Ndoa ya mke mmoja au wengi? Vipi kuhusu talaka? Soma hapa ujue msimamo wa Biblia

Hakuna mahali Biblia inapokataza mkristo wa kawaida kuoa mke zaidi ya mmoja. Angalizo limewekwa kwa Askofu na Shemasi hawa ndio wameshauriwa kuwa na mke mmoja, wengine wasio na vyeo hivyo ni ruksa kuwa na mke zaidi ya mmoja. 1 Timotheo 3:1-7 na 1 Timotheo 4:1-5

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja , mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana,
Mkuu kwa jinsi ulivyojibu kwa facts huku ukitupia vifungu vya biblia nimeona nisiseme lolote kwa hizi comments zako zaidi ya kukupa heshima. Nimeona nikubaliane kutokukubaliana. Wewe una hoja nzito kwahiyo kwa upande wangu nimeona nisubiri comments nyingine kama hizi zako ili nami nizidi kujifunza na kuchimba zaidi.
 
Mwanzo 4:23

Lameki akawaambia WAKE ZAKE, “Ada na Sila sikieni sauti yangu! Sikilizeni nisemayo enyi WAKE za Lameki.

Mwanzo 32:22

Usiku huohuo Yakobo akaamka, akawachukua WAKE ZAKE WAWILI, wajakazi wake wawili na watoto wake kumi na mmoja, akapita kivuko cha Yaboki...
 
Comment za hivi napenda sana. Zinachangamsha akili. Najipanga kukutafutia majibu
 
Mwanzo 4:23

Lameki akawaambia WAKE ZAKE, “Ada na Sila sikieni sauti yangu! Sikilizeni nisemayo enyi WAKE za Lameki.

Mwanzo 32:22

Usiku huohuo Yakobo akaamka, akawachukua WAKE ZAKE WAWILI, wajakazi wake wawili na watoto wake kumi na mmoja, akapita kivuko cha Yaboki...
Ongeza na Kumbukumbu la Torati 14:22-28 unaona kabisa Mungu hajazuia watu kunywa vileo pamoja na wachungaji. Neno lasema hivi:

"Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako; ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
Kum 14:22‭-‬27 SUV
 
Mambo ya imani ni magumu. Ila kusema ukweli ktk ukristo hili jambo la kuoa mke mmoja linachaganya
 
Hivi km huyu muumba anataka tuwe na mke mmoja tu. Kwa nini aliumba idadi kubwa ya wanawake wao wataolewa na nani??
Nafikiri hapa tunachaganya maagizo ya Mungu na sheria au utaratibu wa dini
 
Kipi bora
Kuwa na mke wa ndoa na bibi wa kando mliozaa na mchepuko aliyenasa?! Au kuwa na wake watatu wanaotambulika kimila/kisheria?!
Nashauri
Bora uwe mchawi ili upate muda mzuri wa kufanya shirki kuliko mara upo ibadani ila unawaza umloge sheikh/mchungaji usiku

Bora uwe mnywaji na mla mdudu kuliko kuwa kwenye nyumba ya ibada huku ukijua hakuna unachofanya/unachokipata pamoja na kuattend
Unamaanisha maandishi yaliyoletwa kwetu na mleta mada yamekosewa?
 
Hali ya uchumi kwa mwanaume inapoyumba na uzinzi kwa mwanamke imekuwa ndiyo chanzo kikuu cha kuvinjika kwa ndoa. Wanandoa wa siku hizi hawana uvumilivu licha ya ndoa kufungwa kwa gharama na ufahari wa anasa. Single mother wanaongezeka kwa kasi ya ajabu wala viongozi wa dini hawana ubavu wa kukemea kuachana kwa wanandoa
Na wataongezeka zaidi baada ya watoto wa shule kuruhusiwa kufanya yao na kuendelea na masomo
 
Wakristo bana, sijui walokole kwani kwenye biblia unayotumia kuna sheria mahususi kwa waisraeli na mahususi kwa binadamu wote? Unazitofautishaje? Mfano kutokula kitimoto ni ya israeli au ya wakristo wote?
Huwezi kung'amua hili kwa fikra zako.
 
Hakuna mahali Biblia inapokataza mkristo wa kawaida kuoa mke zaidi ya mmoja. Angalizo limewekwa kwa Askofu na Shemasi hawa ndio wameshauriwa kuwa na mke mmoja, wengine wasio na vyeo hivyo ni ruksa kuwa na mke zaidi ya mmoja. 1 Timotheo 3:1-7 na 1 Timotheo 4:1-5

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja , mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
1 Tim 3:1‭-‬3 SUV

Vivyo hivyo Biblia haijakataza unywaji wa vileo na divai. Askofu hatakiwi kuwa mlevi bali awe mnywaji wa kiasi, vivyo hivyo na shemasi. Katazo hili haliwagusi wakristo wa kawaida ila nao kistaarabu wanatakiwa kunywa kiasi ili waweze kujikontroo.

Ukisoma 1 Timotheo 4:1-5 unaona Paulo anatahadharisha kuwa kutakuwa na wapotoshaji wanaozuia watu kuoa na kula baadhi ya vyakula. Neno ni hili;

Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
1 Tim 4:1‭-‬4 SUV
Upo vizuri sana mkuu, nahitaji zaidi madini ya namna hii..
 
Huwezi kung'amua hili kwa fikra zako.

Kwa nini asiweze? Tafuta Ukweli hadi upatikane. Siyo ukishindwa ulete vitisho vya jehanamu na kufuru!

Biblia inaeleweka ndiyo maana tumeandikiwa Watu...

Kuna wachache huwatisha Watu wasihoji biblia... kuhoji tumeruhusiwa ili tuijue Kweli!

Tutahoji kila kitu na kila mtu.

1 Thessalonians 5:21

but test ( prove, question) everything...
 
Wakristo bana, sijui walokole kwani kwenye biblia unayotumia kuna sheria mahususi kwa waisraeli na mahususi kwa binadamu wote? Unazitofautishaje? Mfano kutokula kitimoto ni ya israeli au ya wakristo wote?
INjili ni habari njema kwa wtu wote
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Ongeza na Kumbukumbu la Torati 14:22-28 unaona kabisa Mungu hajazuia watu kunywa vileo pamoja na wachungaji. Neno lasema hivi:

"Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako; ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
Kum 14:22‭-‬27 SUV
Kupitia hili neno nimepata vitu vizuri kuhusu fungu la 10.
1. Ilikuwa lazima litokane na shamba aka mazao etc
2. Lazima liwe la. Mwaka to mwaka sababu ni la shamba na sio mwezi to mwezi kama makanisa ya Sasa yanavyotufundisha.
3. Ilikuwa sio fedha ilikuwa ni mazao sababu tangu mwanzo Alisema ni shamba.
4. Ilibadilishwa kuwa fedha pale tu unayempelekea ambaye ni Mjane au Malawi yuko mbali na huwezi kuvibeba
5. Ilikuwa ni kwa ajili yako Malawi na wajane na wasiojiweza. Hii ya kulaizmishana kupeleka Church ilianza wapi???
So kuna fungu la 10.la Mungu aliloagiza na fungu la 10.la makanisa ya Sasa ambalo sijui lilitoka wapi.
 
Umeelewa vyema sana. Fungu la kumi linatolewa popote pale ambapo roho yako itakuwa na amani napo maana Bwana ndio atakuwa amepachagua. Makanisa yamekuwa yakilazimisha waumini wapeleke fungu la kumi makanisani na hiyo ndio imefanya ionekane kuwa sadaka hii wanaoitaka ni wachungaji na sio Mungu mwenyewe (yaani wanafaidika nayo). Makanisani kwenyewe wamekuwa wakiing'ang'ania kuwa ni yao (wachungaji) maana imenenwa kuwa Walawi hawana kazi nyingine hivyo fungu la kumi ni lao. Kujenga hoja yao ya kuleta fungu la kumi hutumia mstari huu wa Malaki 3:10-11

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
Mal 3:10‭-‬11 SUV

Kimsingi, neno kuu ni kuwa usiache kutoa fungu la kumi kwa Mungu, mahali pa kutoa ni popote pale Bwana atakapopachagua (yaani pale ambapo utatoa huku moyo wako una amani), inaweza kuwa ni hospitali, kwa wajane, kwa yatima au nyumbani kwako mwenyewe au kanisani nk sio lazima upeleke kanisani
 
Acheni kupotosha kwa hiyo huko hospital ni nyumbani kwa Bwana?
 
Umeelezea vizuri Sana nada yako Ila umekosea sehemu Moja tu. Kusema KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO (SDA) linatulazimisha kushika Sheria za Musa.. umekosea.

1:Wapi limekulazimisha nipe Mwongozo wowote wa Kanisa la SDA unaomlazimisha Kila mtu Ashike Sheria za Musa?

2:Kila Dhehebu au Dini Lina/Ina taratibu zake za kuendesha mambo Yao kwa misingi ya Imani Yao kwa Mungu. Hivyo kama Kuna kitu hukijui Uliza watu wa Dini hiyo au Dhehebu Hilo wakupatie ufafanuzi..siyo kukurupuka tu na kutoa tuhuma usizokuwa na ushahidi nazo.

3:Watu flan wa Dini flan au Dhehebu flan wao wakikubaliana na kuwekeana taratibu za kuendesha Dhehebu lao Bila kuvunja Taratibu za nchi husika.. unapaswa kuwaheshimu maana wao wamekubali kwa Akili zao timamu na hawajakulazimisha na wewe uwafuate.. hata Selikali ya Mungu kule Mbinguni Kwa wanaoiamini Biblia ilikuwa na taratibu za kuishi kule Lusifa zilipomshinda Ikabidi atimuliwe.. heshimu Taratibu za SDA walizojiwekea wao zinawafaa.. na kinachowafaa wao siyo lazima na wewe Kikufae.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nilichokipata hapa ni kuwa kumbe inaruhusiwa kutoa talaka kwa mke aliyefanya kosa la kuchepuka tu (Matayo 5:31-32)

Japo Biblia nayo inazingua kwa kusema walioachana waweza kurudiana na wasiachane tena 1 Wakorinto 7:11 (Sasa kulikuwa na haja gani ya kuruhusu Talaka kwa mke mzinifu tu?)

Vitabu vya dini viliandikwa siku nyingi na viliendana na mazingira ya sikuhizo. Kwa sasa idadi ya wanawake ni mara 4 zaidi ya wanaume. Hivyo kwa mazingira ya sasa ni busara sana wanaume waoe wake wengi ili kuwe na uwiano wa haki sawa kwa wote.

Pia kwa kuwa Mungu amekataza kuchumbia mke aliyeachika (Walawi 21:7) basi suluhisho ni kwamba - Mke pasua kichwa asiachwe kwa Talaka kwakuwa hataolewa tena bali mume aruhusiwe kuongeza mke wa pili bila kumuacha mke wa kwanza.

Hivyo ndoa za wake wengi ndio suluhisho sahihi la kukataza kutoa Talaka. Itasaidia wanawake kuanza kuwa na adabu kwa waume zao.
 
Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom