakika kama yeye ndo kiwazo cha kupambana na ufisadi.
Tusishangilie kwa kitu ambacho akitaleta mabadiliko hapo baadae tunatakiwa kudai PCCB iliyo huru zaidi na sio kiongozi wa PCCB mwadilifu kwani bila yeye kuwa huru hakuna chochote cha maana kitakachotokea.
Naungana na wewe kwa kiasi kikubwa. Lakini nadhani Hosea (in his own right) ni fisadi. Kwa hiyo aondolewe. Lakini tusishangilie sana kwa sababu ulizotoa. Pia nadhani wakiweka mtu mkali/msafi kidogo (mwingine ameshauri akina warioba na ulimwengu) nadhani tunaweza kuona mabadiliko kidogo. Unajua wakiweka mtu serious ambaye hata wakubwa zake wakimlazimisha kukubali jambo akaamua kuwakatalia/kujiuzulu tutakuwa tumepiga hatua. Hili la kudai PCCB huru, ni muhimu lakini maadam kwa sasa halionekani kuwa linawezekana (in the short run) basi tuweke mtu atakayeonyesha angalau tofauti (kama wanavyofanya akina Sita, Mwakyembe nk). Suala la PCCB kuwa na mandate linaweza kuwa gumu kama la kudai katiba mpya! Maana hawa jamaa wote wanaweza kupelekwa Keko!