Ndoa ya mtoto wa Mungai bado kitendawili

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,147
Habari zaidi!
Ndoa ya mtoto wa Mungai bado kitendawili
Frank Leonard, Iringa
Daily News; Tuesday,February 24, 2009 @19:18

kura

Mahakama ya Mkoa wa Iringa imeshindwa kutoa uamuzi kesi ya madai namba moja ya mwaka 2009 inayomkabili mfanyabiashara maarufu wa mjini hapa, Jofrey Mungai baada Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kuitisha jalada la kesi hiyo.

Jofrey Mungai alishitakiwa mahakamani hapo na mkewe Vivian Mtasiwa waliyeishi kwa zaidi ya miaka 11 na kuchuma mali nyingi, baada ya kusikia Kanisa Katoliki Parokia ya Mshindo Iringa Mjini likitangaza ndoa mpya baina ya mumewe huyo na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Iringa, Safina Herihaki.

Ndoa hiyo ilipangwa kufanyika Jumamosi ijayo, Februari 28.Mahakama hiyo iliyokuwa itoe uamuzi wake juzi baada ya Mungai kwa kupitia wakili wake, Basil Mkwata kuweka pingamizi kupinga madai yote ya mkewe huyo ambaye hajamtaliki.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Firmin Matogoro aliyesikiliza pingamizi la kesi hiyo Februari 18 na kuahidi kutoa uamuzi Februari 23, alisema mahakamani hapo kwamba uamuzi dhidi ya pingamizi hilo haupo tena baada ya mmoja wa wahusika katika kesi hiyo (hakumtaja) kupeleka malalamiko ya mwenendo wa kesi hiyo kwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Fakiri Jundu ambaye aliitisha jalada la kesi hiyo.

Pamoja na kumfikisha mahakamani, Mtasiwa aliweka pingamizi kanisani kuzuia ndoa hiyo isifanyike mpaka pale madai yake ya msingi dhidi ya mumewe huyo yatakaposikilizwa na mahakama.

Kanisa Katoliki kwa kupitia Katekista wake, Idfonce Kilamlilo ambaye pia ni Mwandikishaji wa Ndoa kanisani hapo lilithibitisha kupokea na kulikubali pingamizi la Mtasiwa mpaka pale wawili hao watakapomaliza tofauti zao au mahakama itakapotoa maelekezo mengine.

Katika mahakama hiyo, Mtasiwa anaomba amri ya mahakama ya kuzuia ndoa baina ya mumewe na Safina Herihaki mpaka pale madai yake yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Katika hati ya madai anataka kupewa nusu ya mali zote walizochuma pamoja na mumewe huyo, matunzo kwake na watoto wawili waliozaa na kupata mgao wake kutokana na faida inayopatikana kutoka katika kampuni yao ya ujenzi ya GNMS.

Mungai ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya ujenzi ya GNMS na mmiliki wa Hoteli ya kifahari ya White Horse Villa ya Iringa ni mtoto wa Charles Mungai ambaye ni mdogo wake na Waziri Mkongwe wa zamani, Joseph Mungai.
 
Mimi nilidhani kanisa Katoliki halifungushi ndoa kwa former married man, au?
 
Nod maana kanisa likatangaza ili mwenye kipingamizi atoe, ila katekista anakosea kusema kuwa watasubiri uamuzi wa mahakama, sheria za kanisa kuhusu ndoa canon law zinapingana sana na za mahakama, je mahakama ikiridhia kulikuwepo ndoa kati ya jeofrey na mtasiwa kanisa litaridhia?

Wanaomfahamu jeofrey wanasema hata huyu binti wa tumaini amepotea kwa ni jamaa ni wembe hatuliii utadhani ndo anabalehe wakati anakaribia 50s
 
maisha bwana! sasa umeishi na m2 miaka 11 unahangaikia nini tena? sijaelewa mahali walikuwa bado wanaishi pa1 akashtukia tu huyo mwenzi wake katangaza ndoa au walitengana?
 
Jamani mbona dunia imekwisha.Umeishi na mkeo 11 years leo eti umepata kabinti kadogo unamtosa. Mmechuma mali naye Kibao, watoto Mungu kawasiadia Mmezaa tena zaidi ya mmoja, shughili zenu Mungu anazibariki zinaenda vizuri kabisa lakni mwanaume Boooooooooooo.............leo hii eti unamfukuza na kutanga Ndoa nyingine.........Hv ni laana au nini

Tuogope Mungu Wandugu
 
Mh yaani siku hizi ndoa si kitu tena.......... cheatings kibao, uonevu kwa sana ili mradi shaghalabaghala tu.
 
Jamani, ngoja na mimi nirudi. Kwani ndoa maana yake nini? Kwanza mpendane bila kuchokana na kutimiza yale mliyokubaliana kwenye MoU. Wengi hawajui kwamba mnapopendana kuna ka MoU mnakaweka kinamna. Sasa hiyo miaka 11, huyu mama, kama si dada, ameendeleza kutimiza yale yaliyomleta pale. Wengi dada zetu mkishajenga au kuzaa, basi, ashakumu si matusi, utaanza kunyimwa unyumba, mara hakusemeshi, ili mradi vurugu tupu! Ndipo wanaume wanachukua dogodogo na kuchunwa! Iangalieni sana hii.
 
