Tetesi: Ndoa ya Azam tv na serikali kupitia chanel ya azam 2 hawarushi taarifa ya habari na wao hawarushi LIVE matukio ya serikali

Leseni walionayo haiwaruhusu kufanya live Broadcasting kwa hapa Nchini, leseni yao ya urushaji wa matangazo ya moja kwa moja haikuwa ya hapa Tanzania.

Sijui kama umeelewa.
kwahiyo sisi wapenzi wa kabumbu ndio basi tena... tuna pata uzoefu mwingine kama tulioupata huku JF... daaah
 
Tangu azam warushe tukio la kupokelewa ndege na baada ya siku chache wakaacha kurisha taarifa ya habari ma badala yake wanaelekeza watu wakaangalia taarifa ya habari kwenye App.

Mwanzo tulidhan ni tatizo la siku moja au mbili lakin sasa linaenda wiki ya pili na wao hawatoi tariifa nyigine zaid ya kusema ipo nje ya uwezo wao kama wachunguzi wa mambo tumeanza kuunganisha dots..

Zamani ilikiwa ni nadra sana serikal iwe na shughuli na azam wasiruke nayo hewan iwe ikulu au wapi mikutano yote ya Rais walikuwa wanarusha live lakin matukio yaliyokea hapa katikati hawajaangaika kurusha live...

Nawaza mengi haswa ukizingatia na aina ya utawala tulionao na mtazamo wao juu ya vyombo vya habari...je wamesimamishwa kurusha habari? Kuna habari iliwakera wakubwa?

Mamlaka zinasemaje mimi nalipia huduma ya king'amuzi halafu napangiwa cha kuangalia naambiwa nikaangalie kwenye App na yaan nilipe huduma mara mbili mbili..!

NB:nazugumzia taarifa ya habari sababu kwa upande wangu ndio taarifa ya habari ambayo ipo live zaid na ina mambo mengi yanazungumzwa kwa kina kuliko wote hali ilimifanya sasa hivi nashindwa kuangalia taarifa za chanel zingine naona maluwe luwe..!

Kwa mwenye kujua kinachoendelea atujuze mimi nimeunganisha dots tu.!
Acha kelele. Uza hicho kingamuzi kama vipi.
 
Leseni walionayo haiwaruhusu kufanya live Broadcasting kwa hapa Nchini, leseni yao ya urushaji wa matangazo ya moja kwa moja haikuwa ya hapa Tanzania.

Sijui kama umeelewa.
Kwaio Live Broadcasting ya taarifa ya habari kipindi cha nyuma wakati wanarusha habari ilikua wapo kwenye kipindi cha maangalizi au
 
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe

INAWEZEKANA ikawa ni kwa sababu hiyo! Maana AZAM tv ipo kwenye kundi la DStv, hawapo kwenye kundi la local tv nyingine! kwa hiyo masharti ya leseni zao huenda yakatofautiana. Lakini si wazungumze, wapeane masharti na wakubaliane ili Maisha yaendelee?
 
Hii waliijua lini hao Serekalee
 
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe
Exactly na mimi ndo nilisikia hivyooo
 
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe
mbona mpira wanaonesha live? Au unamaanisha nini kwenye live broadcasting
 
INAWEZEKANA ikawa ni kwa sababu hiyo! Maana AZAM tv ipo kwenye kundi la DStv, hawapo kwenye kundi la local tv nyingine! kwa hiyo masharti ya leseni zao huenda yakatofautiana. Lakini si wazungumze, wapeane masharti na wakubaliane ili Maisha yaendelee?
Hiyo kweli mkuu nimekusoma
 
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe
Kwa hiyo kumuona Messi mubashara ni dhambi?
 
kama kuna mtu anadhani hili jiwe ni nema Mungu ametupa basi ajitafakari mara mbili....
 
Back
Top Bottom