Ndoa ya mke mmoja au wengi? Vipi kuhusu talaka? Soma hapa ujue msimamo wa Biblia

Nilichokipata hapa ni kuwa kumbe inaruhusiwa kutoa talaka kwa mke aliyefanya kosa la kuchepuka tu (Matayo 5:31-32)

Japo Biblia nayo inazingua kwa kusema walioachana waweza kurudiana na wasiachane tena 1 Wakorinto 7:11 (Sasa kulikuwa na haja gani ya kuruhusu Talaka?)

Vitabu vya dini viliandikwa siku nyingi na viliendana na mazingira ya sikuhizo. Kwa sasa idadi ya wanawake ni mara 4 zaidi ya wanaume. Hivyo kwa mazingira ya sasa ni busara sana wanaume waoe wake wengi ili kuwe na uwiano wa haki sawa kwa wote.

Pia kwa kuwa Mungu amekataza kuchumbia mke aliyeachika (Walawi 21:7) basi suluhisho ni kwamba - Mke pasua kichwa asiachwe kwa Talaka kwakuwa hataolewa tena bali mume aruhusiwe kuongeza mke wa pili bila kumuacha mke wa kwanza.

Hivyo ndoa za wake wengi ndio suluhisho sahihi la kukataza kutoa Talaka. Itasaidia wanawake kuanza kuwa na adabu kwa waume zao.
kuna dini ishaoba mbali sana na ikaruhusu wake wa4

karibuni bhna
 
Umeelewa vyema sana. Fungu la kumi linatolewa popote pale ambapo roho yako itakuwa na amani napo maana Bwana ndio atakuwa amepachagua. Makanisa yamekuwa yakilazimisha waumini wapeleke fungu la kumi makanisani na hiyo ndio imefanya ionekane kuwa sadaka hii wanaoitaka ni wachungaji na sio Mungu mwenyewe (yaani wanafaidika nayo). Makanisani kwenyewe wamekuwa wakiing'ang'ania kuwa ni yao (wachungaji) maana imenenwa kuwa Walawi hawana kazi nyingine hivyo fungu la kumi ni lao. Kujenga hoja yao ya kuleta fungu la kumi hutumia mstari huu wa Malaki 3:10-11

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
Mal 3:10‭-‬11 SUV


Kimsingi, neno kuu ni kuwa usiache kutoa fungu la kumi kwa Mungu, mahali pa kutoa ni popote pale Bwana atakapopachagua (yaani pale ambapo utatoa huku moyo wako una amani), inaweza kuwa ni hospitali, kwa wajane, kwa yatima au nyumbani kwako mwenyewe au kanisani nk sio lazima upeleke kanisani
Na hii ya hawa wachungaji kujipa vyeo ya ulawi wakati Mungu alikuwa anaelekeza specifically kwa kabila la LAWI na sio kabila la MKURYA au Msambaa ndo nawashangaa kabisa. Na hao WALAWI pia hawakuwa na kazi ya kipato ndo maana walipelekewa wao hilo fungu la 10 na ndo maana ilikuwa lazima iwe matunda ya ardhi. Na sio pesa. Sijajua ni kifungu gani kilihamisha kabila la LAWI kuwa ni wachungaji wa Sasa?? Sasa hawa wachungaji wa Sasa wenye MISHAHARA bado wanataka fungu la 10
 
Hakuna mahali Biblia inapokataza mkristo wa kawaida kuoa mke zaidi ya mmoja. Angalizo limewekwa kwa Askofu na Shemasi hawa ndio wameshauriwa kuwa na mke mmoja, wengine wasio na vyeo hivyo ni ruksa kuwa na mke zaidi ya mmoja. 1 Timotheo 3:1-7 na 1 Timotheo 4:1-5

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja , mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
1 Tim 3:1‭-‬3 SUV

Mkuu unajua sana, hapa huu mstari nitaenda kuwatesa sana watu mahali...
 
Na hii ya hawa wachungaji kujipa vyeo ya ulawi wakati Mungu alikuwa anaelekeza specifically kwa kabila la LAWI na sio kabila la MKURYA au Msambaa ndo nawashangaa kabisa. Na hao WALAWI pia hawakuwa na kazi ya kipato ndo maana walipelekewa wao hilo fungu la 10 na ndo maana ilikuwa lazima iwe matunda ya ardhi. Na sio pesa. Sijajua ni kifungu gani kilihamisha kabila la LAWI kuwa ni wachungaji wa Sasa?? Sasa hawa wachungaji wa Sasa wenye MISHAHARA bado wanataka fungu la 10
Ni kweli Walawi walikuwa ndo kabila la kikuhani lakini hilo lilikuwa ni Agano la Mungu na WAISRAEL.

Ujio wa Yesu na kufa kwake kumekamilisha Agano jipya kati ya Mungu na watu wa mataifa yote(Gentiles).Hili ndilo agano jipya lililoahidiwa na Mungu kupitia Jeremiah,Isaya na manabii wengine.

Katika Agano hili Yesu ametupatia wote mamlaka ya kikuhani tafauti na awali ambapo ni watu wa kabila fulani tu(Walawi) ndo walikuwa na power za kikuhani.

Kwa maana hiyo basi sasa kila mtu anauwezo wa kusogea mbele za Mungu kumtolea sadaka na kupeleka maombi yake.Hatuhitaji tena mtu wa kati kupeleka maombi na kutoa sadaka kwa niaba yetu.

(Go and study Old Covenant and New Covenant)
 
Hali ya uchumi kwa mwanaume inapoyumba na uzinzi kwa mwanamke imekuwa ndiyo chanzo kikuu cha kuvinjika kwa ndoa. Wanandoa wa siku hizi hawana uvumilivu licha ya ndoa kufungwa kwa gharama na ufahari wa anasa. Single mother wanaongezeka kwa kasi ya ajabu wala viongozi wa dini hawana ubavu wa kukemea kuachana kwa wanandoa
Kwa nini wasisepe wakati lengo kuu la wao kuingia kwenye ndoa ni kuhudumiwa. Ukifulia wee hesabu maumivu tuu ya kubwagwa🤣🤣🤣🤣🤣
 
Amina SoMo nzuri sana, Tuache tabia Mbaya ya kuoa oa hovyo,
Ila changamoto ni kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume, Sasa Hawa wanawake wengine watashugulikiwa na nani?
Siyo kazi yetu! Hiyo tumwachie Mungu mwenyewe anajua jinsi ya kufanya.Pia kama angeona hivyo kwamba wanawake ni wengi angetooa amri tungeoa kadiri ya uwezo wetu.
 
NDOA YA MKE MMOJA AU WENGI? VIPI KUHUSU TALAKA? SOMA HAPA UJUE MSIMAMO ULIOPO KWA MUJIBU WA BIBLIA.

"Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote". Hiyo ni ahadi namba 6 ya mwanachama wa CCM. Mimi kama ilivyo wakati wote nitaendelea kutimiza hiyo ahadi. Hii post itajikita kwenye suala zima la ndoa. Je, sisi wakristo tunaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja? Talaka je? Biblia inasemaje? Soma kwa makini aya zinazofuata upate majibu.

Kabla ya kujibu hilo swali lazima tujue kwanza ndoa ni nini ikiwemo historia yake nzima.

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

Kibiblia ndoa ni mpango mtakatifu wa Mungu ulioanzia Edeni. Mwanzo 2:18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Kama ilivyo kwa sheria ya jamhuri ya TZ basi hata kibiblia tafsiri haijapishana;
Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja".

Kwa kifupi ndoa ni taasisi takatifu iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe. Mwanaume na mwanamke wataungana bila kujali kabila, dhehebu wala taifa. Cha muhimu muwe mmejitoa nafsi zenu kwa dhati kabisa kuitumikia taasisi ya ndoa. Ni ruksa mke kuolewa na asiyeamini au mume kuoa asiyeamini (1 Wakorintho 7:12-16). Kwa msisitizo imeandikwa kwenye 1 Wakorintho 7:16 "Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?".. ukipata asiyeamini na mnaelewana biblia imesema msiachane kwasababu anayeamini atamwokoa mwenzake.

