Tetesi: Ndoa ya Azam tv na serikali kupitia chanel ya azam 2 hawarushi taarifa ya habari na wao hawarushi LIVE matukio ya serikali

Half Genious

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
491
784
Tangu azam warushe tukio la kupokelewa ndege na baada ya siku chache wakaacha kurisha taarifa ya habari ma badala yake wanaelekeza watu wakaangalia taarifa ya habari kwenye App.

Mwanzo tulidhan ni tatizo la siku moja au mbili lakin sasa linaenda wiki ya pili na wao hawatoi tariifa nyigine zaid ya kusema ipo nje ya uwezo wao kama wachunguzi wa mambo tumeanza kuunganisha dots..

Zamani ilikiwa ni nadra sana serikal iwe na shughuli na azam wasiruke nayo hewan iwe ikulu au wapi mikutano yote ya Rais walikuwa wanarusha live lakin matukio yaliyokea hapa katikati hawajaangaika kurusha live...

Nawaza mengi haswa ukizingatia na aina ya utawala tulionao na mtazamo wao juu ya vyombo vya habari...je wamesimamishwa kurusha habari? Kuna habari iliwakera wakubwa?

Mamlaka zinasemaje mimi nalipia huduma ya king'amuzi halafu napangiwa cha kuangalia naambiwa nikaangalie kwenye App na yaan nilipe huduma mara mbili mbili..!

NB:nazugumzia taarifa ya habari sababu kwa upande wangu ndio taarifa ya habari ambayo ipo live zaid na ina mambo mengi yanazungumzwa kwa kina kuliko wote hali ilimifanya sasa hivi nashindwa kuangalia taarifa za chanel zingine naona maluwe luwe..!

Kwa mwenye kujua kinachoendelea atujuze mimi nimeunganisha dots tu.!
 
Last edited by a moderator:
Azama kuna mkono wa jiwe sio rahisi kujimaliza wenyewe, jiwe limeingiza mkono wake
 
Kutakuwa kuna jambo na leakage ya hilo jambo imedhibitiwa. But time will tell
 
Kuna wakati inabidi ufungue channel za ajabu ajabu au uunge picha kuliko kuangalia mawazo yao, sie ni walaji hivyo wanatakiwa watupe vitu ambavyo ni palatable kwetu sio walete vitu wanavyotaka wao
 
saiv waandishi wa habari na vyombo vya habari vinafanya kazi kwa taabu sana,hata ukienda kufanya interview unaambiwa kabisa hiki na hiki usizungumzie maana ukizungumza utatuachia msala.TCRA wanatandika faini za kimya kimya alafu za hela mingi na onyo juu.
 
Azam walitakiwa wawe na channel moja ya bure itakayo onesha habari, sio king'amuzi kikiisha na channel zote zinakata ! Tatizo lipo hapo
 
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe
 
Nimemsoma mtoa mada na nimekusoma wewe, bado...!
 
Ndivyo ilivyo kumbe nawe umeling'amua hilo.
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe
 
Inasemekana leseni yao ndio ilikuwa na shida, haikuomba urushaji wa matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) isipokuwa uzalishaji wa vipindi tu (production) na serikali ikapitia mwanya huo kujustify usimamizi wake..so ni kosa la kiufundi walilosababisha Azam wenyewe
Hawa jamaa waliopo serikalini wangekuwa wanatumia akili hizi kwenye maendeleo tungekuwa mbali sana .
Ila wanatumia akili nyingi sana kukomoa mambo yanayowahusu wananchi moj kwa moja
 
Back
Top Bottom