Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Ningeomba kusisitiza tena kwamba hupaswi kuwa mtumwa wa mwanamke au mwanaume. Leo hii kuna wanawake na wanaume ambao maisha yao ya ndoa yamekuwa ni jela zao wenyewe. Wanaume na wanawake hawa wamekuwa wakiishi kama vile roho zao ni hao wanaume au wanawake.
Bahati mbaya ni kwamba ndugu na jamaa wa wanaume au wanawake hao huwa wanadhani kwamba ndugu zao wamelogwa na wanawake au wanaume hao wanaowageuza watumwa wao. Je unajua kwamba kuna wanaume hapa nchini ambao huwa wanatambulishwa kwa mahawara wa wake zao wakidai kuwa hao ni kaka zao binamu wakati sio kweli, na wakati mwingine hulazimishwa na wake zao kutoa misaada ya kifedha kwa hao makaka binamu feki?
Je unajua kwamba kuna wake wa ndoa ambao huwa wanaletewa na wanaume zao mahawara wa wanaume hao kila wakati na kutambulishwa kwao kwamba Huyu ni hawara yangu na bado wake hao wakanyamaza na kuendelea kuwaheshimu waume zao? Wapo, tena wengi kuliko unavyoweza kuamini wewe.
Basi kwa taarifa yako hakuna uchawi wala limbwata katika jambo hili, bali kuna utegemezi wa kiakili na hata kimwili. Mwanamke au mwanaume anafikia mahali ambapo anaamini kwamba akiachwa au kuachana na mke au mume aliyenaye hataweza kuishi kwa amani tena, hatamudu kamwe kuishi bila kumuona. Wengine wanaamini kwamba wakiachana na waume au wake hao hawatamudu maisha peke yao. Huu ni utegemezi mbaya kuliko sumu inayouwa haraka.