Ndoa ya kimila ni ndoa nzuri sana kwa wanaume wa kikristo matajiri zama hizi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,516
Habari wadau.

Wanaume wengi wa kikristo wanalalamika tabia za wake zao huwa wanabadilika baada tu ya kufunga ndoa kanisani ama uzeeni kwa kiburi cha ndoa haivunjiki na pia migogoro ya mali ni mingi sana.

Sheria ya ndoa ya Tanzania inatambua ndoa 3.

Ambazo ni ndoa za kidini, ambazo ni ndoa ya kikristo na kiislam

2. Ndoa ya kiserikali

3. Ndoa ya kimila

Mahakama huwa zinaendesha mashauri ya ndoa ama mirathi kwa kutazama cheti cha ndoa kilifungwa kwa ndoa ya aina gani?

Kama ndoa ya kimila mirathi itaendeshwa kimila, kama ni ndoa ya kikristo mirathi ama talaka itaendeshwa kiserikali ama kikristo, kama ni ndoa ya kiislam mirathi ama talaka itaendeshwa kwa kufata taratib za kiislam

Mfano mzee mengi angekuwa amefunga ndoa na k lyn ya kimila. Kesi ingeenda kwa kufata taratibu za kimila ya kimachame.

Bilionea msuya nae hivyo hivyo angefunga ndoa ya kimila. Ukoo wa msuya ungekuwa na nguvu kwenye mirathi. Lakini ndoa ya kikristo imewapunguza nguvu na mali za mtoto wao zinasimamiwa na upande wa kikeni maana mke yupo jela.

Ushauri kwa Wanaume wa kikristo wenye pesa msiogope ndoa. Fungeni ndoa za kimila. Kwa kufata taratibu za makabila yenu. Kama una pesa nyingi Usije ukajiroga ukampandisha kanisani sister du wa kisasa cheti cha ndoa kikapigwa muhuri wa kanisa.
 
Mm nitafanya hv
Mke wa kwanza ndoa itakuwa ya kidini,
mke wa pili ndoa itakuwa ya kimila,
mke wa tatu ndoa utakuwa ya kiserikali,
mke wa nne nitasusiwa na wazazi wake baada ya kufumaniwa na mwanao.
 
Hivi kuna wanaume bado wanaoa...??😯
Sasa kwanini wanaume mnakubali kuingia kwenyw ndoa wakati mnateseka hivi...??
Mie nilisha washauri sana, hakuna haja ya kuoa, ebu muishi kama mimi....
 
Back
Top Bottom