Ndoa yako mwenyewe ikupeleke kaburini!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Ningeomba kusisitiza tena kwamba hupaswi kuwa mtumwa wa mwanamke au mwanaume. Leo hii kuna wanawake na wanaume ambao maisha yao ya ndoa yamekuwa ni jela zao wenyewe. Wanaume na wanawake hawa wamekuwa wakiishi kama vile roho zao ni hao wanaume au wanawake.

Bahati mbaya ni kwamba ndugu na jamaa wa wanaume au wanawake hao huwa wanadhani kwamba ndugu zao wamelogwa na wanawake au wanaume hao wanaowageuza watumwa wao. Je unajua kwamba kuna wanaume hapa nchini ambao huwa wanatambulishwa kwa mahawara wa wake zao wakidai kuwa hao ni kaka zao binamu wakati sio kweli, na wakati mwingine hulazimishwa na wake zao kutoa misaada ya kifedha kwa hao makaka binamu feki?

Je unajua kwamba kuna wake wa ndoa ambao huwa wanaletewa na wanaume zao mahawara wa wanaume hao kila wakati na kutambulishwa kwao kwamba “Huyu ni hawara yangu” na bado wake hao wakanyamaza na kuendelea kuwaheshimu waume zao? Wapo, tena wengi kuliko unavyoweza kuamini wewe.

Basi kwa taarifa yako hakuna uchawi wala limbwata katika jambo hili, bali kuna utegemezi wa kiakili na hata kimwili. Mwanamke au mwanaume anafikia mahali ambapo anaamini kwamba akiachwa au kuachana na mke au mume aliyenaye hataweza kuishi kwa amani tena, hatamudu kamwe kuishi bila kumuona. Wengine wanaamini kwamba wakiachana na waume au wake hao hawatamudu maisha peke yao. Huu ni utegemezi mbaya kuliko sumu inayouwa haraka.
 
Thanks for usefull post

Nimekereka sana wiki hii, nimemshuhudia ndugu wa rafiki yangu akifanyiwa vibweka na mkewe wazi wazi, lakini jamaa yupo tu......... na kila siku haishi kulalamika kuwa mkewe anamtenda visivyo............... Mtu mzima na akili zake timamu anashindwa kuchukua maamuzi anabaki kulalamika .....................!!!!!!
 
I hope this will not happen to my expected marriage!

Ni vyema ikawa hivyo kama utaamua kuishi kama mwanadamu aliyekamilika................. lakini ukitegemea kukamilishwa na mwingine....... You will be in trouble...........
 
Duuh mbona tunatishana kuingia huko kwenye ndoa, kwamtindo huo mbona watanishkia bakora kuhusu kuoa..
 
Hawa wako wengi sana tena sana, na wanaita eti upendo!Shame on us!Pia kuna udhaifu wa kijinga unaoitwa wivu nao umehalalishwa siku hizi!Onother problem!
 
Nimekereka sana wiki hii, nimemshuhudia ndugu wa rafiki yangu akifanyiwa vibweka na mkewe wazi wazi, lakini jamaa yupo tu......... na kila siku haishi kulalamika kuwa mkewe anamtenda visivyo............... Mtu mzima na akili zake timamu anashindwa kuchukua maamuzi anabaki kulalamika .....................!!!!!!

Kabla ya kuja hapa jamvini ulimsaidia vp kamanda wako??
 
Ni vyema ikawa hivyo kama utaamua kuishi kama mwanadamu aliyekamilika................. lakini ukitegemea kukamilishwa na mwingine....... You will be in trouble...........
Huo ndio ukweli halisi... Mtu akiishi kama aliyekamilika atajiamini no mata what, na siku zote anayejiamini yupo huru!..
 
Kabla ya kuja hapa jamvini ulimsaidia vp kamanda wako??

Nimejitahidi kila namna kumsaidia ili auone ukweli, lakini nikimaliza kuzungumza naye anakwenda kumweleza mkewe yote tuliyoyazungumza, akimtaka ushauri!........ Mke huyo huyo akutese na huyo huyo akupe ushauri mzuri wa mustakabali wa ndoa yenu! ujinga gani huu.........

Unajua, Sizinga, mtu kutoka katika utumwa wa ndoa atake mwenyewe, na hata mimi wala sikujipeleka kiherehere kumshauri, bali alijileta mwenyewe kwangu akitaka nimsaidie, baada ya kuzungumza naye kwa muda mrefu tulikubaliana afanye mambo fulani...........ili kuboresha ndoa yake, lakini cha kushangaza, MKEWE KANIPIGIA SIMU AKINILALAMIKIA KWAMBA NATAKA KUMVUNJIA NDOA YAKE.............MH!!! nilimwambia wayamalize wenyewe na wala wasinihusishe kabisa.
 
Back
Top Bottom