ndoa za bomani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,873
2,736
Majuzi jamaa yangu kahudhuria bonge la harusi ya rafiki yake. akanionyesha kadi ambayo ilikuwa matata kweli. nikasoma majina-mwanaume mkrisru na mwanamke muislam. nikauliza mbona bibi muislam? akaniambia ilifungiwa bomani. nina mashaka na hizi ndoa kwani kwa maana nyingine ni kuwa wanandoa wamekubaliana katika kutokukubaliana. na hili ni mbaya sana. kila mmoja mbabe hapo. ni sawa na kuahirisha matatizo ambayo yatafumka upya siku za mbeleni na kwa namna mpya. wadau mnasemaje
 
Si huwa wanadai wamekubaliana wao wenyewe na hivyo kupanga mikakati ya namna ya kuishi? though mara nyingi uamuzi huu hufanyika wakati ambapo si mmuafaka kwami wahusika huwa wanakuwa wamepofushwa na ile hali ya mapenzi kati yao so si rahisi kuona ugumu wa uamuzi huu.
 
Kweli ni kuahirisha matatizo, ila zipo. Na nyingine huwa for convenience tu.
 
Inategemea. Nyingine na ambazo zipo zimedumu bila matatizo. Kama kweli wamekubaliana itadumu, kama ni usanii wamezika bomu kwenye majivu wakasahau moto ukiwaka litajibu.
 
Kikubwa ni maelewano tu. Unaweza kuta hao wa dini tofauti(waliofungia bomani) wakadumu kuliko nyie wa dini moja. Penzi halina dini tuwatakie mema.
 
Ndo hizo ni makubaliano kati ya watu wawili wenye kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Kwa vile watu wengi tumelelewa kwenye misingi imara ya dini, tunaamini kitu maalum kama ndoa maishani kupata baraka mbele ya nyumba ya Mungu ni muhimu. Wengine wanakubaliana kubakia na dini zao kutokana na vizingiti fulani ila wanapendana na kuwa tayari kuoana.

Kubadili dini ili mfungie msikitini/kanisani au kutobadili dini na kuifungia bomani hakuchagui matatizo wala kudumu/kutodumu kwa ndoa maana matatizo hayachagui fungu la watu.
 
Ndoa bora ni ile ambayo wanandoa mko imani moja. Hata kama kutatokea matatizo chanzo si imani, ila hao wa bomani tatizo laweza kuanzia na imani au imani ikachochea tatizo jingine
 
Ndoa bora ni ile ambayo wanandoa mko imani moja. Hata kama kutatokea matatizo chanzo si imani, ila hao wa bomani tatizo laweza kuanzia na imani au imani ikachochea tatizo jingine

Ndoa nyingi zinazovunjika tatizo si imani,matatizo makubwa ya ndoa mara nyingi hua,usaliti,ubabe,kutopata mtoto,kukosa uwazi,ubinafsi na siku hizi limejitokeza lingine ambalo ni uchovu wa kiuchumi hasa kwa mkuu wa kaya.

Kwa hiyo tatizo likiibuka,watu hutumia dini kulitatua, ambapo sasa,mmoja anakuwa haelewi ni kwa vipi suluhu ipatikane kwa kufuata misingi ya dini asiyoijua. Nawasilisha hoja.
 
ni kweli, lakini ukweli ni kuwa kama mlikubaliana kutokukubaliana ni wazi kuwa hata mapenzi yenu yatakuwa na mashaka tu. tatizo huanzia watoto wanapozaliwa
 
Ndoa bora ni ile ambayo wanandoa mko imani moja. Hata kama kutatokea matatizo chanzo si imani, ila hao wa bomani tatizo laweza kuanzia na imani au imani ikachochea tatizo jingine

Ndoa nyingi huwa zinavunjika kwa matatizo mengine tu! Imani sio tatizo la kufanya watu wasiishi kwa furaha kwenye ndoa zao. Kama wanandoa wamekubalia kuishi kila mmoja na imani yake hapo hakuna tatizo kabisa.
 
ni sawa usemavyo ila ndoa za bomani hazina mvuto kijamii. watu watasherehehea tu lakini wafanyeje. ndoa ikishafungiwa bomani piga ua, lazima kuna walakini sehemu.
 
Back
Top Bottom