Ndoa ya Pili ni Ndoa bila kuvunja ya Kwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa ya Pili ni Ndoa bila kuvunja ya Kwanza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 24, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hili linahusu ndoa halali iwe ya Kikristu au ya Kiislamu au kimila na kiserikali. Mtu unapoenda kufunga ndoa na mtu unatarajia kuwa yule mtu mwingine hayuko kwenye ndoa nyingine halali - aidha alikuwa kapera au kaachika, au mwenza wake amemtoka. Na pale ambapo mtu yuko kwenye ndoa nyingine (kama katika Uislamu) ni haki yako kujua kuwa huyu mtu yuko kwenye ndoa nyingine.

  Masharti ya ndoa zote yalikuwa yanataka kuwa kama mtu anataka kufunga ndoa nyingine (kuongeza mwenza) basi ni lazima apate ridhaa ya mwenzake - kama katika Uislamu.

  Endapo inatokea kuwa mtu unafunga ndoa ukiamini kabisa kuwa mwenzako hana ndoa nyingine, na sherehe ikafanyika, pilau likaliwa na saini zikadondoshwa kwenye vyeti vya ndoa na mashahidi wakawepo halafu baada ya mwaka mmoja wa mapenzi na hata watoto na mali za "ndoa" ikaja taarifa kuwa wakati unafunga ndoa mwenzio alikuwa na mwenza halali wa ndoa sehemu nyingine ya nchi;

  a. Je ndoa ya pili (bigamy) ni halali?
  b. Wakati mnafunga ndoa ni nani alikuwa na haki ya kudisclose kwa mwenzake kuwa alikuwa tayari kwenye ndoa nyingine?
  c. Je vyote vilivyofanyika katika "ndoa" ya pili vyaweza kuwa mali ya 'ndoa'?
  d. Baada ya kupewa taarifa kuwa uliingia kwenye ndoa wakati mwenzio alikuwa kwenye ndoa nyingine ambayo nayo ilikuwa akiihudumia - zile safari za hapa na pale kumbe ni kwa mke/mume mwenza, ukaamua kutoka kwenye ndoa hiyo na kutangazwa iwe annulled utalaumiwa kuwa "hukufanya due diligence" ya kujua kama mwenzio alikuwa katika ndoa nyingine? ni kosa lako kutokujua!?

  Ni maswali ambayo yanatukabili kwenye suala la Richmond, Dowans, na Tanesco!
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Slaa anaweza kulijibu vizuri zaidi.
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Slaa hana uzoefu wa kuoana au kuoa mke wa mtu; bali ana uzoefu kuishi kinyumba na hawara ambaye ni mke wa mtu. Kwa mantiki hiyo ndugu Kibunango uko nje ya mada.
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkataba wa aina yeyote...narudia...'yeyote' halali baina ya pande moja halali na moja mufilisi usitambuliwe km mkataba halali....Kwanzia mwanzo Richmond ilionekana ni kampuni hewa (ya kitapeli) hivyo kufanya makabidhiano haramu na kampuni halali (DOWANS) Ilibidi kutotambuliwa kwa kua mchakato uliingia doa tokea mwanzo!...DOWANS itaipeleka CCM kaburini...na iking'oka itang'oka km jino bovu! ambalo liking'olewa halina mahali pengine pakufitisha!...nachangia hoja!
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Kwa mfano wa ndoa ya pili na ndoa ya kwanza na kushabihisha na Dowans,umenunua utata..umezunguka na utapata majibu ya kiaina aina.
  Bila shaka ni kwa nia njema tu umetumia mfano wa ndoa lakini umewapa watu nafasi wafanye spin.
  Kama kuna uwezekano, edit, weka mfano na hoja za kisheria zisizo za ndoa. Ni ushauri tu, mkuu.
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ndoa ya pili si halali.

  Kwa Wakristo na kwa waislam pia. Swali la kujiuliza ni hili: Je, huyo Mungu anayeaminiwa na watu wa deen, aliumba Eve wangapi kwa Adam? Maana kama Mungu anajuwa yote, na Mungu ni mwenye hekma, na Mungu alimpenda Adam, basi kwanini Mungu alimpa Mke mmoja tu kwa ADAM?

  Basi namaliza kwa kusema Mungu aliumba ADAM mmoja, na Eva mmoja kwa ADAM. Ambayo ndio ndoa halali mbele ya Mungu.
   
 7. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Hata km asingetaja DOWANS ...jukwaa alipoanzia hii thread na aya ya kwanza vilitosha tu kumpa alert mtu asiye mvivu wa kufikiri kujua anachomaanisha!...nadhani watu wanaelewa,si wakutafuniwa hivyo!..Shime mkuu MM
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  :focus: can we get back to Husbands (dowans and Richmond) and a Wife (Tanesco) please
   
 9. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Bila kumtaja Dr.Slaa hupati usingizi. Una kazi kweli kweli. Msg. sent na umeelewa kwa ujumla. Tunashukuru kwa hilo. Lingine????
   
 10. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MMKJJ,
  Ndoa ya pili itakuwa batili ( wanasheria watatusaidia kwa hili). Ubatili hauleti haki, hivyo wote - muoaji na muolewaji wa ndoa ya pili watakuwa wamecheza pata potea!
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  a) Ndoa ya pili ni halali kama ile ya kwanza halali imevunjika katika misingi inayoeleweka na vyombo husika vimeridhia..

  b) Kila partners ana haki ya kudisclose previous status kwa mwenzie

  c)Vyote vyaweza kuwa mali ya ndoa ya pili kama ndoa ni halali

  d)Yaweza kuwa kosa lako kutokujua kama hukuchukua hatua yeyote kutaka kujua kuhusu partner wako kabla ya kufanya maamuzi ya ndoa
  Na pia kosa laweza kuwa si lako kama ulidanganywa kuwa hakukuwa na ndoa kabla japokuwa you were suppose to do your homework kujua background ya partner wako...........

  In relation to DOWANS,hii ni drama,walijuana status zao na bado wakafunga ndoa ya pili batili........:disapointed:
   
 12. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Richmond ilikuwa declared "kampuni feki/hewa".
  Kama ni "hewa/feki" then haiwezi kuingia mkataba unaotambuliwa kisheria na "mtu" yeyote yule.
  Iwapo hiyo kampuni "hewa/feki" itaingia ktk mkataba na kampuni nyinine, huo mkataba ni "null and void ab initio", maana hautatambuliwa kisheria popote pale.
   
 13. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  .

  Mkuu hwa mabwana walipitia katiba na sheria zetu,wakatafuta vifungu vyote ambavyo vingewabana na renumerations zake ndio wakaingia mkataba....ukisoma mkataba walioingia utaona ni lazima DOWANS walipwe,lakini kanuni yetu ya mwanzo ni kwa kua maridhiano ya kubadilishana hatamu yalifanyika na kampuni mama Richmond iliyokua haramu basi tusitambue hata huu mkataba "mzuri"...hilo tu
   
 14. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ni muhimu tujue mkataba wa ndoa ya pili hawa wanndoa (Tanesco na Dowans) walikubaliana nini, ila my take ni kuwa ndoa hii ni batili
   
 15. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ignorance in law is not an excuse...
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,352
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, mkataba wa ndoa ndio mkataba pekee katika ya mikataba yote ambao unaweza kuingia kwa hiari, lakini kamwe huwezi kuuvunja kwa hiari, ni mahakama pekee ndio yenye mamlaka ya kuuvunja tena ikiridhishwa na sababu. Pia ndio mkataba pekee ambao hauna haki ya ku huishwa!.

  Mikataba mingine yote, mnaingia kwa hiari, na mnaweka vifungu vitakavyopelekea mkataba huu kuvunjika pamoja na haki ya ku huishwa kwa mkataba husika.

  Kwa hiyo kisheria, ndoa ya serikali na Richmond inahuishwalika kihalali kwa paende mbili kuridhia bwana mpya au bibi mpya. Kwa mujibu wa mkataba ule, ulikuwa kama ndoa ya Ki Hindu kwa Bwana ni Richmond na serikali ya Tanzania ndio iligeuzwa bibi, lakini kikawaida, anayalipa mahari ndio huwa bwana, na anayelipiwa ndio huwa bibi.

