Ndoa yangu inateketea

Umeoa? Una ndoa? Una Watoto?? Huujui unachosema

Jamaa alichoongea namuunga mkono mm nimeoa lkn huwez niambia mwanamke anitushie kuondoka sijamkosea nimzuie kuondoka et kisa nimemuoa au kisa watoto hapana hata mm pia nahitaj sehem tulivu ya amani nyie ndio mnakufa kwa presha na msongi wa mawazo kisa tu unavumilia ujinga wa mwanamk sababu umezaa nae
 
Tatizo lilianzia hapo ulipooa ukiwa na miaka30 tu,,! huo umri bado sana kuwa na mke

Hapana hiyo haiwez kuwa sababu kwahy unaniambia ukitaka kuenjoy ndoa uoe ukiwa na miaka 40 hapo tatizo ni mwanamke huwez shirikisha umri wa jamaa kuoa na ndoa kikubwa swala la mke hapo ni km bahat kuomba Mola ajalie mke aliemwema na mvumilivu weng wao ni wapenda pesa tu ila ukifulia na yeye anakudump
 
Don't ever try to hold it!!.....Let her go


Wanawake WAPUMBAVU wenye mshahara, ukiwa umekwama kiuchumi ,ubongo wao huwaaminisha kua Wewe sio msaada tena kwao na Hivo anauwezo wa kujiendeshea maisha, na akipata Bwana mwingine wa kumsaidia basi atafika mbali..
Wanawake wapumbavu atataka muachane ili awe huru kwenye Bar, afanye matendo wanayofanya waschana...

Wanawake hawa wapumbavu, hawana Hofu ya Mungu.


Ninamjua mmoja, alifunga ndoa na Mumewe, bahati mbaya jamaa ni Injinia, hapa kati Kampun yao ilifilisika,,, Demu akachukua watoto na kuwapeleka kwao kwa wazazi wake..

Jamaa yake akaenda mkoa wa Jiran kuanzisha kakampuni..., Basi bwana huyu demu analiwaaa,, siunajua Ana Pesa ,magari n.k alafu umri miaka 33-35 , yaan mpaka juzi kati kaamua kuanza mchakato wa Kuvunja Ndoa.


Sasa unachopitia, ndo Jamaa anapitia. .


CHAKUFANYA....

Kama ni mimi, Ningehakikisha watoto nakua nao ,yaan niwachukue ( kama kiumri wako vzuri). .......huyo Demu wako ,akiwa nao, atawalishaga sumu kua wee ulikua mbaya mbayaa ulimtenda, watoto hawatokujua.


Pili, Ningeamua Kuachana naye bila hata kumwambia kua Ninakuachaa uendelee na yangu, UNGEMPOTEZEA ,UKIMPOTEZEA NA UKAPIGA KIMYA, UKIMYA NI SILAHA .

Tatu, ningendelea kujiboresha, kupambana, kutafuta kazi n.k , awe anasikia watoto wanakula, wanaishi vizuri, mnaenda kutembea nao, Yaan awe anakuona FB hukohuko kwenye mapicha picha.



Mwanamke ukishamzalisha watoto kuanzia wawili ,asikusumbue kwa kukoswa kwake akili.

Mwanamke ukishamzalisha watoto hasa wawili asikusumbue kwa kukosa kwake akili...


Asipokuelewa hapa basi tena.

Kuna wanawake wawili aina 2 wasikusumbue uliyemuoa halafu bado hamjapata mtoto na uliyezaa nae watoto wawili.

Usiwe loser mto mada
 
Habari wana JF wote kwa ujumla, bila ya kupoteza muda naomba kuja kwenye mada husika. Mimi ni kijana wa miaka 35,ndoa yanagu mpaka sasa inamiaka 5 tuu. Katika kipindi chote hichi tumeishi kwa furaha na upendo mkubwa tumebahatika kupata watoto 2.

