Ndoa ya Mkataba Ndo Mpango Mzima

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Wakuu,

Wasaalam,

Nashauri tuwe na ndoa za mkataba tu sasa. Tuachane na haya mambo ya kale ya kutenganishwa na kifo.

Huu mfumo wa sasa ni wa kizamani sana na kiukweli saivi mambo yamebadilika sana. Mazingira ya wakati huo na sasa yana utofauti mkubwa.

Changamoto za ndoa za sasa ni tofauti kabisa na zama hizo. Ndomaana watu saivi watu wanaoana baada ya siku/miezi/miaka michache unasikia wameachana, hlf inakuwa ndo stori ya tauni. Ni kama vile watu tumekaririshwa lazima ndoa idumu.

Ndoa nyingi saivi (hata zile unazodhani ni imara) zipo ICU. Yaani kuna moto/fukuto la chini kwa chini lakini cha ajabu watu wanakomaa na tai shingoni. Kamwe hakuna anayethubutu kumwambia mwenzake ebwanae...inatosha, mimi sasa basi. Hakuna aliyetayari kusema ndoa imenishinda!! Japo ukweli ndio huo.

Najiuliza sana ktk hali hii kwanini basi ndoa zisiwe za mkataba tu. Mnakubaliana muda wa uhai wa ndoa, mambo ya mali mtazochuma na watoto itakuwaje. Mtakuwa mnahuisha huo mkataba unapokaribia kuisha na hapo kama mmoja hataki ndo inakuwa mwisho wa habari.

Hii itasaidia kupunguza fukuto ndani ya familia na itaongeza uwajibikaji ndani ya ndoa coz mtu anajua hapa nikimbwanda tu jamaa analeta chombo kipya majira ya joto.

Cha mwisho hizi ndoa za mkataba zitasaidia kuwarejesha 'relini' masingle mother wengi sana kama unaangalia kwa jicho la tatu.

Karibuni.
 
Kabla ya kuleta bandiko lako umeangalia mkataba utaathiri vipi vizazi vyenu?
 
Nishaeleza mkuu....ni hivi mkataba (huohuo wa ndoa) ndo utasema maslahi ya watoto yanalindwaje. Najua sio kitu rahisi sana lakin naamini kinawezekana.
Kabla ya kuleta bandiko lako umeangalia mkataba utaathiri vipi vizazi vyenu?
 
Tuanze na kurahisisha talaka kwanza.
Isiwe na mlolongo wa kikuda Kama Sasa hivi.
Watu wamefukia hatua ya kutovumiliana Tena wanaambiwa nendeni mkasuluhishane!!
Wanataka mkauane ndio wajue haiwezekani?
Au Ile imeandikwa Hadi kwenye vitabu wanavyosoma kuwa uzinzi unatakiwa kuwa sababu ya kuvunja ndoa.
Watu wanafumaniana lakini ukiwaendea wanaolisoma neno watakuambia
"Alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganisha"
Kwani Mungu alikuwepo wakati wa kufunga ndoa!?
Sia alikuwa Padre/mchungaji?
 
Wanaume ndo wanaoongoza kulalamika mambo ya ndoa, halafu hao masingle mother kwa nini wanaoumia zaidi ni Wanaume klk Wanawake wenyewe wahusika? Kwa maana kila kukicha Wanaume wanafungua post baada ya post kuhusu Wanawake huku wakilia lia, kwa nini wanawake hawalalamiki iweje huo usingo mother uwaume zaidi wanaume?

Wakati mwingine unaweza kufikiri TZ Wanawake ni strong zaidi na Wanaume ni dhaifu sana vinginevyo nashindwa kuelewa hivi vilio vya wanaume kila kukicha.
 
Back
Top Bottom