Ndoa za watu waliooana na wote wasomi wanaongoza kwa kuchepuka

Msemajiwao

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
619
1,513
Ukweli Mchungu, lakini ukweli lazima usemwe; Ndoa za watu waliooana wote wasomi kwa maana ya wote kila mmoja anakazi yake kwa utafiti wangu mdogo nimegundua kwamba nyingi Hazina furaha kama ambavyo watu wanafikiria, Nyingi zinaongoza kwa migogoro ya kimapenzi inayosabisha wanandoa kuwa na MCHEPUKO!

Udadisi wangu umeenda mbali zaidi kwa kuangalia pia ndoa za wale ambao wameoa au kuolewa na mme/ mke ambaye siyo msomi zinaonekana kuwa nafuraha zaidi kuriko ndoa za wasomi!

Ndoa za wasomi; nyingi zinaongozwa na sera ya "UKIMWAGA MBOGA, MI NAMWAGA UGALI" ,KAMA MBWAI IWE MBWAI n.k

Wapenzi wote ni wababe na kila mmoja ana jeuri,Kiufupi zimejaa malumbano na majibizano yasiyoisha kila siku yenye kumfanya kila mmoja anajiona mwamba kwa mwenzake.

Wasomi wanandoa ni wachepkaji kuliko kawaida sababu kuu ikiwa ni Semina na Vikao visivyoisha.

Wanandoa wasomi Mungu anawaona kwa michepuko yenu!
 
Ukweli upo kwa 99.9%, najua kuuthibitisha ni ngumu. Hii ya kuhoji hoji utafiti ni namna ya kukwepa Ukweli. Na Ndio sample hizo
 
Ukweli upo kwa 99.9%, najua kuuthibitisha ni ngumu. Hii ya kuhoji hoji utafiti ni namna ya kukwepa Ukweli. Na Ndio sample hizo
Police walivyoanza kukagua magesti watu walitokwa mapovu kupinga! Hajui ndio utafti wenyewe huo.
 
poor you...haya kaoe darasa la saba...utagongewa hadi uchanganyikiwe
Wazazi wako wameoana na PHD? Kama hakuna ..je baba ako tuambie hadi Leo yuko mirembe kachanganyikiwa...mbona wamedumu Kwa Aman hadi wewe umekuwa?
 
Back
Top Bottom