'ndoa' Za Vyuoni Zina Athari Zipi Kwa Mwanachuo?

Mchumia juani

Member
Jan 28, 2008
27
13
“………..nikiwa nimejipumzisha chumbani kwangu,chumba ambacho kipo mahali ambapo kwa lugha ya wenyewe tuyaita ‘Hostel’,ghafla mlango ulifunguliwa kwa kasi ya ajabu,akaingia rafiki yangu ,kabla sijauliza kulikoni alianza kufoka na machozi yakimtoka.”Najuta sana kumpenda ‘R’,Mapenzi yetu yalikuwa yanaenda vizuri,lakini mara tu baada ya kumaliza ‘University exams’ leo hii nimemkuta na yule jamaa yake wa zamani,yule……………”

Ni kawaida kwa kijana aliyefikisha umri wa kuamua kile anachoweza kufanya na nani na kwa wakati gani kupewa uhuru huo pasipo kuingiliwa kimaamuzi na mtu yeyote ilimradi tu sheria ya nchi inalindwa.Uhuru huu pia ni pamoja na uhuru wa kuchagua na kumpenda yeyote wa kupendeka kwa sababu zake mwenyewe,si unajua hiki ni kizazi cha ‘DOT COM’ yaani kizazi cha utandawazi,kizazi ambacho mzazi wangu aliyepo kijijini hawezi kunichagulia huko binti wa kuoa nikakubali,huu ndiyo ukweli halisi na lazima tukubaliane nao.

Kwa wanachuo, kama walivyo vijana wengine,na hata jamii na serikali wanalitambua hilo,wanao uhuru wa kufanya maamuzi yao wenyewe,si mnajua mtu wa ‘Diploma’ au ‘Degree’ ni mtu mkubwa kifikra na hata kiumri?.Hali hii imewapelekea wasomi hawa kuchukua maamuzi ambayo siwezi kuhukumu moja kwa moja kuwa ni mazuri au mabaya kwani nitakuwa nimeingilia uhuru wa vijana kufanya mambo ambayo pengine sisi hatuwezi kujua manufaa yake kwa tathmini ya haraka haraka.

Uhuru huu wa kimaamuzi umewafanya wanavyuo wanaoishi katika ‘Campus’ ama ‘Hostel’ waamue kuazisha mahusiano kati yao au na watu wengine wa nje ya pale wanapoishi.Ikumbukwe tu kuwa kuna mambo mengi sana yanayomzunguka mwanachuo hasa kayika maisha yake ya kimapenzi.Zipo sababu za kijana wa kiume mwanachuo kuwa na uhisiano na binti wa ‘mtaani’ ambaye si mwanachuo na zipo sababu pia kwa kijana wa kike mwanachuo kuwa na uhusiano na Mwanamume wa ‘mtaani’ asiye mwanachuo.Labda mambo hayo tutayaangalia kwa undani katika matoleo yajayo ya gazeti hili la Familia.Kwa leo tuangalie mahusiano ya kimapenzi kati ya wanachuo.Si unajua upendo hauchagui ili mradi tu umempenda wa kupendeka?.Mahusiano haya kati ya wanachuo,mengi kati ya aya yamezaa ‘Ndoa’ za haki hasa pale wanazuoni hawa wanapohitimu Degree na Diploma zao na kuingia mitaani lakini pia si mahusiano yote yanayodumu kwa muda mrefu na baadhi ya watafiti mbalimabali wamebainisha kuwa mahusiano haya yamechangia ‘kuporomoka’ kielimu kwa baadhi ya wahusika na hata wengine hushindwa kuendelea kabisa na masomo yao,sisi tunaita ‘Discontinuation’.Japokuwa inaweza kuwa ni asilimia ndogo tu ya wanaoshindwa kuendelea na masomo yao lakini lazima tutambue kuwa tayari serikali imewekeza kwa watu hawa kwa mamilioni ya fedha za mikopo wanayopewa.

Mtafiti mmoja aliyefanya uchunguzi katika vyuo kadhaa hapa nchini,alibainisha kwamba kati ya asilimia arobaini na tisini na saba ya wanachuo wako katika mahusiano ya kimapenzi ,na kati ya hao,asilimia hamsini hadi sabini wana mahusiano ya kimapenzi kati yao kwa wao na ni asilimia 0.5 hadi 2 tu ndio wanaodumu katika mahusioano hadi mwisho wa masomo yao chuoni na hatimaye kuoana kabisa.Si vibaya kabisa kuwa katika mahusiano ,suala kubwa hapa ni kuwa nini faida au hasara ya mahusiano haya hasa katika nyakati hizi za Ukimwi?

Mtafiti mwingine alibainisha kuwa kila mwaka takribani asilimia moja hadi tano ya mabinti wanachuo wanapata mimba.Baadhi yao hujifungua na kuendelea na masomo yao na wengine hatujui mimba hizo zinapoishia kwani hatimaye wahusika huendelea na masomo.Bahati nzuri ni kwamba hakuna sheria inayomzuia binti mwenye mimba chuoni kuendelea na masomo si unajua wengine ni wake za watu.

Faida kubwa zilizoelezwa za kujiingiza katika mahusiano haya zimetajwa kuwa ni pamoja na kupata misaada ya kielimu hasa mitihani inapokaribia na misaada ya kifedha hasa pale zile za mkopo ‘Boom’ zinzpoisha,kupata mwenza wa kukuliwaza na kukupa moyo hasa masomo yanapokuwa magumu na kupunguza ‘Academic stress’,kuepuka upweke(msononeko) na kusaidiana kumudu gharama za maisha ya chuo na wengine husema wanajiepusha na ukimwi kwa kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na Wengine husema hii ndiyo njia ya kumpata mke au mme ambaye mnafahamiana na kuzoeana kwa muda mrefu hasa ukiwa katika uhusiano imara.

Madhara makubwa ya mahusiano haya yamegawanyika kati ya wavulana na wasichana,japo kuna madhara ya jumla kama vile uwezekanifu wa kupata magonjwa ya zinaa,Chuki ‘hate’ kati ya wanachuo hasa pale wanapochangia bwana au binti na kuna ushahidi wa migogoro na mizozano kadha kati ya wanachuo ambayo mingi imehusishwa na kuchangia mpenzi kama chanzo.

Kwa wasichana mimba za mapema haziepukiki na japokuwa wengine wanavumilia na kuzilea mimba hizo hadi wakajifungua wakati huohuo wakiendelea na masomo yao kama kawaida,kwa wengine uwezekanifu wa mimba hizo kutolewa kwa wakati wowote hauepukiki hasa pale mhusika anapokwepa jukumu lake na hofu ya wazazi au wanachuo wengine kugundua.Mahusiano haya pia yamehusishwa na kuporomoka kielimu kwa mhusika hasa kutokana Stress na migogoro ya kimapenzi inapojitokeza wakati wa mitihani au mitihani inapokaribia,Kupoteza muda mwingi kulea mtoto hasa kwa wale wanaojifungua hayab yote yamepelekea kushuka kwa kiwango cha kufaulu kwa baadhi ya wasomi.

Kwa wavulana tatizo kubwa linalijitokeza ni kuishiwab fedha mapema kabla ya muda uliopangwa na Bodi ya mkopo kwani japo mnapata mkopo uliosawa mabinti wengi hubana fedha yao hasa wakati kupata chakula na kumuachia mvulana jukumu hilo ili waweze kupata fedha ya ziada kwa ajili ya saluni na mambo ya urembo si unajua dada zetu wa vyuo wanavyopenda kupendeza?.Madhara mengine kwa wavulana ni kuporomoka kielimu hasa mahusiano yanapovunjika.Kwa kawaida msichana anayekupenda ili apate msaada wa kielimu,uhusiano wenu huimarika pale mnapokaribia mitihani na hulegalega au hata kuvunjika kabisa mara tu mitihani inapoisha.

Matatizo yanayopelekea kuvunjika kwa mahusiano ambayo mmoja kati ya wapenzi alimpenda mwingine kwa dhati husababisha madhara ya kiakili na hivyo magonjwa kama ‘Depression’ au Post Traumatic Stress Disoder’ Hayaepukiki ambayo huweza kuwa na matokeo mabaya sana kwa mhusika.

Kwa mfumo huu wa maisha,maisha ya kila mtu kuamua nani wa kumpenda kwa wakati gani na wapi changamoto kubwa zinazoibuka ni kuwa nani awajibike? Wazazi ambao wako huko vijijini ambako ndiko wasomi wengi wanapotokea? Au Waadhiri ambao wajibu wao ni kutoa elimu ya ‘Degree’ au ‘Diploma’ darasani tu na sio elimu ya mahusiano?Je washauri wa wanachuo wanatimiza wajibu wao?Au ni jukumu la wanachuo hawa kutatua matatizo ambayo ni matokeo ya maamuzi yao wenyewe?.Tunaweza kujiuliza maswali mengi ambayo tunaweza tusipate majibu yake kwa haraka,labda tuwaachie hawa wasomi wenyewe kwa kuwa ni watu wazima kifikra na kimwili kuamua kusuka au kunyoa.Kwani kila mmoja anao uhuru wa kupenda au kutopenda na wanavyuo wanajua jema na baya.!!!!!!!!!

Tukutane wiki ijayo ambayo nitakuletea makala ya kusisimua zaidi.
 
wakati ule tunasoma tulizoe kuwaita ACADEMIC BUZZ
 
sasa hivi wanaitwaje?

lkn makala bomba imetulia, mtihani mkuu kuoa mtoto ambaye jamaa shule alikuwa akichapa na baadae ukajua. sijui maisha yanakuwaje hapo?

ila kuna wengi wanaogopa kuoa wasomi kwa kuhofia hayo
 
uzuri wa kuwa na rafiki wa kike mahari kama hapa ni kwamba mtu anajipunguzia vikwazo vya tamaa kwani mabinti wanavaa utadhani "stage show" wa R.Kelly ndani ya "burn it up"
bora uwe na mke wako ili utengeneze cheti safi kuliko kuishia kuwawaza hawa wasichana. hebu fikiria kule hostel unakwenda zako jioni kuchota maji halafu jinsi wanavyokuja pale bombani.
ukitaka kuweka maisha yako ya baadaye vizuri kuwa na wako.tengeneza GPA kwa raha kabisa. utasoma kwa raha ukiwa ume-relux moyoni kuliko kuhangaika na unstable heart.
ila hatari yake ni hii; most of the ladies now are looking for physical materials wealth. wewe ukiwa kipanga hiyo ni software therefore non physical materials; they dont care about you. unaweza ukawa naye kumbe yeye ameegesha lakini siku ya siku kajamaa kakija na usafiri hata wa kuiba ofisini kanachukua. unajua makampuni mengi mtu anaweza akawa anatoroka na gari kila siku jioni na kurudisha mapema. atakuchukulia tu kwani hao mabinti zenu siku hizi kwa magari hawana ubishi wowote.
utajikuta hiyo ndoa yako imekufikisha pabaya.
 
Yaani kweli vyuoni ndo kuna maambukizi ya ikimwi balaa! Unakuta jamaa ana mademu wawili wanaishi mabweni tofauti na kila demu ana buzi mtaani wa kumtunza!

Sasa hapo kama sii kuambukizana maradhi ni nini?
 
.......mabinti wengi hubana fedha yao hasa wakati kupata chakula na kumuachia mvulana jukumu hilo ili waweze kupata fedha ya ziada kwa ajili ya saluni na mambo ya urembo si unajua dada zetu wa vyuo wanavyopenda kupendeza?.....

MJ hapa umepiga ikulu kakake na as far as I know tatizo kubwa ndipo lilipo. Dada zetu wakishaona kiboom chako unakibaniabania (japokuwa nao wanapata sawa na sisi tu au zaidi) wanaamua kutafuta kibuzi kingine- kama sio mtaani, atalamba kichwa kingine hapohapo chuoni, hall tofauti tu!
Hivi dada zetu wanaona uvivu gani kuchangia bills za vyakula na vinywaji kwenye mitoko na partners zao? Na kwanini wengi wao hawajifunzi kuishi kulingana na kipato chao? kama hela hairuhusu kwenda salon,kwani ni lazima uende?- si unyoe au upige dreads!Hivi ni lazima suala la hela liingie katika mapenzi?
 
mzee nnakuamini ila hapa umeteleza.

maumbile mwanamke hupokea na mwanamme hutoa.

angalia mnapotenda tendo la ndoa nani anatoa na nani anapokea.

suala la ujauzito.

ukiangalia kimaumbile tena kote hata huko walikoendelea mwanamme lazima atoe na dem apokee sasa usikonde.

sawa na kutongoza mwanamme lazma aanze ila mara chache huwa kinyume sawa na mtu kuzaliwa na miguu mitatu ni mara chache na huenda ikawa ni maajabu
 
Unajua suala la vyuoni demu unaweza kuta ana weakness zake ktk somo fulani then anajirafikisha na mshikani alafu mshikaji anakuwa kazimia.Bila kujua motive ya uyu binti ni msaada wa kisomo tuu thats why baada ya chuo kila mtu na zake.

I had four of my friends mpaka sasa watu waliokuwa wenzi wao chuo wameolewa na mabwana zao as a result ata wachumba zao wa kale wamewatosa.Yaani unakosa mwana na mbeleko.

Niliapa kutokuwa na demu chuoni zaid ya kushika pembe na makamuzi ya apa na pale.Na atlast ikawork.Otherwise ukiwa na demu chuoni na hasa mkawa Course moja ata assignment zake utafanya na kudidimiza elimu ya uyu kiumbe na baada ya chuo hakutambui.
 
Hii mada ni yamsingi sana kwa wanafunzi walioko vyuoni.Suala la kumiliki mpenzi vyuoni ni hatari kubwa sana kitaaluma.Kwa waliosoma mlimani miaka ya nyuma watakubaliana na mimi kwamba kunamwanachuo aliwahi kujiua kwa ajili ya kutoswa na demu wa pale chuoni na kisa ni kwamba yule demu alipata njemba nyingine palepale chuoni.

Unajua iko hivi,ukimpenda sana huyo manzi,hataukiwa darasani lecture itakua haipandi wewe kichwani mwako utakua unamuwazia huyo demu wako tu.Hatari kubwa hutokea pale mwanaume unatoswa na kimwana ambae tayari umekwishaingia gharama kibao halafu unasikia kwamba jamaa mwingine ndio anakula uroda,hapo ndio shule inapotea kabisa.

Kweli mazingira ya wanawake wa vyuoni yanavutia sana ktk ngono,lakini mimi nilichofanya baada ya kuona mavazi ya hao mabinti ni hatari kwa shule yangu then niliamua kukaa mtaani na nilimaliza shule yangu vizuri.

TO AVOID UNECESSARY FRUSTRATION IN YOUR ACADEMIC ARENA DONT ENGAGE IN THIS BUSINESS
 
Mimi nilisoma SUA, siku zile wanafunzi wa kike wa chuo walikuwa wakiitwa "wasaigoni" na hall namba 5 lao liliitwa "saigoni". Wasichana wa nje ya wanafunzi waliitwa "Wagrovesu". Hili neno la wagrovesu lilitokana na kamapuni ya ku-supply vyakula pale chuoni iliyoitwa Wananchi Growing Vegetables and Supply.

Kwa sababu hizo hizo zilizokwisha jadiriwa hapo awali nilikuwa sihangaiki sana na "msaigoni" yeyeto. Sana sana katika kuweka "biological balance" vizuri siku moja moja nilitafuta "wagro". Mwaka wa mwisho nilipata "msaigoni" aliyenivutia sana lakini baadaye hako "kasaigoni" kalichukuliwa na Lecturer mmoja. Iliniuma sana lakini labda kwa kuwa nilikuwa mdogo kimaisha, kwa bahati nzuri nilimaliza salama. Leo najiuliza kama ningekaa miaka yote hiyo (4) chuoni na hali hii iliyonitokea mwaka wa mwisho sijui ningevumilia kiasi gani.

To cut the long story short, DONT ENGAGE INTO THESE THINGS WHILE ON STUDIES PERHAPS MARRY, ESPECIALLY WITH THAT DEADLY MICRO-ORGANISM, mengi ya mahusiano yanakuwa sio REAL. BUT A NICE EXPERIENCE.
 
mzee nnakuamini ila hapa umeteleza.

maumbile mwanamke hupokea na mwanamme hutoa.

angalia mnapotenda tendo la ndoa nani anatoa na nani anapokea.

suala la ujauzito.

ukiangalia kimaumbile tena kote hata huko walikoendelea mwanamme lazima atoe na dem apokee sasa usikonde.

sawa na kutongoza mwanamme lazma aanze ila mara chache huwa kinyume sawa na mtu kuzaliwa na miguu mitatu ni mara chache na huenda ikawa ni maajabu

Du? kweli we mtu wa pwani, mwinyi kabisaa, sitashangaa ukisema hutaki mkeo aende hata sokoni, wataka akae ndani tu!
 
