Ndoa ya chadema na sabodo si mtihani tosha kwa upinzani?

Jamani tuache unazi wa Simba na Yanga,mleta hoja huenda anakiona mbali kwani hawa jamaa( "waasia wenye asili ya Tanzania") wako kikazi zaidi.
my take:Tuwe makini
 
Ninaandika kutoa masikitiko yangu hapa jf,mashabiki wa ccm wamepungua sana kama sio kwisha kuna post zingine hutawaona kabisa.mmekwiba sana pesa zetu for 50yrs hata kutetea chama chenu mnashidwa hata nape ndio usiseme,mbona kipindi cha uchaguzi kule arumeru mlikuwa wengi hadi mkaweka rehani uhai wenu endapo dm ingeshida? Njooni tuwavue hizo gamba!
Usiwe na wasi wasi mkuu mbona tupo kwa sana tu.
Tatizo ni posti nyingine hazina kichwa wala miguu na inaelekea zimeandikwa na vijana wa CDM wenye level of thinking ya chekechea.
Hao tunawapa uwanja watukane saizi yao, huwezi bishana na mtu ambaye uelewa wake ni below standard. kwa taarifa yako mimi nilikuwa wa kwanza kuwapongeza CDM kwa kushinda Arumeru.
Tatizo tu ikawa kumbe hata CDM wamechagua uozo, kijana tuliyedhani ni kichwa kumbe kichwa cha mwenda wazimu.
 
source: mpayukaji.blogspot.com




Hakuna ubishi kuwa ndoa ya anayeitwa mfanyabiashara maarufu kwa jina la Mustafa Sabodo imeshika kasi. Kwa wanaojua jamaa zetu hawa walivyoletwa na kuchuma, anahofia usafi wa huyu jamaa anayesifika kutumia jina la marehem Mwalimu Julius Nyerere kujinufaisha. Anajiita mpenzi wa Mwalimu ambaye wakati wa uhai wake hata hivyo hatukuwahi kumsikia.

Je hii ni janja ya wahindi kuanza kutafuta pa kushika baada ya kuona CCM ikiyoyoma? Je kama wameitosa CCM iliyowalea na kuwakumbatia hadi wengine kuzawadiwa ubunge, CHADEMA ni nani wasiifanyie hivyo?

Je nao falsafa yao ni ya 'Sina adui au rafiki wa kudumu bali maslahi'?

Mwanzoni Sabodo aliahidi kuwapa CHADEMA jengo lake la Mwenge. Ghafla amepiga U-turn na kusema eti atawajengea ofisi. Tusije tukaruka mkojo tukaishia kukalia manonihino. Ndoa ya Sabodo na CHADEMA inabidi iangaliwe isijekuwa ni mtego wa CCM kumtuma kada wake kuwachafua. Kama Sabodo anaipenda CHADEMA anangoja nini CCM? Kimsingi anataka kuweka vyama vyote mfukoni mwake.


Sabodo alikaririwa akisema, “Kwa kweli nimefurahi sana kunialika kwenye mkutano wenu, nimeshawahi kuisaidia CCM, lakini hawajawahi kunishukuru kama mlivyofanya ninyi.”Je hii ni sababu yenye mashiko kumfanya aipende CHADEMA hivyo au anaandaa pa kushika baada ya CCM kujiishia?


My take: Nimeshindwa kuipuuza habari hii

Huyo mdosi dawa yake ndogo, nina uhakika akileta za kuleta atatembelewa na vijana wa TRA kujua kodi anayolipa katika biashara zake.
 
Back
Top Bottom