Last edited:
Mkiishi na mwanamke na mwanamume zaidi ya miezi sita inakuwa considered kama ni ndoa where are you peeople? Suala hapo ni mtu wa kuithibitishia mahakama kama kweli waliishi na vithibitisho nadhani vitakuwepo. Siko upande wowote lakini hivyo ndivyo ilivyo. Kama kuna mwanasheria naomba alifanyie ufafanuzi
 
Yaani wanaume ameshidwa kishi na mke wake na afunge naye ndoa walee watoto wao vizuri.
halafu na huyo dada anteolewa na yeye hana akili nyumba aliyotoka mwenzako wewe huiwezi una nini cha mno ambacho mwenzako hana, na kesho atamuona mwingine na huyo atamuacha mimi nashangaa wanawake wenzangu kweli mambo haya yote anayosikia yanatokea anashidwa kujifunza.
halafu anaweza akafunga ndoa na bado akaachwa.

Nakumbuka zamani mama mmoja alikuwa mzazi huko mkoani kwetu mume akaleta mwanamke mwingine ndani yule mama alimkata sehemu za siri akalazwa hospital mwezi 1 toka hapo ameshika adabu na wanaishi vizuri japo jamaa amedhurika
 
Ni kweli jamani wanawake wamezidi! Mimi nahisi huyo Vivian alianza kumletea mumewe za kuleta ndio maana jamaa kaamua kuoa mwingine. Mwanaume ukitaka kuwa na starehe ndani ya nyumba yako usije ukafunga ndoa na huyo mwanamke uliyenae, bora kuishi nae tu kama mchumba maana wachumba huwa wanapenda na kujali mwanaume, lakini akishaolewa anabadilika kabisa utadhani siye yule! Unapokuwa nae kama mchumba anakupa penzi zuri ajabu, na hata unyumba hadi unaona mashallahu mwanamke ndio huyu! Ngoja ufunge hiyo ndoa! Siku za mwanzo atajitahidi kidogo hadi apate mtoto, na kama bado mnatafuta mali pia atavuta muda hadi aone sasa kuna mali za kutosha, cha kudai kipo. Hapo utaanza kunyimwa unyumba, kununiwa, kuagiziwa kuwa chakula kiko jikoni anayetaka ale asiyetaka aache! Sasa katika hali kama hii kwanini mwanaume asitafute mchumba mwingine? Ya nini kuteseka wakati uwezekano wa kufurahi upo?
 
Hili liwe fundisho kwa mabinti , wasipende kukaa/kuzaa na wanaume kabla hawajafunga nao nadhiri za milele
 
Suala ni huyu dada/mama kupata haki yake, tukianza kutafuta sababu ya kuachana hatutamaliza kwani masuala ya ndoa ni yawana ndoa wenyewe.Bin Mungai patia huyo mama haki yake akalee watoto wake, kwani pia naye amechangia kwa namna moja ama nyingine ktk mafanikio yako. kumbuka wafanyakazi hupata retrenchment benefits pindi waachishwapo kazi sembuse mama watoto wako ambaye ninaimani siku za mbeleni waweza kurudiana.
 
Kufunga ndoa ya milele hakumkatazi mwanaume kuoa mke mwingine. Suala ni kulinda na kuheshimu mchango wa mwenzi wako ktk mafanikio ya familia.
 
Ndoa ndoana....mshikemshike....mikikimikiki.

Kwa wale ambao hawamo humo....jiahadharini na kitu ndoa...kwa wale waliomo humo, vumiilieni mikiki hiyo....
Laiti kumngelikuwa na njia nyingine decent ya kupata wwt.....ndoa ingekuwa ndoto kwangu.....naungana na Mtu B kuishi bila formalities za ndoa kunasaidia..............
"Ole wao waoao, maana nao wataolewa"
 
Mlioko karibu Jofrey Mungai tupasheni zaidi,,,, habari niliyoipata toka Iringa inasemekana Harusi ya huyu ndugu haitafungwa kesho kama ilivyotarajiwa. Hi ni kutokana na pingamizi aliloliweka bi Vivian. Baada ya kukubaliana kumpatia Vivian numba, gari na shilingi milioni kumi, Bwana harusi mtarajiwa hakukamilisha ahadi hiyo hivyo Vivian kuweka pingamizi hadi atakapopewa kama alivyoahidiwa. Nasikia katika hela kapewa milioni moja tu na wala si 10 kama walivyokubaliana.
Wenye data zaidi waziweke hapa
 
Niko iringa nimezungumza na geofrey muda mfupi uliopita, ametoka arusha kwenye send off na huyu binti wa kichagga wa hapa tumaini university, ni wazi kanisa katoliki halitakubali kutumbukia kwenye kashfa hii kwa kufunga ndoa yenye utata, geofrey aliishampatia mama watoto nyumba moja na gari aina ya cresta

kuhusu hisa za kampuni ni wazi kuwa kampuni za ukandarasi huwa haziwi na cash bank labda hayo magari

lakini ni wazi kuwa penzi kati yake na mama watoto limeloloma ni vema tu wakafikia muafaka
 
Back
Top Bottom