  Anayelipa mahari ndio hupanga anataka nini, (Tanesco) na kumtogoza bibi (Richmond), ukimwambia unataka nini, naye hupanga bei, mkikubaliana ndoa kufungwa kama ilivyofungwa.

  Mkataba na masharti ya mkataba ilikuwa ayatayarishe bwana, Tanesco, lakini kutokana na kubabaika na uzuri wa sura, bwana akamwachia bibi ayatengeneze na yeye akabakia, kutia mkono tuu akiamini ni mapenzi ya dhati.

  Baada ya ndoa kufungwa, licha ya Bibi Richmond kushindwa kutoa huduma, na hapa ndipo kwenye moja ya vipengele vywa kumalizika ndoa hiyo kwa amani, kama Bibi Richmond, angekubali kui consumate hii ndoa lakini rigwaride likamshinda, angekuwa na haki ya kuomba talaka na mkawanya mali mliochuma kwenye ndoa yenu.

  Lakini ndoa hii ya Tanesco na Richmond, haikuwahi kuwa consumated, hivyo inageuka ni void ab-initio yaani ndoa imefungwa lakini hakuna ndoa, kinachotakiwa kufanyika ni kwenda mahakamani ili mahakama iibatilishe ndoa ile. Baada ya Richmond kushindwa kutimiza masharti, na bwana alistahili kurudishiwa mahari yake, au wangekubaliana kila mmoja kuubeba msalaba wake.

  Cha ajabu badala ya bwana Tanesco kuomba kuibatilisha ndoa, bibi Richmond akakiri kwa bwana, kuwa ndoa imemshinda, ila atamletea mwanamke mwingine Bingwa kuikamilisha ndoa ile, na mwanamke bingwa ndio Dowans na bwana hata kabla hajaulizwa na kukubali, mzazi wa bwana, Tanesco, ambaye ni serikali, akamlazimisha mwanae, amkubali mwanamke mpya na ndoa ikahuishwa na ikaendelea.

  Ingekuwa ni ndoa ya kweli, hakuna ku huishwa, lakini ndoa ya kimkataba, uhuishwaji huu ni halali, ndio maana ICC ikazingatia kuwa mkataba ule ni halali.

  Mzee Mwanakijiji, na wengine wote mnaoitakia nchini yetu mema, tutajadili na kujadili lakini kwa mkataba ule niliouona humu, tumefungwa mikono na miguu, hatuna pa kutokea, pesa zile ni lazima tulipe, tupende, tusipende, vingevyo viongozi wetu wajivike ujasiri kama wa Nyerere na kusema, " to hell with ICC", hao wawekezaji na waondoke tuu, watuachie madini yetu, tutayachimba hata kwa kucha, na almasi zetu tutachezea bao!.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,352
  Trophy Points: 280
  GAGAGIGIKOKO, kwenye batili, kuna void, na voidable, void ni ule ubatili ambao una rekebishika na ndoa kuendelea, mathalani imeshindikana kuwa consumated kwa vile njia ni nyembamba mno, na haipitiki, njia ikitanuliwa na kupitika, ndoa inakuwa consumated na kuendelea.

  Ndoa ya Tanesco na Richmond, was voidable, baada ya Tanesco kunchukua mke mwingine, Dowans, ile ndoa ilikuja kuwa consumated na kugeuka ndoa halali, hata kama imeibukia kwenye ubatili, ndio maana nasisitiza hakuna pa kutokea, pesa lazima zilipwe!.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,352
  Trophy Points: 280
  Not only that, hata kama ulijua mke ana matatizo, na wewe hukuchukua hatua zozote kushitaki tatizo hilo, inachukuliwa kuwa umemkubali mke huyo na matatizo yake, ukishapitiliza muda fulani, kupitia limitation clause, haiwezekani ukaibuka na kudai mke wangu ana matatizo. Tanesco ilikuwa na chance ya kuivunjilia mbali hii ndoa pale Richmond, aliposhindwa kutimiza wajibu wake, kwa kutofanya kitu ni kukubali matatizo yale, na sio tuu ilikubali bali kumpokea mwanamwali mpya kuendeleza pale mwanamwali wa mwanzo aliposhindiwa na ndoa iliendelea.
   
 19. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Where have i indicated that ignorance is an excuse in law in my statements???
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye red&bold: tupe evidensi
   
Loading...