Ndoa yangu imekuwa mwiba, nisaidieni jamani

Tulia na mumeo wewe mwanamke....acha kuhangaika majukwaani huku....ukaishia kutongozwa na wenye akili Kama zako, upeleke magonjwa kwenu....acha ujinga.
 
Sija aribu mkuu
Hivi unakaa na mwanaume wiki,mwezi hakugusi kwani we dadake?
Au huyo mwanamke hana hisia yy cyo binadamu?
Mambo mengine wanaume mnasababisha bob.
Sawa ilaa kumbuka nae akitoka nje atanogewa asa nan atamtibu nan kama wote watakua wagonjwa ndan ya nyumba
 
dawa yake ndogo,kwa kuwa unalala na unakula vzur,we mpotezee,ikibidi mtafutie mjanja wake,
 
Hayo malalamiko kama yanafanana na ya mke wangu, ingawa mumeo kidogo amenizidi.Anyway nitajitahidi kujirekebisha.
 
Habari zenu wana JF,

Mume wangu hajaniomba papuchi miezi mitano now, siku hizi amekuwa bize sana na kuchati katika magrup ya wasap kiasi kwamba hana hata muda wa kuongea either na mimi au mtoto anakaa sebuleni mpaka saa 7 usiku akija room anakuta tulishalala na mtoto saa nyingi. Then Siku nikimgusagusa anageukia ukutani anajifunika gubi asubuhi anaanza kusema oh kichwa kinauma Mara alijisika tumbo linauma yani kama anaua soo hivi.

Niliwahi kumkuta na msg za mapenzi akadai kwamba mimi ni mpekuzi nisimfwatilie kuanzia hapo kaweka simu zake zote password.

Kwa kifupi kawa mkorofi ukitaka kuchat naye anakujibu short hataki maongezi marefu, imefika akitaka kusafiri hata hakuambii utasikia tu anakwambia Leo nitaenda South. Ndoa yetu ina miaka mitatu now lakini nina miaka miwili sijaitwa jina zuri kama mpenzi mke wangu nk achilia mbali kuwa mimi namwita majina mazuri, namfulia, nampasia,nampakia vizuri nk.

Amekua mbinafsi shoping anafanya yake tu na mtoto mimi hata bodyspray hakuna wala hela ya matumizi haachi kwa kuwa ananipa laki na nusu kila mwisho wa mwezi ninunulie kila kitu.

Mimi ni mwanamke mzuri, nina hofu ya Mungu na elimu ya degree ndoivyo tena ajira hamna, nikimwomba hela ya mtaji nifanye biashara anasema hana hela na wakati hela anazo tu na mimi naziona.

Nianyaje ndugu zangu naumia sana kwani tulipendana sana na tulifahamiana vizuri miaka mitatu kabla ya ndoa. Je niachane na hii ndoa nikaishi tu kivyangu maana nimechokwa vibaya kiasi cha kukata tamaa sasa.

Asanteni naomba ushauri utakaobadilisha haya maisha yangu.
Pole sana, muombe Mungu akutatulie tatizo lako
 
Zamani sana,na wajukuu ninao
Ushauri wako ulinitia mashaka hata ivo nna wasiwasi na majibu ila kifupi ulivosema nitofauti ukiwa ktk ndoa unaweza jishughulisha mwanamme akaacha kukupa matumiz kabsaa apo kinachotakiwa ni suluhisho la maelewano amani iludi ndani ya nyumba ndo masikilizano na mengine yatafuata
 
Dada yangu pole sana , najua situation ur in na jinsi unavyojisikia, nakuomba sana anza kumuombea ni ngumu najua lkn husije ukaacha kumwombea na kuzidi kumpenda pamoja na hayo mapungufu..mwambie kwa upole kuwa wote hao waliopo watapita ila wewe ndio mke wake na ya kwamba utatoa hesabu husiposimama na kumwambia ukweli, am sure atajisikia vibaya na siku utaona anabadilika MUNGU akupe neema ya kuvumilia na kumpenda zaidi..Ubarikiwe sana
Ni ngumu kumpenda mtu asiye kujali.Tafuta mtaji au shughuli yoyote ya kukuingizia kipato, heshima itarudi then mtaweza kuzungumza juu ya ndoa yenu mkiwa on that level. Kwa sasa wewe huna ujanja ni wakubembeleza tu, unabaki kuomba msamaha bila kujua kosa. Muoneshe kuwa unao uwezo wa kusimama mwenyewe ila tu unachaguwa kusimama nae kwa kuwa unampenda na vinginevyo. Heshima ndio kila kitu mkuu.
 
Pole my dear...
Huo umekuwa ugonjwa mkuu kwenye ndoa nyingi.
Jitahidi kusali sana hiyo situation ni ngumu sana ila the only hope ni prayer
 
Back
Top Bottom