Ndoa za Kanisani Zifutwe , tuwe na ndoa za Serikali tu, mauaji mengi

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Nashauri Ndoa za Kanisani ambazo hakuna kuachana mpaka kufa zifutuliwe mbali na badala yake tuanze na tuwe na ndoa za mahakamani tu ambapo mkuu wa wilaya hapo bomani anawafungisha ndoa, na ni rahisi sana kuitengua ndoa hii.

Kwakuwa mauaji ndoani yameshika Kasi ,ambayo yanasababishwa na hizi ndoa za milele.

Sasa ni wakati serikali kufuta ndoa hizi Ili watu waoane kiserikali na Kama ikitokea kufumaniana basi ni rahisi kuachana kabisa, na Nina uhakika ndoa hizi zitapunguza vifo.
 
Wewe umeamua kumuasi Yesu Kristo basi utulie hivyohivyo. Miaka michache ijayo hautakuwepo tena duniani lakini biblia na maagizo yake yanadumu milele.
 
Nashauri Ndoa za Kanisani ambazo hakuna kuachana mpaka kufa zifutuliwe mbali na badala yake tuanze na tuwe na ndoa za mahakamani tu ambapo mkuu wa wilaya hapo bomani anawafungisha ndoa, na ni rahisi sana kuitengua ndoa hii.

Kwakuwa mauaji ndoani yameshika Kasi ,ambayo yanasababishwa na hizi ndoa za milele.

Sasa ni wakati serikali kufuta ndoa hizi Ili watu waoane kiserikali na Kama ikitokea kufumaniana basi ni rahisi kuachana kabisa, na Nina uhakika ndoa hizi zitapunguza vifo.
Jambo jema wanawake waishi mikoa yao na wanaume mikoa yao, kuzalishana kwa chupa.
 
Kwa vijana na wale wasiofaham utaratibu wa vyeti vya NDOA.

Kwanza cheti hicho ni mali ya serikali kabla hakijakabidhiwa mikononi mwako.

Mtu as sijui mchungaji nk lazima wawe na vigezo vinavyomfanya aende akasajiliwe kiserikali ili afungishe NDOA.

Kwa sababu serikali haina dini ndiyo maana kwenye cheti kuna segments zinabainisha aina ya NDOA unayoitaka as, mke mmoja, wake wengi, mitala, kikristo, kiislam au kimila nk.

So mchungaji, sheikh nk anapokwenda na kupewa hivyo vyeti anakwenda akiwa na muongozo wa imani yake ya mke mmoja, wengi nk.

Ukienda bomani urafungishwa NDOA kutokana na makubaliano yako na huyo mwali wako, as yeye tu au utamuongezea mwingine na kwa utaratibu mliopanga hapo kabla.

Mambo ya mkataba ni makubaliano yako na mwenzako, hicho kipengere labda kiwekwe sasa hivi.
 
Kufunga ndoa kanisani ni kitu cha HIARI, hakuna aliyelazimishwa . Kama hun uhakika funga ya bomani tuu
 
Ndoa gani hakuna kuachana!?..wakati binadam anaweza kuugua wakati wowote asiweze hudumia ndoa,au akiugua wazimu inakuaje!?
Kwamba ndoa ya wawili inapovunjika mbingu utetemeka! Siku zote nimeshindwa kuelewa kauli hii. Yaani wanandoa washindwane kutokana na tabia zao mfano mmoja wao au wote wawili kuwa fuska, jambazi, muuaji n.k. halafu ndoa ya watu hao inapovunjika eti mbingu itetemeke kweli? Shetani mwenyewe alipoasi huko mbinguni hatujaambiwa kama kulitokea tetemeko mbinguni.
 
Wivu wa kimapenzi unauhusiano wowote na ndoa ya milele?

Ina maana kwamba wanaofunga ndoa zenye uwezo wa kuachana muda wowote hawana wivu wa kimapenzi? Mbn nao tunaona wanauana kila siku.

Au mtoa mada ulitaka kutuaminisha nini ambacho unakielewa zaidi wakati wadau wengine wameonesha wana uwezo mkubwa wa kufikili zaidi yako.

Kwenye ndoa ya milele mkishindwana hamuachani ila kama mmeridhia wenyewe kila mtu anaendelea na mambo yake sio kama wewe ulivofikilia.
 
Kumbuka tu Swalha na Said ni waislamu talaka nje nje ila wakaishia kutwangana risasi.

Halafu mkijibiwa mnakua wakwanza kulalamika dini yenu inakashifiwa.
 
Back
Top Bottom