Ndoa za makaratasi hizoooo!!!

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
354
MIAMI - The honeymoons are over for a 26-year-old woman who authorities say has at least 10 husbands.

Eunice Lopez has been charged with bigamy, accused of marrying 10 men between 2002 and 2006 without divorcing any of them, federal immigration authorities say. The Miami Herald reported Saturday that a records search by the newspaper found seven additional marriages under the bride's name and birth date.

Lopez arrived in South Florida from Cuba in 2002 and was a legal U.S. resident.

"I can tell you that none of the individuals she married had any type of residency," said Terry Chavez, a spokesman for the Miami-Dade office of the state attorney.

Prosecutors say she charged her husbands an unspecified amount to help them secure immigration status and continued asking the men for money long after the wedding, threatening to expose them if they didn't pay.

Chavez said the state attorney's office began investigating after being tipped off by Immigration and Customs Enforcement.

Lopez was released on $18,000 bond. Her last known address was in Hialeah, just north of Miami. A telephone listing for her could not be located, and it was not known whether she had an attorne

SOURCE-MIAMI HERALD.
 
Kama pale Bongo ambapo 100% hakuna any registered physical addresses then one can mary as many as possible.
 
Bongo zipo hizi lkn si nyingi..walitaka kuufanya wale wabunge wa CUF wakashtukiwa na wakafukuzwa Uongozi...

Jafar kinachofanywa wajue Jamaa si address tu..bali ELECTRONIC SYSTEM zao... kuweza register ndoa zote na vizaz na vifo..inawezekana wengi humu JF wameenda Nje ya NCHI kwa vyeti FEKI vya kuzaliwa...
 
Bongo zipo hizi lkn si nyingi..walitaka kuufanya wale wabunge wa CUF wakashtukiwa na wakafukuzwa Uongozi...

Jafar kinachofanywa wajue Jamaa si address tu..bali ELECTRONIC SYSTEM zao... kuweza register ndoa zote na vizaz na vifo..inawezekana wengi humu JF wameenda Nje ya NCHI kwa vyeti FEKI vya kuzaliwa...

Kuna kesi ya namna hii bado inaendelea pale Kisutu mahakamani, mwanadada "alioa" (ama kuolewa?)wanaume watatu. Shida ilikuwa katika kuwapa huduma, kwani alikuwa na udhuru usioisha wa kwenda "kwao", kumbe anaenda kwenye nyumba nyingine! Jamaa waligongana siku moja, baada ya mmoja wao kufuatilia udhuru huo usiokwisha, na kukuta kumbe ana nyumba nyingine, ndio wanaume hao wenza wakaamua kutatua kadhia yao mahakamani!
Haya mambo yapo sana tu hapa duniani!
 
Sio Marekani tu, hata uswazi hizi zipo. Soma hapa chini!
Mwanamke aolewa na wanaume wawili

2004-06-17 16:28:04
Na Mwandishi wetu


Mume wa pili kashtukia dili, alipofuatilia akakuta mume mwenza kajaa tele kama pishi la ubwabwaZawadi Kapambwe, Kibaha.

Ukisikia anja ya nyani kula hindi bichi, basi ni kama hii alivyocheza mwanamama huyu ambaye aliweza kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja na akawa anawafanyia zamu za kulala bila kugundulika.

Hata hivyo kama Waswahili wanavyosema kuwa njia ya mwongo ni fupi na siku za mwizi ni arobaini, basi mume wa pili wa mwanamke huyo ameshtukia dili hiyo hatari na kukimbilia kortini kutaka atenganishwe na mwanamke huyo laghai.

Sekeseke lenyewe liko hivi:
Miaka kadhaa iliyopita mwanamama Lucy Alfred
aliolewa kwa ndoa ya kanisani na mume anayefahamika kwa jina la Osmund Chiwalo aishiye huko Morogoro na kubahatikana kupata watoto wawili.

Baada ya ndoa waliishi kwa raha mstarehe na mumewe huku wakipanga hili na lile kuboresha maisha yao.
Lakini mara shetani mbaya alimwingia mwanamama huyo kichwani na akaamua kuukimbia mji kasoro bahari na kujitoma Bongo, kwenye Jiji lililojaa raha na karaha.

Baada ya kutinga Bongo, mwanamama huyo akanasa kwa Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania ajulikanaye kama A.K.Kamuhabwa.

Penzi likawa penzi na wawili hao wakakubaliana kufunga ngoa takatifu ili waishi maisha ya utimilifu ya mume na mke.

Baba wa watu bila kujua hili wala lile akaanza maisha ya ndoa na mwanamama huyo laghai ambaye alimwapia mzee kutowahi kuolewa wala kuwa na mtoto.
Sasa dili limebumbuluka na sakati kutinga kizimbani.

Mwanajeshi huyo ndiye amemburuza kizimbani mkewe akitaka talaka yake ili kila mmoja aanze kivyake vyake.
Kesi hiyo ya aina yake imefunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo Mkuza, Kibaha.

Mbele ya hakimu Andrea Sekimanga Mwanajeshi huyo amedai kuwa mwanamke huyo kabla ya kufunga naye ndoa alimwambia kuwa hana mume na wala hajawahi kuolewa.

Afande huyo akaendelea kusema kuwa lakini baada ya kuanza maisha yao ya ndoa, alishangaa mkewe safari za Morogoro haziishi.

Akasema alipomuuliza kulikoni kwenda Moro kila kukicha, mwanamama huyo akamfunga kamba kuwa huko kuna watoto wa marehemu dada yake ambao ameachiwa awatunze.

Hata hivyo Afande huyo akasema machale yalimcheza na kuanza kufuatilia ili kujua siri iliyojificha.
Akasema katika kufuatilia ndipo alipobaini mkewe kuwa na mwanamume mwingine tena waliyefunga naye ndoa na kuwepo kwa watoto wawili.

Mwanajeshi huyo akasema katika uchunguzi wake, alikwenda mpaka katika kanisa walilofungia ndoa ambapo alithibitishiwa na Padri aliyewafungisha ndoa kuwa mwanamama huyo ana ndoa halali.

“Baada ya kupata uhakika kuwa mke niliyemuoa ni mke wa mtu, nikamueleza na kumpa talaka ili arudi kwa mume wake lakini aligoma huku akieleza kuwa hawezi kurudi kwa mumewe wa kwanza kwa madai kuwa jogoo wake mgumu kuwika,” akasema afande huyo.

Akaendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kuona mkewe amegoma kurudi kwa mumewe, aliamua kumfungulia kesi mahakamani kwa kuhofia usalama wake baina yake na mume mwenza.

Baada ya afande huyo kumalizika kutoa maelezo yake na mwanamke huyo kupata nafasi ya kutoa maelezo yake, hakimu Sekimanga ametoa uamuzi wa shauri hilo.

Katika uamuzi huo amemtaka mwanamama huyo kurudi haraka kwa mumewe wa kwanza.
Hata hivyo mwanamama huyo aligoma kabisa akidai kuwa bwana huyo jogoo wake hawiki. Hoja hiyo hata hivyo iligonga mwamba.

Hakimu pia amempa ruksa mwanajeshi huyo kuoa mke mwingine wakati wowote atakapotaka.

SOURCE: Alasiri
 
Kuna kesi ya namna hii bado inaendelea pale Kisutu mahakamani, mwanadada "alioa" (ama kuolewa?)wanaume watatu. Shida ilikuwa katika kuwapa huduma, kwani alikuwa na udhuru usioisha wa kwenda "kwao", kumbe anaenda kwenye nyumba nyingine! Jamaa waligongana siku moja, baada ya mmoja wao kufuatilia udhuru huo usiokwisha, na kukuta kumbe ana nyumba nyingine, ndio wanaume hao wenza wakaamua kutatua kadhia yao mahakamani!
Haya mambo yapo sana tu hapa duniani!

Mkuu Idimi hii ni business, hakuna cha unyumba kwenye hiyo issue ya huyo mwanamke wa kimarekani, unafunga naye ndoa unamkatia chake, mkitoka kwa registrer mchezo umekwisha. UK naskia kuna watu wanatoa hadi £10,000 kwa hizi ndoa za makaratasi.
 
Mwanangu, hii ni ishu nyeti sana, kumbe mwanadada anafanya business ya kuwachukua washikaji makwao na "Kuwauzia" uraia? Hii kali sana. Nadhani hii ndio sababu iliyofanya baadhi za serikali majuu kuamua kwamba kabla ya kutoa kwa hati kamili za kudumu kwa wanandoa ambao mmojawappo si raia, lazima waishi kindoa si chini ya miaka saba! Baada ya hapo ndio huweza kuomba hati za uraia. Vinginevyo, mtaishi kwa ku renew vibali kila baada ya miaka miwili.
Kumbe kulikuwa na biashara ya namna hii?
Duh?
Nashukuru kwa taarifa hizi.
 
Back
Top Bottom