Tukisoma biblia zaidi tutaona watu pekee waliowahi kuwekewa masharti zaidi wakati wa kuoa walikuwa ni Walawi. Hawa waliongezewa masharti kwasababu walitengwa kwa kazi maalum ya ukuhani. Waliambiwa hivi;

Mambo ya Walawi 21:7 "Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake".

Mungu hufurahishwa pale watu wanapofunga ndoa badala ya kufanya uzinzi. Lengo kuu la Mungu kwa wanandoa ni kuijaza dunia kupitia vizazi vyao. Tunaona Adam na Hawa waliambiwa zaeni mkaongezeke muijazw dunia na hata baada ya gharika aliendelea kusisitiza watu wazaliane. Ingawa Mungu mwenyewe hufurahi mtoto anapozaliwa bila kujali ni wa ndani ya ndoa au nje ila kasisitiza kabla ya lolote ni vema kufunga ndoa. Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake".

Je, ni sahihi kuoa mke zaidi ya mmoja? Hili swali lina mtego mkubwa kwa sababu hata kwenye biblia tumeona kina Suleman na Yakobo wakioa mke zaidi ya mmoja hivyo kuleta maswali mengi zaidi miongoni mwa wakristo wa leo. Kwa sisi wakristo tukisoma vizuri biblia huku tukizishirikisha akili zetu vizuri tutaona wazi mpango wa Mungu ni ndoa ya mume na mke mmoja na sio mume na wake wengi. Mwanzo 2:18 mkisoma mtaona imeandikwa "nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" na sio wasaidizi. Hata mwanzo 2:24 imeandikwa "mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja". Kwahiyo hadi hapo tumeona point ilikuwa ni "mume na mke" na sio "mume na wake".

Marko 10:2-12 tumeona pia Yesu akiwasisitiza mafarisayo kwamba ndoa ni ya mke na mume tu. Mtume Paulo nae alieleza umuhimu wa kuwa na mke mmoja akitaja uzinzi kama sababu kuu. 1 Wakorintho 7:2 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe". Hata sisi tunaona kwamba mume mmoja na mke mmoja ni bora zaidi hasa nyakati hizi ili kuepuka maradhi. Hivyo wakristo tuelewe kwamba mpango mzima ni mume na mke mmoja tu.

Je, vipi kuhusu talaka? Kwa kifupi talaka haikuwa mpango wa Mungu kabisa. Na wanandoa wanapoachana ni huzuni kubwa hadi kwa muumba mwenyewe. Mpango wa Mungu ni wanandoa watenganishwe na kifo tu na sio sababu nyingine. Yesu anasema alichokiunganisha Mungu basi binadamu asitenganishe (Marko 10:9)

Kama ilivyokuwa kwa mafarisayo enzi za Yesu bado kuna wengi tunajiuliza mbona kwenye agano la kale tunaona Musa aliwaruhusu waisrael kutoa talaka? Soma Kumbukumbu la torati 24:1-4 uone maelekezo waliyopewa. Yesu alijibu swali hili vizuri sana kwa kutuambia "Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. " (Mathayo 19:8 na Marko 10:5).. ni kwamba waisrael waliruhusiwa mambo ya talaka kwasababu walikuwa walalamishi mno. Hawakuwa wakiridhika hata wafanyiwe kitu gani. Kule jangwani ilibidi Mungu kupitia Musa atunge sheria ndogondogo nyingi sana ili aweze kwenda nao sawa. Baadhi ya sheria ndo hizi ambazo SDA wanalazimisha tuzifuate hadi leo hii.

Pia tujue kwamba sababu pekee inayokubalika mbele za Mungu kwamba inaweza kusababisha talaka ni uzinzi (kuchepuka). Mathayo 5:31-32 "Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini". Lakini ili kuonyesha jinsi gani talaka isivyo jambo la kumpendeza Mungu, biblia imeshauri kupitia 1 Wakorintho 7:11 kwamba watu wakiachana yule mwanamke asikimbilie kuolewa bali atafute suluhu na arudiane na mumewe na pia huyo mume asimuache mkewe tena.

Kiukweli ingawa sababu inayotambulika ni hii ya kuchepuka ila hata Mungu mwenyewe anajua mabalaa ya wanawake. Anaweza asiwe anachepuka ila hizo kero ukajikuta uko jehanam hapahapa duniani. Biblia imetamka wazi.. Mithali 21:9 "Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi". Na Mithali 21:19 "Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi".

Pamoja na yote hayo bado mwenyezi Mungu ni mtetezi mkuu wa wanawake. Mwanzo 21 tunaona jinsi gani Sara alimkera mumewe Ibrahim ambapo kibinadamu ingeleta shida ila Mungu akamwambia Ibrahim aliyekuwa kakasirika aendelee kumsikiliza mkewe. Kuna visa vingi vya wanawake kupata utetezi lakini kubwa ni pale biblia inapotuambia mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo tunapaswa kuishi nao kwa akili (1 Petro 3:7). Kimsingi wanawake wanatakiwa kuwatii waume zao na waume wanatakiwa kuwapenda wake zao.
Nadhani ni tafasiri mbaya. Na hiyo bible nadhani walipindisha. Nadhani pasiwe na limit ya mke mmoja kwa sababu hata kwenye zizi la Ng’ombe dume moja majike kibao. Hata Mungu angetaka iwe mke mmoja ina maana angehakikisha basi kila mtoto wa kike anazaliwa mtoto wa kiume mmoja ila kwa sasa wanawake kibao lazima wanaume wawaoe ili kila mtu awe na haki ya kufurahia tendo la ndoa
 
Unachanganya kidogo kwenye tafsiri. Hakunaga ndoa ya wake wengi inayofungwa mara moja, bali kuna ndoa kati ya mwanamke na mwanaume ambaye ana mke au wake wengine tayari, kwa maana ya kwamba kila mwanamke atapozungumza atasema "mume wangu" na sio "mume wetu".

Ndoa ni makubaliano ya mtu mume na mke, hata waislamu na wakabila ndoa hufungwa kati ya watu wawili tu, hakuna mahali (hata kwenye sheria) watazungumzia wake badala ya mke, maana kila mmoja (kama wapo zaidi ya mmoja) ana ndoa yake, hakuna ndoa ya pamoja.

Kwa mantiki hiyo, huwezi kuona katika biblia panaposemwa atapewa wasaidizi (sababu hawaoi kwa mara moja), inaandikwa msaidizi sababu anayeolewa ni mmoja tu. Hata mtu mume akioa mara nane, wale wanawake wanakua na ndoa moja tu, kati ya huyo mwanamke na huyo mwanaume.
Mkuu nadhani kwa mafundisho yako haya,1 Timo4:1-5 inakuhusu wewe! Yesu alishatoa ufafanuzi hapa,Mathayo 19:4-7 MME MMOJA NA MKE MMOJA TU.Na tena hakuna kitu TALAKA kinaruhusiwa,(Mathay5:31-32).
 
Mkuu nadhani kwa mafundisho yako haya,1 Timo4:1-5 inakuhusu wewe! Yesu alishatoa ufafanuzi hapa,Mathayo 19:4-7 MME MMOJA NA MKE MMOJA TU.Na tena hakuna kitu TALAKA kinaruhusiwa,(Mathay5:31-32).
1 Tim 4:3 inakuhusu wewe na vuongozi wengine wa dini. Mnazuia watu wasioe bila kutoa sababu ya kwa nini mnazuia, Soma 1 Sam 25:42-43 unaona Daudi ameoa tayari na akaoa tena, ndio ile nayokuambia, neno litatamka mtu na mkewe kwa kuwa mtu haoi wanawake wawili kwa mara moja. Ila akishaoa zaidi ya mara moja wale wanakuwa wake wa huyo mtu, lakini kila mwanamke anakua na cheti chake cha ndoa.
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom