Ndolanga chupuchupu kutandikwa na waumini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndolanga chupuchupu kutandikwa na waumini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Jan 7, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]NDOLANGA CHUPUCHUPU KUTANDIKWA NA WAUMINI[/h]

  [​IMG]
  ALIYEWAHI kuwa mwenyekiti wa Chama cha soka Tanzania (FAT) sasa TFF ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Muhidin Ndolanga jana aliponea kipigo toka kwa waumini wa Waumini wa Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa.  Tukio hilo lilitokea mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa ambapo kama si askari wa jeshi la polisi kumuokoa mambo yangekuwa mengine.


  Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika toka katika msikiti huo, ni kwamba Ndolanga ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya msikiti huo, alikumbana na maswahibu hayo mara baada ya kusoma taarifa ya kwa ajili ya kuwasilisha maamuzi yaliyofikiwa na Bodi ya Udhamini iliyokutana kujadili mambo mbalimbali ya msikiti huo.


  Imeelezwa kwamba kwa takribani miezi miwili viongozi wa msikiti huo wamekuwa kwenye mgogoro mzito ambao umewahi kufika kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa usuluhishi bila mafanikio.


  Tukio hilo lilitokea katika msikiti huo baada ya kumalizika kwa Swala ya Ijumaa ambapo inadaiwa Ndolanga, alisimama kwa ajili ya kuwasilisha maamuzi yaliyofikiwa na Bodi ya Udhamini iliyokutana kujadili mambo mbalimbali ya msikiti huo.


  Imeelezwa kuwa baada ya kuisoma taarifa hiyo, waumini wa msikiti huo, walipinga taarifa hiyo na kudai kuwa ni tofauti na matakwa ya waumini na ndipo waumini hao walipopandwa na jazba na kutaka kumpiga makonde kiongozi huyo.


  Hata hivyo Polisi waliwahi kumwondosha na kumkimbiza katika Kituo cha Polisi Magomeni.


  Taarifa zinaongeza kuwa, Baraza la Msikiti huo, lilimsimamisha Imamu Mkuu wa msikiti huo,Walid Alhad na wasaidizi wake wawili, Japhary Mohamed na Murshad Athman kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hakunusurika, katandikwa kisawasawa!
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee analeta uchakachuaji hadi misikitini, kweli jasiri haachi asili...

  Ila ni good publicity kwake kwani tulishamsahau...
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika Jasili haachi asili huyu ndie ndolanga yule watanzania waliepiga kelele yeye uku anakula bata.Leo kaibukia msikitini ama kweli laana ya Watanzania Kiboko,yani leo laana imemkumbukia ndani ya nyumba ya Mungu sasa itakuwaje manake uko ndiko kwenye imani ameenda kukuza migogolo ama kweli kuwa uyaone.Vipi Mikwaju aikutembea toka kwa maustaadhi kwa kuwa nyumba ya Mungu sio sehemu za upunguani wa kunganganiza migogolo kisa Mkwanja.|

  Kwa Mzee huyo maalufu na alwatani wa migogolo hiyo ni aibu kwake na kwa familia yake.Hata kama hausiki lakini kitendo chake cha kutajwa kwenye mahusianao hayo ya mgogolo bado ni aibu kwa kuwa sifa yake kwenye umma wa watanzania ni mbaya kwa kuwa imeegamia kwenye kiongozi aliyeshindwa na msimamizi wa mfumo mchafu wa chanzo cha maovu kwenye sekta ya mpira wa miguu Tanzania
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapa yeye alikua anazuia ufisadi msikitini hapo,kuna mchwa wanakula pesa za msikiti na misaada mbalimbli toka kwa wahisani wanaitumia kwa maslahi binafsi,ndolanga na kamati yake ndio wadhamini wa mali za msikiti,sasa alikua anatimiza wajibu wake,ya FAT ni mengine,lakini hapa yuko sahihi,wasiotaka kudhibitiwa ndio waliandaa magenge ya wahuni baada ya kuona anaingilia maslahi yao!Naelewa jamaa anaponzwa na historia yake pale FAT
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndiyo uzuri/ubaya wa hawa wenzetu. Kupigana bakora msikitini katikati ya ibada siyo news kabisa. Ni jambo la kawaida tu.
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hata upande huu mwingine inatokezea si unakumbuka yale mapanga ya arumeru au kule mwanga mzee msuya na mwenegoha,it happens!
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Yes, but rarely and when it happens it becomes news and goes directly to the headlines of various media. For the other side, it is just normal and indeed a common practice.
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yah!pia umesahau ni kwa kuwa huwa inachukua uhai wa watu kadhaa,haishii kutandikana bakora tu kama ya hawa waswahili!
   
 10. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndolanga nakumbuka enzi za FAT,duh kweli noma.Alikuja kung'olewa na Sumaye huyu mzee kule FAT,siyo?Sasa huko msikitini wameamua kumpa cheo tena?
   
Loading...