Ndoa nyingi za kikristo zinaitaji kujivua gamba!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa nyingi za kikristo zinaitaji kujivua gamba!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, May 16, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Pengine wawezaa jiuliza kwanini?

  Hii ni hali halisi na ukweli,

  Habarini za asubuhi wapendwa ktk bwana natumaini Mungu amewawezesha kuikwepa folen ya asubuhi hii na kama bado basi si haba waweza tumiia mawazo haya kama stepstone yako kufungulia kinywa.

  Kumekuwa na ndoa nyingiza zenye matatizo na hasa zile zinazofungishwa makanisani, wapo walioamini wanapo olewa watakuwa wakiishi kama peponi. La hasha napenda kuwapongeza wazazi wetu wa nyuma walikuwa wanajitahidi kutimiza upendo wa Agape, leo hii ukiuliza wengi kwa nini unaoa utapata majibu yafuatayo.

  --Nahitaji mtoto

  --Mke mzuri sana aisee siwezi kumuacha

  --Wazazi wameni lazimisha yule ndie atakaenisaidia

  --Ametoka kwa Mungu

  --Nimeshauriwa na shangazi nimuoe

  --Hana hela sana yule binti lazima niweke mambo yangu safi akiwa mkononi

  --Aisee amesoma sana yule binti atatusaidia huko mbele

  Na mengine mengi mno hayawezi kuja yote mahali hapa.

  Sasa basi ukifwatilia kwa karibu utaona akuna Ndoa zenye upendo halisia, na ndio maana shetani anawakamata ndani ya mwezi mmoja mpaka sita amekamilisha kazi yake.

  Kitu cha kwanza ninachoshauri ni vyema kabla ujaoa ujue ama kuuliza wakubwa nini maana ya ndoa?

  Kitu gani kitakufurahisha ukiwa na ndoa yako? Napenda nikujuze shetani nae anaamini na kutetemeka, kama hutamwomba MUngu asimamie ndoa yako utaingia kwenye list ya guiness book kwa walioachwa amakuachika mapema.

  Ukisoma Kitabu cha mwanzo utamuona Rahel, ni wa chache sana leo hii kwenye ulimwengu wa sasa kuliko Leah. Je ni kwa nini kila anaeoa anakamata Leah?

  Je mi matamanio? ni kuoana bila UPENDO wa kweli?

  Ndoa nyingi leo hii napenda kuweka wazi sio kusudi la MUNGU, kusudi la Mungu si mtengane kusudi la Mungu si kuanza kurushiana Ngumi kila siku iitwapo Leo.

  Kusudi la Mungu sio kuabisha watumishi wake. lazima uwe makini unapoomba mke ama mume uombe Mungu akupe kusudi lake.

  Kuna watu wameoana mpaka leo hii hata kusafishana Mgongo imekuwa kituo cha polisi. Hivi jiulize kule mgongoni nani anakusafishia kama utomsafisha umpendao jamani?

  Ukisoma Kitabu cha AMOS kwenye baibo utaona inasema amwezi kutembea wawili kabla hamjapatana. Ndoa nyingi leo hii zimevamiwa na WEKUNDU WA MSIMBAZI, ZIMEVAMIWA NA AINA ZA MAGARI, MAJUMBA YA AINA MBALI MBALI.

  Nini kimepelekea muoane je ni pesa aliokuwanayo mwenza wako? Je ni yale magari, utajiri alio nao? Wewe ndugu yangu wa karibu leo si mbaya kukuweka wazi hakuna Utajiri mzuri kama kuwa na Mke mwema Mwaminifu mkiwa Na MUNGU ndani yake.

  Maisha yenu mnaongozwa na Yesu nakwambia haijalishi una magari mangapi aijalishi umesoma kiasi gani na kama elimu yako ingekuwa ya maana leo hii ma Prof wa mlimani wasingeachika Ndoa zao.

  Hili ni swala muhimu sana kuwa makini usiweke CV yako kwenye Ndoa yako utalia. Dawa muhimu ni kmtanguliza Mungu, haijalishi una elimu gani mwenzio akiwa juu wewe jitahdi uwe chini hata kama ana makosa msubiri mkiwa sehemu ya furaha mjulishe unajua mwenzangu pale uliharibu.

  Sio kwamba atuna shida wengine tulikuwa na hasira mbaya lakini wake zetu wametubadilisha.

  Nanyi wa mama napenda kuwambiia laiti mkikaa katika nafasi zenu nawaambia akuna bar atakayogusa mumeo akuna machangu wataokao mgusa mumeo. Jitahdi ukae nafasi yako mlilie Mungu sema na Mungu usiache kulia kwa Mungu juu ya mwenzako.

  Hakuna aliye sawa kumbuka babako na mamako hawaku zaliwa na wakwe zako, so hamuwezi kuwa na tabia sawa hata siku moja ila yupo mtu mmoja ambae ndie Bwana Yesu mkimwamini nakumtanguliza kwenye ndoa yenu hakuna Raha mtakayo acha kuiona.

  Mwambie Mungu akupe mke kama Rahel, nakwambia Rahel anafungua channel hata kama huna kazi kupitia amani na upendo mlionao nakwambia kazi inakuja. Rahel anafungua channel za biashara eo hii kuna wanawake ukiwaoa ni nuksi tupu lakini na kwambia huyo huyo kama mwanaume ukichukua nafasi yako vyema hakuna atakaenyanyuka juu yako.

  Kwa wanaume kama hamjui siri ya MUNGU wanawake ni DARAJA LA KUTOKEA KIMAISHA KAMA UAMINI MUUZI MKEO UONE, HATA DILI AZIPATAKANI HATA CHANNEL ZINAPOTEA.

  WATCH OUT NITARUDI BAADAE KWA MAELEKEZO ZAIDI. MUNGU AWAPE KUWAPENDA WAKE/WAUME ZENU KAMA MNAVYYOPENDA WENZENU

  MBARIKIWE
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  WATCH OUT NTARUDI BAADAE KWA MAELEKEZO ZAIDI MUNGU AWAPE KUWAPENDA WAKE/WAUME ZENU KAMA MNAVYYOPENDA WENZENU


  P afadhali umesema unarudi baadae.... Hii yaitaji ni print ili niisome kwa ufasaha...lol .. enways nimepita hapa narudi...
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu naomba nitoke nje ya mada kidogo, JE UNAWEZA NIPA TOFAUTI KATI YA LEAH NA RAHEL? NADHANI HAPO NITAELEWA SOMO VYEMA!
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Dah! Nimegundua lilikua ni somo.... hasa kwa akina baba... ingawa kuna contradiction kidogo... Hata hivyo Kwaheri...
   
 5. A

  Aine JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Umeongea vizuri sana sana, ila sijui ni kwanini unazungumzia ndoa za kikristo tu? Kwa hiyo una maana ndoa za kiislam hazihitaji kujivua gamba? Does it mean ndoa za kiislam ziko perfect? au? Please naomba unifafanulie hapo ndiyo niweze kuchangia kama litakuwepo!
   
 6. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  well well said mpendwa ubarikiwe sana nadhani nimepata somo la kutosha nakumbuka mama mmoja kwenye ktpat alisema"wengi wenu mnaomba Mungu awalinde muendako,kazini na mrudi salama nyumbani lkn leo ntawafundisha sala ambayo nayo muhim katika maombi yenu hasa kina mama,mwambie Mungu baba naombea chupi ya Mume wangu,naitakasa kwa damu yako,anapotoka ktk nyumba hii ivaliwe hapa na ivuliwe hapa tu,kama atavua sehemu nyengine tofauti na nyumbani kwangu basi iwe kwa jili ya haja ndogo au kubwa tu,naikabidhi ikiwa safi niliyoifua mwenyewe naomba irudi safi niifue mwenyewe amina."
   
 7. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ndio hivo Pdidy tupo imara na tunasali sana kwa ajili ya wenzetu ila ya dunia nayo mengi, na majaribu mengi pia, kuna wakati tunadondokea uso tunasimama upya na kuendelea na safari, twajaribu kumfikia rahel ila dunia ya rahel na dunia ya sasa ya gaga ina mabadiliko mengi, hivo tunaenda hivohivo kutokana na wakati, na tunamuomba Mwenyezi Mungu atufikishe huko tuendako
   
 8. A

  Aine JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mh Pearl, umeua!!!
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Amen. Asante Mama Mchungaji
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pearl hyo sala imesimama kinyama, nimeipenda na nitaisali kwa ajil ya Gf wangu!
   
 11. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  DUUU! no swimming in pools, body massaging !!
   
 12. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  chezea mm eeeeh?
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kuna haja ya mimi kukuombea namna hiyo hiyo, Mungu baba naiombea Bikini/Thong ya mke wangu naitakasa kwa damu yako anapotoka nyumbani ivaliwe na ivuliwe hapa hapa.Haya sema Amen sasa.
   
 14. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  makubwa so mm mkeo?naona unaleta za kisharo eeeeh?mm ntakuwa barooooooooooo
   
 15. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Dr. Phil tumekusikia
   
 16. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mhh Pearl wewe kiboko! Hii Sala yako! haya wanaume vueni hivyo viatu vya uzinzi na kuvalia makoti wake wa wenzenu!
   
 17. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  hivi inapply hata kwa GF&BF? Mie nilifikiri kwa wandoa tu
   
 18. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Pearl mamii, hata mie umeniacha hoi. What a prayer!!..
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hautaki, unakataa au unajibaraguza??? Lol!!!!
   
 20. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Mwambie Mungu akupe mke kama Rahel, nakwambia Rahel anafungua channel hata kama huna kazi kupitia amani na upendo mlionao nakwambia kazi inakuja. Rahel anafungua channel za biashara eo hii kuna wanawake ukiwaoa ni nuksi tupu lakini na kwambia huyo huyo kama mwanaume ukichukua nafasi yako vyema hakuna atakaenyanyuka juu yako.

  Kwa wanaume kama hamjui siri ya MUNGU wanawake ni DARAJA LA KUTOKEA KIMAISHA KAMA UAMINI MUUZI MKEO UONE, HATA DILI AZIPATAKANI HATA CHANNEL ZINAPOTEA.


  unayosema ni kweli kabisaaa, ukijichanganya utapata nuksi mpaka ushangae na ukibahatika utapata neema mpaka upagawe. 90% ya matajiri duniani walipata utajiri baada ya kuoa...wachache walizaliwa familia tajiri.


   
Loading...