Fugwe
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 1,676
- 656
Nahitaji ushauri wenu wanaJF,
Ndoa yangu ina umri wa miaka 21 na mimi mwenyewe nina umri wa miaka 46. Katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto 3. Mke wangu yeye ni mjasiria mali (siwezi kusema ni mama wa home) kwani anasimamia vijimiradi vya familia na mimi nimwajiriwa wa seriakli. Katika maisha ya ndoa mimi kama baba nimejenga nyumba 2, nina usafiri mzuri magari 3, nina mashamba 2 ya nguvu na vimifugo kidogo si haba. kati ya hivyo vyote hakuna senti iliyotoka mfukoni mwa wife. Nyumbani kama mnavyofahamu kuna facilities za kumuwezesha wife aihudumie familia kwa urahisi, kule kitchen kila kifaa cha kurahisisha mapishi kipo.
Sikilizeni tatizo lilipo, kama mnavyojua sahani zikikaa pamoja lazima zigongane, sasa ikitokea kutoelewana wife hawajibiki kwa maana sipikiwi chai, hakuna kusimamia mafundi na vibarua wataachwa wachakachue wapendavyo, achilia mbali tendo la ndoa ambalo lazima nisahau. Kaenda mbali ndugu kawaambia ninavyomnyanyasa nao bila kuuliza wameungana naye. mambo hayo ni karibu miaka 5 na zaidi hakuna maelewano ndani ya nyumba. Labda nijisemee na mimi, kweli najijua nina hasira lakini pamoja na hayo kwa miaka yote hiyo 21 ya ndoa sijawahi kunyosha mkono kumpiga wife, kurudi nyumbani usiku sio tabia yangu, sina mtoto wa nje wala small house na sijawahi lala nje hata siku moja. Nilikuwa nikipokea mshahara namkabidhi, then naomba hela ya matumizi lakini yeye hela inayopatikana kwenye vijimradi vyetu sijui inatumikaje.
Hatua tulizochukua kujaribu kupata muafaka, sisi wenyewe tumekaa several time hakuna kusikilizana ikabidi tushirikishe family friend tunakaa kidogo yanajirudia, ndugu wa pande zote wamejaribu hakuna muafaka, Hali iliyopo sisi wenyewe hatuwezi tena kuyamaliza ingawa ndio tulikuwa na dhamana ya kuyamaliza.
Nipeni ushauri, ni-sacrify kila kitu niondoke zangu? maana naona uchungu eti tugawane mali wakati najua nina madeni bank kwa ajili ya mali hizo ambapo yeye hakuchangia achilia mbali usemi wa sasa hivi kwamba mali ya ndoa ni ya wanandoa wote. Nitafute small house maana tunda nimeshanyimwa takribani mk2 sasa. Nisiwachose, maoni yenu tafadhali