Ndoa za mkataba

zhi you nhi

Member
Dec 16, 2012
60
18
Jaman wapendwa hv swala la ndoa za mikataba mnalitazama kwa jicho gani?
My self napenda ndoa ya mkataba.....
vp kuhusu wenzangu mna maoni gani?
 
Kama wewe ni muumini wa dini nenda kapekue vitabu vya dini yako utapata jibu kuhusu ndoa za mikataba
 
kila m2 na apendacho wewe waweza penda lkn mwingine asipende na hakuna kisicho na faida kikakosa hasara ni nzuri pia kwa upande mwingine
 
Haukuwa mpango wa Mungu kuoa au kuolewa kwa mkataba. Hata Yesu alisema kuwa talaka zitatoka pale tu Uzinzi utapohusika vinginevyo ukioa mke aliekuwa wa mtu utakuwa unazini.............
Hii mikataba ni suala la ushetani

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
:confused2: The world is over flying, I can see ..................!:confused2:
 
Jaman wapendwa hv swala la ndoa za mikataba mnalitazama kwa jicho gani?
My self napenda ndoa ya mkataba.....
vp kuhusu wenzangu mna maoni gani?
wewe ni mchina?ujue jina lako linanishinda kulitaja
aisee ndoa za mkataba kitaalam tunaziita mutaaa
raha tupu miezi 3 watu8
miezi3@Asprin wana mmu na chitchat wotee unawapitia wapi mzabzab kuja huku:glasses-nerdy:
 
Last edited by a moderator:
wewe ni mchina?ujue jina lako linanishinda kulitaja
aisee ndoa za mkataba kitaalam tunaziita mutaaa
raha tupu miezi 3 watu8
miezi3@Asprin wana mmu na chitchat wotee unawapitia wapi mzabzab kuja huku:glasses-nerdy:

Rabeka rafiki...tutafunga yetu ya siku moja tu!!! nitakupeleka Puerto Rico tukasahau tabu zote za Tanganyika...

BTW: majina yake mawili ya mwanzo ndio ya Kichina, ila hilo la linaweza kuwa la kiVietenam, kiLaos etc.
Zhi - tamka kama Ji(lakini inakua nzito kama katamka Msukuma)
You - tamka kama ilivyoandikwa
 
Last edited by a moderator:
Hiyo habari ya mikataba ni uzinzi tu hakuna
lolote, hebu tupe sababu za msingi
zinazoanzia na herufi X na Q kwa lugha ya
Kiswahili
 
Mapenzi mara zote huwa yanaisha au kufifia baada ya muda fulani na yanapoisha ndipo wanandoa wanaanza kukwaruzana sana na hatimaye kuachana. Kwa hiyo kufikiria kuishi na mtu maisha yako yote na ambaye mtaboana tu ni changamoto. Hii inaweza kuwa moja ya argument za ku-support ndoa za mikataba. Hata hivyo ndoa za mikataba zina madhara ambayo yatahitaji miaka zaidi ya hamsini kuyashughulikia. Nchi za Scandinavia ni mashahidi wa hili. Nusu ya wakazi wa Sweden, kwa mfano, ni wahamiaji. Sasa niliongea na rafiki yangu Mswidi akasema imebidi nchi iangalie upya sera ya ajira na uraia kwa sababu ilifika mahali ikajikuta haina nguvu kazi. Wazee walikuwa wengi kuliko vijana na watu wa kufanya kazi viwandani wakawa hakuna, ikabidi iwe inapokea wahamiaji na wakimbizi wengi ambao wangeziba gap hilo (ukienda maeneo kama ya Tensta ni kama upo Somalia vile). Hii inatokana na ukweli kwamba walichezea hii taasisi ya ndoa. Kuna haja gani ya kuzaa na mtu ambaye una uhakika mtaachana baada ya miezi 6 au mwaka mmoja? Waswidi waliendelea kuoana na kuachana bila kuzaana kwa kipindi kirefu toka waliporuhusu flexibility kubwa kwenye ndoa (Si unajua kule wamama wapo juu na hawataki kubanwa???), sasa mpaka kufikia mwaka 2007 kulikuwa na watu milioni 9 huku milioni 4.5 wakiwa wahamiaji na wengi wa waswidi original wakiwa wazee. Sasa hivi kule ukizaa mtoto serikali inalea mpaka university, kila kitu bure. Kwa maana nyingine mtoto ni wa serikali wewe ni chombo kilichotumika kumleta hapa duniani. Na wanasera za chinichini za kulazimisha wanandoa kukaa pamoja muda mrefu na kuwashawishi wazae watoto wengi (Watoto wengi unapata hela nyingi za malezi toka serikalini). Labda tupitishe ndoa za mikataba ili kupunguza idadi ya watu wanaotokana na kuzaliana. Tujifunze kwa wenzetu, tusichezee ndoa. Tuache sheria zetu za ndoa kama zilivyo kwa sasa.
 
So na watoto nao wanakuwa wa mkataba, au? na je wazazi wako wangefanya hvyo ungekuwa wapi?
 
Fafanua kwanini unapenda ndoa ya mkataba na pia tujuze inakuwaje hiyo ndoa ya mkataba?
 
Neno ndoa linamaanisha ni watu wawili walioamua kuishi pamoja wakiwa mume na mke kwa muda wote wa maisha yao. Ukisema ndoa ya mkataba hiyo siyo ndoa ila mkataba wa kuishi pamoja kwa muda mliopanga. Kwa wakristo na waislam wanaamini kuwa ndoa ya kwanza ilifungwa na Mungu mwenyewe kwenye bustani ya Eden na vitabu vitakatifu havionyeshi kuwa hao wazazi wetu wa kwanza walikaa pamoja kwa mkataba ila tunajua waliishi pamoja siku Zao zote. Sasa wewe unaetaka mkataba umevutiwa na nini kama si tamaa inayokusumbua?
 
wamagharibi wamekula cereblum, cerebellum, medula oblongata, brain stem, spinal cord zetu...basi sie waafrika twakopi na kupesti...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom