Ndoa zetu na umiliki wa mali...kizungumkuti kingine!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa zetu na umiliki wa mali...kizungumkuti kingine!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Apr 27, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mijadala mingi ya ndoa imeangalia sana mambo ya mapenzi na tendo la ndoa. Haya yameonekana kuwa ndiyo chanzo cha mifarakano na matukio ya kutisha kwenye ndoa. Hata hivyo watu wamekuwa hawajadili masuala yanayohusu mali zinazomilikiwa na wanandoa. Matokeo yake ni vurugu tena nyingine zenye hatari pale inapotokea ndoa kwenda halijojo au kifo cha mmoja wa wanandoa (mara nyingi wanaume). Kuna mambo mengi yanatia wasi na kustua sana.
  1. Wanaume wengi wanalalamikia sheria inayowapa wanawake haki ya kumiliki 50% ya mali zilizopatikana kwenye ndoa
  2. Baadhi ya wanandoa wanakuwa na mali binafsi ila hawana ujasiri wa kuwaeleza wenzao na badala yake wanaziandikisha kwa majina ya ndugu zao. Mwisho wa siku wanaweza kutapeliwa au zinapotea pale ambapo mhusika anapofariki
  3. Hakuna uwazi katika baadhi ya ndoa kuhusu mapato na matumiz ya kila mwanandoa
  4. Tulio wengi tunashindwa kuandika wosia na hivyo kusababisha kizazaa pale inapotokea msiba wa mwanandoa (mara nyingi wanaume).

  Je, kuna ugumu gani kujadili mambo ya mali kwenye ndoa na kuweka kila kitu sawa?
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Dark City nitarudi..
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mzee hili suala la umiliki wa mali kwenye ndoa zetu linakuwa tatizo pindi unapokuta familia husika ni tajiri ni in my many cases ni kwenye familia zenye uwwezo
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Rudi tu dada Asha...Michango yako hapa ni muhimu sana!
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Halafu kitu kingine DC hatuna hulka ya kuandika wosia mapema tunasubiri pale tunapokaribia kufa au pale ambapo tupo mahatuti pengine unakuta unawaandikia wosia wakiisiajua watakusumbua uwaagawie mapema pia unaweza kukuta ndugu nao wako interested na mali zako
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika kama ni kweli ila tatizo la umiliki wa mali liko katika ndoa nyingi sana. Unakutata Baba ananunua viwanja hata 10 na kujenga nyumba ya kuishi bila kumshirikisha mama watoto. Na kwenye familia za kawaida huko kuna matatizo kibao. Wanaume bado hawaamini kwamba mwanamke anachangia kitu kwenye mali za ndoa akiwa house-wife.

  Nadhani tatizo hali liko kwenye ndoa nyingi bila kujali uwezo wa kiuchumi!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hilo ni kweli. Lakini kwa nini hatuandiki wosi? Na kama hatuandiki, wosia wa maneno unakubalika?
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni kweli DC wanaume wanakuwa wagumu hasa ikizingatia labda zile mali alizapata kabla hajao huyo mwanamke hapo ndio kazi ipo huyo mwanamke anaweza asihusishwe kwenye jambo lolote kikubwa hnakuwa ni inferiority complex kwamba yule mwanamke either anaweza kufanya kitu fulani akiandikiwa wosia (I have seen this happening) mtu anakwambia "Niwaandikie wosia je wakiniua kabla ya muda wangu ili wapate hizo mali" so kuna visa kama hivyo DC.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mimi naweza kusema ni hulka tuliyonayo tu hatuoni kama kuna umuhimu wa kuandika woria mapema ukifariki ghafla unaacha mtafaruku familia badala ya ku-mourn kifo chako wao wanaanza kupigana vikumbo kugombania mali zako.
   
 10. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Mzee DC shikamoo
  kwanza samahani kwa usumbufu mwingi
  na pili nashukuru sana kwa nimejifunza mawili
  matatu kuhusu ndoa kwenye ile thread..

  Nway hapa nichotaka
  kusemawatu wengi wenye mali nyingi
  huwa wanachukua prenatu agreement..
  hii huwa inasaidia kwa chochote kitakachotokea kwenye ndoa..
   
 11. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wengi hawapendi kujadili swala la mali kwasababu nyingi tofauti tofauti, mojawapo ni mtizamo kwa yule atakaye anzisha maada hii, mwanamke akianzisha ataonekana yupo ki maslahi zaidi, na mwanaume ataonekana amehisi kitu/anajihami Halafu kujadili swala la mali kwa wanandoa wengi inaonekana kama ni kutokuwa na uhakika wa ndoa kudumu kwa muda mrefu.. kwahiyo kila mtu anaogopa kuanzisha hii topic, Pia TUMESIKIA VIFO VYA WATU WENGI SANA AMBAO WAMEULIWA ILI KUHARAKISHA UTIMILIFU WA WOSIA(MGAWANYO WA MAHALI). ni mtizamo wangu tu! Ila hili swala la mali ni muhimu kuliweka wazi.
   
 12. N

  Nancy70 Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama upendo (Love) wa kweli haupo matokeo yake ndo hayo, mi sioni sababu ya kutomshirikisha mke wako ambaye kweli unampenda na si ajabu amekuzalia watoto, sasa unataka nini tena? Tatizo lao wanaume wengi hawajiamini na ni wadanganyifu...na wengi wa hivyo wanavimada na watoto nje ya ndoa maana anajua akimshirikisha mke kujua mali walizonazo mke ataanza kumonitor inflow na outflow ya mali walizonazo. Kwa hy ili ajiweke huru kwa ufedhuli anaoufanya anaona bora asimshirikishe mkewe. Na wengine unakuta hata baada ya kifo familia inaweza kosa kabisa maana biashara nyingine zinakuwa partnership mke anakuwa hana analolijua.
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sijui naandike wosia mapema nikurithishe ile hotel niliyojenga Hawaii
   
 14. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mimi nakurithisha deni la EPA! :A S 39:
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndo maana huko nyuma niliwahi kusema kuwa Watanzania wengi tena tulioenda shule tunasumbuliwa na ujinga wa kujua vitu muhimu sana katika maisha. Suala la mali zilizopatikana kabla ya ndoa liko wazi kisheri...Ni jambo la kuandika kisheria kuwa hazitajumuishwa kwenye mali za ndoa (matrimonial properties).

  Sasa kwa nini tunashindwa kujadili mambo ya mali wakati kila kitu kiko wazi?
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  AD,

  Hebu fafanua kidogo hapo kwenye red. Lugha imegoma!
   
 17. vena

  vena JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh...
   
 18. A

  Aine JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kuona jirani yetu mmoja alipofariki tu yaani muda huo huo bila kulia wala huzununi yoyote watoto wakaanza kukimbilia chumbani kwake na mwenye funguo akazificha ikawa badala ya kuomboleza ni ugomvi wa mali yaani hadi aibu mzee alikuwa na magari ya kutosha yanafanya biashara mbalimbali na nyumba kadha wa kadha, ilisikitisha sana na hakuna aliyetegemea kwa kweli, hao aslili yao ni Waarabu koko probably angeandika wosia ingesaidia
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Elia ahaa ahaa tukutane leo tujadili
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  DC nashukuru umeleta hii topic nimepata kitu cha kujifunza hapa ingawa bado sijaoa lakini mwelekeo ndio huko huko kwahizo najua itanisaidia kupata uelewa wa jambo hili.
   
Loading...