Ndolanga ni janga

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,438
Muhidin Ndolanga ni mchafuzi, aliharibu FAT sasa ameharibu uchaguzi DRFA na FRAT, hana uadilifu wa kuwa mwenyekit wa kamati yoyote ya uchaguzi ni mvunja sheria anafahamika na ni AIBU KUBWA KWA TFF eti kumteua mjumbe wa Heshima! k

Kwa heshima ipi aliyonayo? Ang'olewe haraka sana kabla hajaharibu zaidi, ni mtu hatari mno kwa maendeleo ya soka.
 
Huyu mzee kwakweli ni janga. Mtu kama huyu angekuwa rais wa nchi angekuwa kama Mobutu au Mugabe. Jamaa mchumia Tumbo sana na ni janga(japo kuwa ni uncle wangu)
 
Wakuu..
Huyu the so called mjumbe wa heshima wa TFF mbona kawa kimeo sasa...
Mwanzoni mwa mwezi wa tisa kaondolewa kwenye wadhifa wa uenyekiti wa DRFA kisa kupitisha majina ya wagombea wasio na sifa na kuondoa majina ya wenye sifa
Jana tena, same story kapigwa chini FRAT kwa kuendesha uchaguzi ulio pigwa stop na kamati ya uchaguzi ya TFF.
Mzee Ndolanga (TYSON) ina maana hazijui sheria au ni ukorofi wake wake?
 
Hao ndio wazee wa mjini na hio mizengwe ndio inayowaweka mjini
amewahi kuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, amewahi kuwa Mwenyekiti wa FAt ambapo alidiriki kumtamkia Mohamed Mwameja kuwa 'hatakaa aichezee timu ya taifa ya Tanzania'.
Laana alizotoka nazo huko inaelekea ndizo zinamwangaisha maana kwa umri alionao Afrika inabidi awe amekaa na wazee kuwashauri watenda kazi njia nzuri za kutumia lakini cha ajabu bado anataka yeye ndiye awe 'mtenda kazi'!!!

hapana MH ndolanga ni jembe, hataki mambo ya mizengwe mizengwe, TFF imejaa mizengwe mizengwe ya kijinga , na tusitegemee .mafanikio yoyote ya mpira ktk nchi hii tukiwategemea viongozi walioko madarakani hivi sasa na rundo la vyeti, ndoo maana jembe Ndolanga linaona upuuzi. jiulize wasomi wanaoongoza mpira kipi? walichooongeza, uwanja wa karume umejengwa na fifa chini ya uongozi wa ndolanga.
 
Tuongee kwa ushahid tunapoelezea mapungufu ya mtu

lakini pia siwez kukupinga kwa hizo hoja zako kwa sababu wewe mwenyewe una amin ya kwamba uko sahihi
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza,inavyoonekana huwajui TFF weweeeeeeeeeeeeeee?!!ukishaona sehemu ambayo kamati ya TFF inafuta uchaguzi ama inawaondoa watu kwa sababu ambazo hazina mashiko ujue kwamba katika eneo hilo hakuna kundi lao ambao wanatarajia kwamba itakapofika wakati wa uchaguzi basi wanakwenda kuwapigia watu wao kura ili washinde na wao kama kamati waendelkee kula na kufaidi fedha za TFF.

Nakupa mifano michache tu hapa kama wewe ni mtafiti tafiti halafu usipobaini haya ninayokwambia basi ujue mimi ni muongo,angalia uchaguzi wa Mtwara namna ambavyo walifanya!,angalia uchaguzi wa Tabora TAREFA!,achilia mbali ucahguzi wa DRFA,angalia uchaguzi wa KATAVI kile ambacho wamekifanya wameufuta ule uchaguzi wakati tayari viongozi wamekaa madarakani kwa zaidi ya mwezi mzima.

Kanuni za uchaguzi ziko wazi kwamba kuna kamati ya uchaguzi ya eneo husika(MKOA) ambayo kazi yake haina tofauti na ile ya TFF ambayo ina mamlaaka kamili ya kushughulikia masuala yote ya uchauzi ikiwa ni pamoja na kuhakiki vyetu wa wagombea kupitia Baraza la Mtihani (NECTA) kama wana mashaka na vyeti vya muhusika,na inapofika kwa kamati ya TFF bado wanafanya vivyo hivyo kabla ya kuwaruhusu wagombea kuanza kampeni na hatimnaye kufanya uchaguzi.

Lakini cha ajabu yote hayo yanafanyika lakini cha ajabu baada ya mambo yoooooooote kukamilika kamati hiyo hiyo ya TFF inaibuka dakika za mwisho siku moja ama siku yenyewe ya uchaguzi ikidai inawaondo baadhi ya wagombea kwa kigezo cha kukosa sifa,ama kuwa na mashaka na vyeti vyao!!!!!!!!!!

