Ndoa ya miaka 24 yavunjika baada ya mume kutambua watoto watatu sio damu yake

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
672
1,000
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter, Julius Mmasi kutoka Kenya ameweka wazi jinsi rafiki yake alivyovunja ndoa yake iliyodumu kwa muda miaka 24 baada tu ya bwana huyo kuamua kwenda kufanya vipimo vya DNA vya watoto wake wanne na matokeo kuonyesha watoto watatu wa mwanzo si wake.

Vipimo hivyo vilibainisha kuwa mtoto mmoja wa kiume ambaye ni wa mwisho peke yake ndiye mtoto halali wa mwanaume huyo na mabinti watatu wakiwa si watoto wake wa damu. Baadaye mke wake alithibitisha hilo akidai mabinti hao ni watoto wa bosi wake.""

Endeleeni kupenda mateso hayaa.

Ila chakuelewa hapo iliyosababisha yotee hapo ni PESA.

Bosi anatoa mawe anapewa papuchi.

TAFUTA HELA KIJANA.

#YNWA

--------------------------------------------------

Ndoa ya miaka 24 yavunjika baada ya mume kutambua watoto 3 si wake.

Japo visa hivi hutokea kwenye filamu pekee, jamaa mmoja ambaye alikumbana na hali hii alithibitisha kuwa mambo haya ni ya kweli.

Kupitia kitandazi cha Twitter, Khasakhala almaarufu Julius Mmasi aliwaacha wanamtandao vinywa wazi baada ya kufichua kuwa rafiki wake wa karibu alilazimika kuvunja ndoa yake ya miaka 24 na mke wake baada ya matokeo ya DNA kubainisha kuwa ni baba halisi wa mtoto mmoja pekee kati ya wanne ambao aliwalea pamoja na mke wake.

Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kuwa mke wake alikiri kuwa bosi wake ndiye baba ya watoto watatu wa kwanza

Mwanamume huyo aliamua kufanyia watoto wake wanne uchunguzi wa DNA baada ya kuanza kumshuku mke wake.

Kwa uchungu mkubwa, aligundua kuwa mabinti wake watatu ni watoto wa bosi wa mke wake huku kitinda mimba ambaye ni wa kiume ndiye mtoto wake pekee halisi katika ndoa hiyo.

"Watoto watatu wa kwanza wa kike, wawili walishamaliza tayari kidato cha nne mwingine yuko kidato cha nne. Mke wake alikiri kuwa watoto watatu wa kwanza ni wa bosi wake.

Utamshauri nini mtu kama huyu ?"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom