Baraza la Ulamaa latengua uamuzi uliovunja Ndoa ya Dkt. Mwaka

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
IMG_1852.jpg
Uamuzi huo umetolewa baada ya Baraza hilo kukutana kwa dharula na kutamka kuwa Ndoa ya Juma Mwaka Juma ‘Dr Mwaka’ na mke wake Qeenie Oscar Masanja haijavunjika kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika Ofisi ya Qadhi.

Taarifa ya Baraza inakuja ikiwa ni siku chache tangu Kikao cha Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Sheikh wa Mkoa, Alhadi Mussa Salum kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka.

Kwa mujibu wa Kikao cha Sheikh Alhadi Mussa, Ndoa hiyo ya Dkt. Mwaka ambaye Mtaalamu wa Tiba Mbadala, na mkewe Queen Masanja ilivunjwa Jumatano, Januari 25, 2023.

=============

Ndoa ya Dr. Juma Mwaka Juma na Mkewe Queen Oscar Masanja haijavunjika, limesema Baraza la Ulamaa lililokutana kwa dharura leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni siku chache toka Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam atangaze kuvunjika kwa Ndoa hiyo.

Taarifa ya Baraza hilo kwa Vyombo vya Habari leo imesema baada ya kuliangalia kwa kina swala la Ndoa hiyo limefikia maazimio ya mambo manne ambapo moja ni kuwa Ndoa hiyo haijavunjika hivyo kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika ofisi ya Qadhi, malalamiko hayo au kesi hiyo iendelee katika ofisi ya Qadhi na Baraza la Ulamaa litafuatilia kwa karibu kinachoendelea.

Azimio la pili la Baraza hilo ni kuwafahamisha Waislamu popote pale walipo wasisite kufanya mawasiliano na Baraza la Ulamaa popote pale watakapoona kuna upindishwaji wa mambo huku azimio la tatu likiwa kuwakumbusha kuwa Muhimili wa Mahakama ya Qadhi ni Muhimili muhimu na ungojitegemea hivyo sio sahihi maamuzi yake kuingiliwa na Mamlaka za BAKWATA Wilaya au Mkoa, na pale suala litakaposhindikana katika Mahakama ya chini suala hilo litapanda katika ngazi ya juu ndani ya Muhimili huo na si vinginevyo.

Azimio la nne ni msisitizo wa Baraza la Ulamaa kwamba utaratibu uliowekwa wa mgawanyo wa madaraka kuanzia katika ngazi zote ni muhimu utaratibu huu ukafuatwa na kudumishwa kwa aili ya kuchunga dhana nzuri ya utawala bora ndani ya Baraza.

MWANANCHI
 
Dr anamkomoa tu huyo demu. Sema na demu mwenyewe inaonekana tegemezi vinginevyo angepiga kimya akaanze maisha hata huko South Africa.
Namuelewa sana huyo dada utegemezi mbaya sana Mungu amsaidie.
 
Bakwata wanajinasibu na mahakama ya kadhi ilihali wakijua ni mahakama ya geresha tu isiyo na meno, wameshindwa kupigania mahakama ya kadhi yenye meno kama ilivyo Kenya, Zanzibar na nchi nyingine kadhaa hata zile zenye waislamu wachache lakini katiba zao zimeruhusu uwepo wa mahakama za kadhi na maamuzi yake kuheshimiwa sio Bongo.
Masheikh wa Bakwata wanajitafutia madhambi ya bure kuingilia ndoa za watu wakati hawana chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo.
 
Uamuzi huo umetolewa baada ya Baraza hilo kukutana kwa dharula na kutamka kuwa Ndoa ya Juma Mwaka Juma ‘Dr Mwaka’ na mke wake Qeenie Oscar Masanja haijavunjika kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika Ofisi ya Qadhi.

Taarifa ya Baraza inakuja ikiwa ni siku chache tangu Kikao cha Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Sheikh wa Mkoa, Alhadi Mussa Salum kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka.

Kwa mujibu wa Kikao cha Sheikh Alhadi Mussa, Ndoa hiyo ya Dkt. Mwaka ambaye Mtaalamu wa Tiba Mbadala, na mkewe Queen Masanja ilivunjwa Jumatano, Januari 25, 2023.

=============

Ndoa ya Dr. Juma Mwaka Juma na Mkewe Queen Oscar Masanja haijavunjika, limesema Baraza la Ulamaa lililokutana kwa dharura leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni siku chache toka Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam atangaze kuvunjika kwa Ndoa hiyo.

Taarifa ya Baraza hilo kwa Vyombo vya Habari leo imesema baada ya kuliangalia kwa kina swala la Ndoa hiyo limefikia maazimio ya mambo manne ambapo moja ni kuwa Ndoa hiyo haijavunjika hivyo kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika ofisi ya Qadhi, malalamiko hayo au kesi hiyo iendelee katika ofisi ya Qadhi na Baraza la Ulamaa litafuatilia kwa karibu kinachoendelea.

Azimio la pili la Baraza hilo ni kuwafahamisha Waislamu popote pale walipo wasisite kufanya mawasiliano na Baraza la Ulamaa popote pale watakapoona kuna upindishwaji wa mambo huku azimio la tatu likiwa kuwakumbusha kuwa Muhimili wa Mahakama ya Qadhi ni Muhimili muhimu na ungojitegemea hivyo sio sahihi maamuzi yake kuingiliwa na Mamlaka za BAKWATA Wilaya au Mkoa, na pale suala litakaposhindikana katika Mahakama ya chini suala hilo litapanda katika ngazi ya juu ndani ya Muhimili huo na si vinginevyo.

Azimio la nne ni msisitizo wa Baraza la Ulamaa kwamba utaratibu uliowekwa wa mgawanyo wa madaraka kuanzia katika ngazi zote ni muhimu utaratibu huu ukafuatwa na kudumishwa kwa aili ya kuchunga dhana nzuri ya utawala bora ndani ya Baraza.

MWANANCHI
Mtu kama amesema hamhitaji mwenzi wake tena hapo hata likija Baraza la majini hakuna kitakachofanikiwa
 
Dr anamkomoa tu huyo demu. Sema na demu mwenyewe inaonekana tegemezi vinginevyo angepiga kimya akaanze maisha hata huko South Africa.
Tatizo sio utegemezi ni tabia tu za watu, wangapi wanapesa na anamuezesha mkewe bila shida yeyote shida ni mmeingia vipi kwenye ndoa labda umepata mwenza kama mwarobaini ukizani ni mpera
 
Huyo mwanamke kapata sponsor Sasa anaona Dr atamletea kauzibe bila kutoa talaka atashindwa kujiachia
Vijana tafuteni pesa na wekezeni kwenye vitega Uchumi kama Nyumba na government bonds. Mke hawezi kukimbia ukiwa na elimu, pesa na PUMZI
 
Back
Top Bottom