Ndodi:Wanaoponda dawa ya babu wana Wivu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndodi:Wanaoponda dawa ya babu wana Wivu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mary Chuwa, Mar 21, 2011.

 1. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Habari hii iliyopo katika gazeti la Mtanzania la Jumatatu machi 21,iliyoandaliwa na Shabani Matutu inasema.
  Daktari wa dawa asili wa kituo cha Haleluya sanitarium,Issack Ndodi amewaponda wachungaji wanaodai dawa za Mchungaji Mwaisapile ni za Kishirikina.

  Akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Juu,alisema tatizo la Askofu Zakaria kakobe na Mtume na Nabii wa kanisa la Efatha,Josephat Mwingira ni wivu wa kumuona mwenzao kapata dawa ya kutibu magonjwa sugu ambayo yalikuwa yameshindikana.

  Kakobe na wenzake walitakiwa kusema Amina kwa watu kupona kuliko kuanza kuonesha wivu wao na kumtaka azuiliwe.

  kitendo cha Kakobe kutaka kujua majibu ya Serikali kwa dawa hiyo inayotolewa kwa maombi haiwezekani kwa kuwa ina miujiza hivyo haiwezi kugunduliwa na vyombo vya kisayansi'' alisema.

  Alisema walichopaswa kusema ni kwamba wale wanaopona ugonjwa huo wawe wanatoa ushuhuda kwa kuonesha kipimo chao cha kwanza kinaonesha wameathirika na baadaye waoneshe baada ya kunywa kikombe na kupona.

  Kauli kama hiyo ilitolewa na Mhubiri Antony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako aliyesema kuwa dawa isiwekewe kipingamizi kwani Mungu ana Nguvu ;na anaweza kufikisha ujumbe kwa mtu asiyetegemewa.
   
 2. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  big up kwa kutambua hilo dk ndodi.
   
 3. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  ndodi wape neno.
  Mungu aliyaponya maji kwa kumwambia Musa akati kipande cha mti(magic tree) ama kwa kiswahil Mlonge na maji yalipona waisrael wakanywa na hawakufa wala kudhurika.(chimba kweny Kutoka)
   
 4. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kasoma upepo mapema huyu
   
 5. Muro

  Muro Senior Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Liberal ideas,big up Mwinjilisti Dk. Ndodi tutakuweka katika sala na wewe muujiza wako uje kama wa babu,uokoe kizazi sasa naamini kuwa Askofu Kakobe hana la ziada kumbe ni mtu wa fedha zaidi,ashindwe na alegee wale manabii wa uongo watajidhihirisha wazi kizazi hiki,hata amri ya mungu inasema "usitamani mke wa jirani yako wala ng`ombe wake wala chochote alicho nacho.sasa babu kuwa nacho imekuwa nongwa kwa Kakobe?au anatamani angekuwa nacho yeye ili aendelee kujikweza?.Tumewahi kumsikia mtu huyu akituambia kuwa ameoteshwa na mungu Mhe.Mrema angekuwa rais wa TZ wakati ule Mrema akigombea kwa tiketi ya NCCR,na mbona haikutokea?.pili Umeme hautapita juu ya kanisa lake mwenge,hivi umeme haupiti? na mengine mengi wana JF mnayajua matamko yake,hivi ni nani aliyempa hizo GUTS za kumshambulia mtumishi mwenzie wa mungu? je ni mungu mwenyewe au ni shetani? wana JF jaribuni kufikiri kidogo nani mwongo au mganga wa kenyeji ni Kakobe,Ndodi au Mwasapile? sasa nafikiri huu ndiyo muda muafaka wa kuwajua matapeli wa injili ni kina nani.
   
Loading...