Jamani kama si uonevuni nini ama kile ninachokisema kwamba ni kupanga safu yao ili siku ya uchaguzi wamchague mtu wao kwa maslahi yao ni nini???!!!!,hivi kama kweli ni hao hao TFF wamethibitisha wagombea wote kwamba wamekidhi vigezo mpaka wanaruhusiwa kufanya kampeni na kuingia kwenye uchaguzi nini kinatokea baadaye tena na kuibuka na hoja kwamba hawajakidhi vigezo,ndiyo maana tunasema kwamba Kamati ya Lyato ina walakini na inahitaji nayo kuvunjwa kwa sababu ndiyo inayoharibu mpira wa nchi hii.

Kwa kifupi ni kwamba kamati hii inataka kuwachukua watu ambao ni mbumbu ambao hawatakuwa na uwezo wa kuhoji matumizi mabaya ya fedha za TFF yaliyowasababisha wakina Tenda kujenga magorofa makubwa Dar,ikiwemo shilingi milioni 800 zinazotolewa kila mwaka na FIFA,shilingi Bilioni 1.4 zinazotolewa na Vodacom na ndiyo maana hata vilabu unaona haviambiwi ukweli wala kuoneshwa mkataba baina ya Vodacom na TFF.

Nakubali kwamba huenda Ndolanga anafanya makosa kama binadamu wa kawaida ama pengine anafanya makosa kwa makusudi kwa sababu anajua tu udhaifu ama pumba zinazofanywa na kamati ya Ucchaguzi ya TFF kwa sababu nayo inavurunda maeneo mengi,mfano ni huo uchaguzi wa FRAT wenyewe ambapo ni hiyohiyo kamati ya uchaguzi ndiyo iliyowapitisha wagombea na kuwaruhusu kufanya kampeni na siku ya uchaguzi asubuhi ndio wakatoa taarifa ya kuwaengua baadhi ya wagombea hao ambao walishinda na sasa wamefuta ushindi wao kwa madai kuwa hawakukidhi vigezo.

Swali la msingi la kujiuuliza hapa iweje wawapitishe na kuwaruhusu kufanya kampeni za uchaguzi na siku ya uchaguzi ndio wabainike kwamba hawana vigezo???!!hapa kuna tatizo na hasa kwa Lyato,lakini na yeye siku zake zinahesabiwa atabainika na kuanikwa haddharani bado naamini anavutiwa tu kasi.

Hata ukija kwenye sababu zilizosababisha wakaweka na vigezo vya elimu ya sekondari ni kwa sababu tu kuna vichwa vikali abavyo vilikuwa vikiwabana kila kona na kuwanyima usingizi kama wakina Abdalah Bulembo kwa hiyo wakajipanga namna ya kuwaondoa,lakini bado kuna taarifa kwamba kuna watu wao ambao wanawaingiza pamoja na kwamba hawana vigezo husika kwa sababu tu wanajua ni kura zao.

Ngoja kwa leo niishie hapa lakini nataka nikwambie kwamba siku za Kamati ya Ligi na TFF zinahesabika
 
Ni kweli kwamba TFF ina matatizo kibao ,lakini leo nimemwangalia Ndolanga tu , tusitumie matatizo mengine ya TFF kuruhusu vurugu za ndolanga , kama alijua anafanya kazi na TFF hawezi kukwepa utaratibu , kumpitisha Bhakhresa ili hali akiwa hana cheti cha kidato cha nne ni Uhuni .
 
Muhidin Ndolanga ni mchafuzi , aliharibu FAT sasa ameharibu uchaguzi DRFA na FRAT , hana uadilifu wa kuwa mwenyekit wa kamati yoyote ya uchaguzi ni mvunja sheria anafahamika na ni AIBU KUBWA KWA TFF eti kumteua mjumbe wa Heshima ! kwa heshima ipi aliyonayo ? Ang'olewe haraka sana kabla hajaharibu zaidi , ni mtu hatari mno kwa maendeleo ya soka .

Sio Ndolanga peke yake, hawa viongozi wote ambao walikuwa kwenye soka kuanzia mwishoni mwa miaka ya 80 ni majanga.
Umri umeenda, achilia mbali ukweli kuwa uwezo wao kiutendaji ni mdogo sana, hawana jipya kwenye soka.
Huwezi kumlaumu Ndolanga kisha ukamuacha mtu kama Aden Rage au Sunday Kayuni.
Wote kwa ujumla wao ni janga, tunahitaji akili mpya za kuongoza mchezo huu.
 
Kwa kuongezea tu, akiwa mwananfunzi wa Tabora Boys enzi hizo kulikuwa na mpira uwanja wa VITA, akawatukana mashabiki wa timu pinzani , basi walimvua kaptula na alikimbia uchi wa nyama nyekundu kutoka uwanja wa VITA mpaka shuleni Tabora Boys. Anayetaka kujua zaidi amuuliza Mh Kapuya wamesoma nae Tabora Boys atawasimulia kadhia za huyu jamaa.

Upuuzi hajaanza leo
 
Back
Top Bottom