uzuri wa kuwa na rafiki wa kike mahari kama hapa ni kwamba mtu anajipunguzia vikwazo vya tamaa kwani mabinti wanavaa utadhani "stage show" wa R.Kelly ndani ya "burn it up"
bora uwe na mke wako ili utengeneze cheti safi kuliko kuishia kuwawaza hawa wasichana. hebu fikiria kule hostel unakwenda zako jioni kuchota maji halafu jinsi wanavyokuja pale bombani.
ukitaka kuweka maisha yako ya baadaye vizuri kuwa na wako.tengeneza GPA kwa raha kabisa. utasoma kwa raha ukiwa ume-relux moyoni kuliko kuhangaika na unstable heart.
ila hatari yake ni hii; most of the ladies now are looking for physical materials wealth. wewe ukiwa kipanga hiyo ni software therefore non physical materials; they dont care about you. unaweza ukawa naye kumbe yeye ameegesha lakini siku ya siku kajamaa kakija na usafiri hata wa kuiba ofisini kanachukua. unajua makampuni mengi mtu anaweza akawa anatoroka na gari kila siku jioni na kurudisha mapema. atakuchukulia tu kwani hao mabinti zenu siku hizi kwa magari hawana ubishi wowote.
utajikuta hiyo ndoa yako imekufikisha pabaya.

Mmmh! Punguza hasira. Dizaini umekumbwa na mambo mengi sana katika sekta hii, jikune panapofikia tuu; anyway, for what is worth, pole sana! Next time find someone of your caliber, and you will never experience the heartaches and frustrations!
 
Yaani kweli vyuoni ndo kuna maambukizi ya ikimwi balaa! Unakuta jamaa ana mademu wawili wanaishi mabweni tofauti na kila demu ana buzi mtaani wa kumtunza!

Sasa hapo kama sii kuambukizana maradhi ni nini?

Statistics zinaonyesha ukimwi uko zaidi mitaani kuliko vyuoni!
 
Katika lile kundi nililokuwepo la B.A mlimani kipindi changu (B.A zote zilizokuwepo Faculty of Arts kipindi hicho na hata education), naweza kusema "couples" zilizokuja kuoana baada ya masomo ni chini ya 0.5%! Na wale mabinti waliokuwa "chakaramu", "haambiliki" kabisa baadhi yao wameolewa tukionana mitaani huwa wananichekesha sana, mmoja tulikutana mahali akaniambia "nyie si mlikuwa mnatuona hatuoleki eti hamtutaki, sasa nimeingia mtaani tu jamaa huyu! Tena kanijia kichwa kichwa! Nilaze damu? Ninaye, subiri utamwona sasa hivi!" Kufumba na kufumbua kweli jamaa akatokea, nikatambulishwa shemeji. Wameoana na wana watoto. Nikajiwazia tu kwa kweli kuwa ukimchunguze sana bata hutoila nyama yake!
 
Ni kweli kabisa.
 
Kwa kweli hii mada imenigusa sana. Maana nilipokuwa chuo nilikuwa na jamaa yangu mtoto wa mkulima pure kama mimi aliyeingia chuo na point tatu za A level! Harafu kibaya jamaa si alikuwa amesoma seminary? eee bwana jamaa first year si akapasua paper fresh, second year bwana jamaa akapata mtoto wa kitanga! Yarabhiiii...... Nyi acheni tuu jamani....kifupi ni kwamba jamaa alichanganyikiwa na well, alikuwa discontinued second year! It was a terrible story ambayo kwa kweli kila nikimuangalia jamaa leo mtaani, ilikuwa kama nuksi maana baada ya hapo ndo alikosa chuo kingine! si ndo biashara za cost sharing zikawa zimeanza? kwa hiyo akipata admission pesa hakuna! ...anyway jamaa ended up doing a diploma!

Kwa kweli mahusiano ya chuo kama wengi mlivyosema yana faida zake, lakini kwa mtoto wa mkulima ambaye ameingia mjini kwa mara ya kwanza na home hawana mbele wala nyuma, think twice before you register in that game! I would rather say it is not worthy it! Wengi wanachanganyikiwa kabisa. Ni mara mia uitwe mshamba wa kijijini kuliko kujiingiza kwenye vitu ambavyo vitakugharimu.
 
Lakini kuna wadada wanajua kubanana na haswa kumuweka mwanaume under rest,Nakumbuka wakati tunasoma nilishuhudia ndoa mbili mbili zikivunjika..yaani jamaa walianza chuo wakiwa wameshaoa na wameacha familia nyumbani wakakutana na wataalamu wa mapenzi yaani wanapikiwa na kufuliwa mpaka wakajisalimisha wenyewe.
 
hahahaah...duh kali hii
 
Back
Top Bottom