Mke wangu ni mtumishi chuo kikuu(mwalimu)na mimi ni unga unga mwana pangu pakavu baada ya kampuni fulani ya mawasiliano niliyokua nafanya kazi kufungiwa na serikali kwa madai ya kukwepa kulipa na kuhujumu uchumi hivyo kesi bado iko mahakamani lakini sijawahi kukosa rizik japo kipato changu ni kidogo ila upendo na furaha viliendelea kushamiri.

KUANZA TATIZO
Mambo yalianza kua mabaya ktk ndoa yangu pale tuu mke wang alivyohamishwa kikazi na kuja hapa Dar ktk chuo kikuu fulani mwaka huu mwez 3 hivyo mimi niliendelea kubaki mkoni kwa lengo la kujipanga ili nihamie dar ili niwe karibu na familia yangu.

Ifahamike kua uhamisho wake haukua wa malipo kutokana na yy ndo aliomba kuhamishwa hivyo alipofika hapa Dar alifikia kwao maana yeye ni mzaliwa wa hapa dar.

Baada ya miezi 2 kupita mimi pia nikatoka mkoani na kuja hapa Dar,ila nilifikia nyumban kwetu kwa wazazi wangu (Mkuranga)
Harakaki za kutafuta nyumba zikaanza,kwa bahati mbaya wakati sijalipia nyumba nikafiwa na mzazi wangu(baba) chakushangaza mke wangu hakuweza kufika msibani kwa madai ya kukosa ruhusa kazini.

Sikua na neno maana bado nilikua kwenye majonzi,baada ya msiba kumalizika nilinza kujisikia homa kali na kulazwa hospitali,baada ya vipimo niligundulika ni Covid 19,

Mungu alisaidia nikaruhusiwa na kuendelea na matibabu nyumban. Wakati naendelea na matibabu mawasiliano na mke wangu yalikua ya tabu sana,simu za zilikua hazipaikan kwa madai mtoto wetu mdogo ameharibu simu yake hivyo ilinibidi niwe namtafuta mama mkwe kuongea na mke wangu

Hali ya kimawasiliano ilizidi kua mbaya zaid kadri siku zinavyozidi kusonga mbele,akawa hanitafuti,mpaka mimi nimtafute yeye, upendo wake kwangu ulikua umepungua sana kwangu. Maana hata kunijulia hali imekua vigumu kwake. Kibaya zaid alinza kufuta account namba yake ya wasapu na kuwa online kupitia Facebook nilivyomuuliza mbona nakuona online ushanunua simu nyingine?alinijibu kua ni ya ndugu yake wanaishi karibu pia namjua huyo mtu.

Nilimuomba namba ya simu anayoitumia ya huyo ndugu yake akanipa. Chaajabu sasa nikipiga ile namba anapokea muhusika wa ile simu na ananimbia yy yuko mbali kidogo na mke wangu.

Hii hali ilinishangaza sana kwan mda ambao nachat na mke wangu Facebook ndo mda huo nimepiga simu baada ya yy kunipa hiyo namba na kaniambia ndo anaitumia kwenye hiyo simu,

Niliendelea kuvumilia hii hali kwakua sikua na jinsi maana bado naendelea na matibabu. Hapa juzi kanitumia ujumbe kupitia Facebook anasema tuachane yy amechoka na maisha ya ndoa hivyo anahitaji kua single,haoni faida ya kua kwenye ndoa. Kwa kwel moyo wangu wote ulikua unawaka moto kwa maumivi makari sana

Kwakua bado naumwa halafu nakutana na changamoto kama hii. Ilinibidi nimtafute kwa kumpigia simu kupitia kwa mama ake akampa simu nikaongea nae.

Nilimuuliza kwan kipi kibaya ambacho nimekufanyia mpaka umefikia maamuz hayo ya kutaka tuachane?alinijibua kua yy amechoka na kudharauliwa hapo kwao maana inaonekama kama mimi nimemdamp tuu hapo kwao,

Nilimuuliza kwan hujui hali yangu ya kiafya kwasasa? Akanijibu kua anajua ila hayo ndo maamuzi aliyaamua kwan kichwa chake hakiko sawa,pia kazin kwake pia hajapandishwa mshahara hivyo hayuko sawa. Baada ya kuniambia hiyo alinikatia simu.

Ifahamike kua kipindi hiki chote ninachoumwa kaja kuniona mara moja tuu mpaka sasa ni mwez umekata hajaja kuniona.
Na mda huu yuko likizo haend kazin.

Naombeni ushauri wenu na mawazao nini nifanye kuinusuru ndoa yangu?hali yangu kiafya bado haija kaa sawa.ndoa inazidi kuniumiza msaada wenu tafadhali.
pole sana boss!!,,ila nakushauli jali afy yako kwanza ili upone huyo mamy alikupenda kat ukiwa na kaz halafu anajivunia hako kaelimu kake,,,kizur kabisa tayar umesha zaa nae,, ko tulia usimutafute wala kwenda pale kama utaenda nenda kusalimia wtt wako tu,,usiache kuwasalimia wtt hata kw sm enough!!ila in short hakuna mke hapo na ukilazimisha utakufa kwa pressure burs kat bado uko mdogo,, saiv huo ndo mda wa ww kujipanga kutafuta not vizur...
 
Kama tajiri wa dunia aliweza kuachwa na mkewe,kwako ni kipi kisichoweza kufanyika? Huyo mwanamke hakuwa pacha wako,zunguka dunia nzima tafuta pacha wako. Wengi tunalazimisha uhusiano kwa mtu ambaye sio pacha wako, matokeo yake ndio kuumizana kwenye mahusiano.
NB:
Pacha-ni mtu mnayeendana kitabia, kimawazo, kihisia n.k
 
Mkuu hatufahamiani, nakuomba ujiheshimu, na kama wewe ni mtu wa dini bas endelea na imani yako, nimeona mengi sana mpaka hapa nilipo, na katika watu wanaoongoza kwa unafiki ni watu wanaojifanya wameishika sana dini.

Hivi unajua watu wanavutwa kwa madawa kuhudhuria huko kwenye nyumba za Ibada(sio zote)?

Niishie hapa...
Maelezo yako yanaonyesha ni jinsi gani ulivyo mshirikina,acha mrudie Mungu
 
Anasema kazini kwake hajapandishwa mshahara!?.Hapo tatizo pesa,amechoka kukulea na kutimiza majukumu yako.
 
Pole mkuu.. kufanya maamuzi ukiwa too emotional hayatakuwa ya busara na ukajutia baadae.Chamuhimu kwanza afya yako..Kipindi unarecover,tumia muda huo kujipa break naye(kwa makubaliano ya pande zote)Naamini haka kamuda kakutafakari katakujana maamuzi mazuri kwa faida ya pande zote

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Hawa wanawake wapo wa aina mbili
1. Anayekupenda wewe km ww. Hapa uwe na hela au hauna bado mtakuwa naye
2. Wanawake wanaopenda vitu. Ukiwa na pesa mtakuwa naye, ila siku ukiwa hauna unakuwa mzigo kwake.
Mwanamke uliyenaye ni huyo type ya pili. Km unampenda na unataka mrudiane. Tafuta pesa atarudi mwenyewe. Tofauti na hapo huwezi kumrudisha.
Nashukuru kwa kunifariji mkuu,yaan kumpoteza mtu uliyemthamin na kushea mambo mengi inaumasana
 
Hawa wanawake wapo wa aina mbili
1. Anayekupenda wewe km ww. Hapa uwe na hela au hauna bado mtakuwa naye
2. Wanawake wanaopenda vitu. Ukiwa na pesa mtakuwa naye, ila siku ukiwa hauna unakuwa mzigo kwake.
Mwanamke uliyenaye ni huyo type ya pili. Km unampenda na unataka mrudiane. Tafuta pesa atarudi mwenyewe. Tofauti na hapo huwezi kumrudisha.
Well said! But jamaa has to move on, asisumbuke kutafuta pesa kwa ajili ya kumridhisha huyo chui aliekua kavaa ngozi ya kondoo..

Hapo MUNGU amsaidie apone kisha apate machungu ya kutafuta PeSA ajiimarishe zaidi kiuchumi asipoteze muda wa kumfikiria tena huyo mwanamke. Atakuja kupata mwingine tu wa kukubaliana na hali yake wakati wote.
 
Bro unatafuta nini kaka!! maisha haya yana muda na hua tunapata funzo, Mungu yupo kuwa karibu nae sana kipindi hiki, tafuta kazi taratibu walau ya kukupa riziki, sali sana, usikate tamaa, sali sana, kuna kitu kikubwa Mungu amekiweka mbele yako, usimlilie mwanamke kwa tamaduni zetu za kiafrika ni mbaya, si uanaume, najua kwa hizi stress za sasa huwez kua na hisia na mwanamke, tulia tafuta kazi!! hayo unayopitia ni ya Muda, Mungu akusaidie!!
 
Daah hapo kikwazo ni wewe kukosa pesa, pole sana mkuu, hapo mke huna piga goti chini muombe mungu atakufungulia njia
 
Ndugu yangu japo mimi mwenyewe sina experience kubwa sana na ndoa ila kwa kusoma hili andiko lako kuna mambo kadhaa nimefikiria na pengine yanaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Kwanza binafsi naona kama kuna shida au jambo ambalo L imefichika kwenye ndoa yenu na jambo hilo inabidi uanze kufikiria tangia kuanza kwa mahusiano yenu hadi maisha ya ndoa kwa kipindi chote ambacho mmekuwa pamoja. Kuna kitu ambacho kama ukiuunganisha vipande vidogo vidogo vya mahusiano ya ndoa utakuja kukipata.

Pili kushaurisha mtandaoni siyo mbaya ila binafsi ningeshauri ungeanza kwa wazee kwanza, ikiwezekana familia yako na yake zikae pamoja, mazungumzo yafanyike naamini palipo wazee hakuna kinachoshindikana na hapa ikishindikana basi huyo mwanamke atakuwa siyo sahihi kwako

Tatu kama mlifunga ndoa kanisani au Msikitini siyo mbaya pia kama ukiweza kupata ushauri kutoka kanisani au msikitini. Inawezekana huyo mwanamke amedanywa na kitu kidogo ila kama mazungumzo yakifanyika anaweza kujirudi na mkajenga ndoa yenu.

Mwisho nakushauri utumie hekima, busara na akili yako yote ktk kufanya maamuzi maana ndoa inapovunjika wahanga wakuu huwa ni watoto ambao hawana hatia.

Nakuombea na nakutakia kila baraka na Neema ya Mungu ktk hili ndugu yangu.
 
Ukweli ni kuwa asilimia75 ya wanawake wenye ajira, wakishapata watoto wawili au watatu Ila hasa wawili wanapenda kuishi na watoto wao tu ili wawe huru,
Ili mume uvumilike ukubali kuwa Mjinga mjinga kwa mkewe Kama ushauri alio utoa mwijaku kwa pett .
 
Mtu kaamua had kuama mkoa ..huyo alijiandaa shekhe..na chanzo ni ngawila

Yaan ishu ni huo upangu pakavu..

Ndio maana mim nawatindua vibaya mno na kuoa sioi ngoo...wacha wanichune tu..ila kuoa wasahau..ni mwendo wa kuwazalisha na kuwaacha tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa unamkomoa nani? Wenzio wanakuchuna, hata ukiwazalisha matumizi unatoa. Hapo hujawakomoa.
 
Kama tajiri wa dunia aliweza kuachwa na mkewe,kwako ni kipi kisichoweza kufanyika? Huyo mwanamke hakuwa pacha wako,zunguka dunia nzima tafuta pacha wako. Wengi tunalazimisha uhusiano kwa mtu ambaye sio pacha wako, matokeo yake ndio kuumizana kwenye mahusiano.
NB:
Pacha-ni mtu mnayeendana kitabia, kimawazo, kihisia n.k
Hakuachwa, aliacha. Elewa!
 

Similar Discussions

37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom