Ndoa nyingi kuvunjika chanzo chake ni kutokuwa na utayari

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Habarini wadau, kama kichwa cha habari kisemavyo

Siku za ivi karibuni kumekuwepo kwa matukio mengi ya ndoa kuvunjika ilihali zengine zikiwa bado chqnga hata miaka 2 hazija fika.
Ni wazi kushamiri kwa matukio haya kunq dhihirisha uwepo mfinyu wa utayari baina ya wanandoa , utayari una zungumziwa hapa ni kumpokea mwenza wako na mapungufu yake, uwezo wa kusamehe, kuvumilia tabia za mwenzako, utambuzi na kuheshimu ndoa bainanya wana ndoa.


N.B : hakuna takwimu halali zilizotolewa mpaka sasa, hivyo mwandishi anatumia nafharia tu.
 
Sikuhizi watu wanaingia kwenye ndoa huku bado wanataka maisha ya ubachelor kwanini ndoa isife
Na nafikiri kwa upande wa ukristu bibble ina maneno makali sanaa kwa wanao vunja ndoa pasipo sababu ya uasherati
Bibble ina sema mume akimwacha mke pasipo sababu ya uasherati na yule mke akakutana na mwanaume mwingine bac ni sawa na wana zini tu .....mathayo 19:9

Sababu tendo la ndoa ni zawadi kwa wana ndoa
 
Na nafikiri kwa upande wa ukristu bibble ina maneno makali sanaa kwa wanao vunja ndoa pasipo sababu ya uasherati
Bibble ina sema mume akimwacha mke pasipo sababu ya uasherati na yule mke akakutana na mwanaume mwingine bac ni sawa na wana zini tu .....

Sababu tendo la ndoa ni zawadi kwa wana ndoa
Sasa wengi wanaoa kufuraisha jamii na sikuhizi wanaume na wanawake wanashindana kuchepuka na hawana hofu kabisa
 
Mi nadhani wengine huwa na utayari wa kuingia kwenye ndoa na wakaingia Ila hujikuta nje ya matarajio...kila kitu kinakuwa tofauti na walivyotarajia mwisho wa siku ndoa huishia njiani.
 
Wanandoa wengi wa kizazi hiki wanapo-fail ni hawapeani muda kuchunguzana,kuna tabia za kurekebishika na zisizorekebishika unazoweza kuzijua kipindi kifupi na kipindi kirefu mf:kauli mbovu,dharau,uzinzi (uzinzi siiweki mmoja wao akiwa na tabia hii hakuna la ziada zaidi ya kum-dump).unapofanya uchumba wa kipindi kirefu kidogo tuseme miaka 2/3 utampa tayari uhuru mwenzako ku-relax kujionyesha alivyo na haraka sana utamueleza ajirekebishe asipojirekebisha immediately unakuwa na maamuzi sasa uchumba wa miezi sita wa nane harusi akija kufunguka ndoani utataka umrekebishe kumbe hilo baya unaloliona leo kwake ndo sahihi hutakuwa na option nyengine ya kufanya umuache au ufe kiume.

Ukitoa kosa kubwa la uzinzi(mwanaume au mwanamke) ndoa ni kitu simple sana kuki-handle kama wote hasa mwanaume akiwa understanding,tukumbuke wote ni watu wazima kila mmoja ana akili zake but msisitizo wangu vijana mnaotaka kuowa tafuteni mabinti mtakaoweza kuwachunguza kwa kipindi kirefu ili muweze kuzisoma tabia zao mapema.
 
Wataendelea kuumiza watoto wasio na hatia kila siku maana sikuhizi hamna upendo watu wanaangalia masilahi yao wakikuta sivyo ndio wanaachana
kila mmoja anamajukumu yake kwenye ndoa sasa niwajibu kwa kila mmoja kuyatiza ipasavyo tatizokubwa nikuepa majukumu
 
Umri wa kuoa kwa mwanaume ni 40 above!

Kikao cha mwisho tulipitisha hili kuepuka kelele hizo zote!
Ni kauli za mtaani tu mkuu mimi niliowa nikiwa aged 27 na maisha yanasogea bila wasi,yupo bro wangu aliowa akiwa 38 sasa hivi ni kama analea wajukuu.

Majukumu hayakimbiwi majukumu yanafuatwa kule yaliko.
 
kila mmoja anamajukumu yake kwenye ndoa sasa niwajibu kwa kila mmoja kuyatiza ipasavyo tatizokubwa nikuepa majukumu
KWA ndoa za sasa ni heri usingle maana waliooa ndo wanatabia chafu kushinda mabachelor, I always wonder shida huwa ni nini hasa
 
mbona hata walio na utayari zinawashinda mkuu? mi nadhani wingi wa mambo katika zama zetu pia kunachangia sana kuvunjika ndoa.
utayari unazungumziwa ni ile hali ya mtu kuitambuq na kuheshimu iyo ndoa, ndoa sio ile tafrija ya siku ya harusi ... Kuishi pamoja na mwenza ndan ya nyumba mojq hqpo sasa ndio maisha ya ndoa baada ya kuihalalisha
 
Siku hiz wanaofunga ndoa ni wachache, wengi wanafanya harusi tu.
Watu wengi tunazania maisha ya ndoa nisawa na maisha ya uchumba, ujana mwingi (uvulana) na ulimbukeni ni chanzo kikubwa cha ndoa nyingi kuvunjika
 
Ni kauli za mtaani tu mkuu mimi niliowa nikiwa aged 27 na maisha yanasogea bila wasi,yupo bro wangu aliowa akiwa 38 sasa hivi ni kama analea wajukuu.

Majukumu hayakimbiwi majukumu yanafuatwa kule yaliko.
Bro analeaje wajukuu, sijakuelewa.
 
Bora usingle tuu
huko nikuta tamaa mkuu maisha ya ndoa yapo vizazi na vizazi ila vijana wa cku hizi hamjui kucheza kwa step unaambiwa cheza kwa step.usimkanyage mwenzio inamaana hata kama mnachepuka basi iwe kwa usir mkubwa na heshima nymbn iwepo kama kawaida sasa unakuta mtu anachati na mchepuko mke au mume yupo hapo hapo kweli jaman

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom