Ndoa sio fasheni..

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
23,557
2,000
Ndoa si msukumo rika, wala kufuata mila,
Ndoa ni kukubalika, bila kufanyiwa hila,
Ndoa si kuhangaika, ili kulipa fadhila,
Ndoa ikikamilika, hutayapata madhila.

Ndoa si kuwa na gari, wala kupanda daraja,
Ndoa isiwe kamari, bali jambo la faraja,
Ndoa isiwe kwa amri, ila ni kuwa wamoja,
Ndoa haitokani na umri, bali nia ya pamoja.

Ndoa sio maigizo, haimei ka uyoga,
Ndoa isiwe likizo, ya kuanza kujikoga,
Ndoa sio bambikizo, hivyo isije kwa woga,
Ndoa ikiwa agizo, kwamwe haiwezi noga.

Ndoa suala la hiyari, si kupigiwa zumari,
Ndoa si kulipa mahari, bali ni kuwa tayari,
Ndoa inakuwa shwari, ifungwapo bila shari,
Ndoa maisha ya heri, yasiyotaka kwaheri

(JJ-8 Mei, 2010; Dar es Salaam, Tunu kwa makapera)
 

Shantel

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
2,020
0
Ndoa sio chai , kila mtu atainywa
inaatakiwa hiyari, hakikisha mnapendana
mambo yatakuwa shwari, ikiwa mnaendana
ndoa ni jambo la heri,mnyaz Mungu amesema
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
Si ndo naona jamaa ameandika uzi anataka kuoa pasipo na penzi. Watu wanaoana na mapenzi kibao na yanachuja; sasa huyu from day one hamna penzi sasa hapo kuna ndoa au kamali. Kha!
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,786
2,000
Ndoa sio chai , kila mtu atainywa
inaatakiwa hiyari, hakikisha mnapendana
mambo yatakuwa shwari, ikiwa mnaendana
ndoa ni jambo la heri,mnyaz Mungu amesema

shanteeeeeeeeeeeel nimekusoma..

Ndoa si riadha, kijiti kupokezana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom