Ndoa ni lazima kupata watoto? Najiuliza sana.

mti wowote bila kuzaa matunda siyo mti..mtoto ndani ya ndoa nikiunganishi cha maagano..acheni kushabikia uongo kuna anayeoa kwa ajili ya kuangalia angel face...najiuliza tu na ndo maana siku hizi hawaingi kwenye ndoa bila kuzini kwanza na kubebeshana mimba....ebo
mbona kuna mambo mengi tu muhimu katika ndoa....? Akili Unazo! unajisikiaje kama utaachwa na mume/mke kwa sababu huzai.. think twice meen !!!
Nitampigia magoti mungu anitoe duniani..Usiombe kukutwa na balaa hili lisikie tu hasa ukiwa kwenye ndoa nazungumzia ukiwa kwenye ndoa ila ukiwa kwenye uzinzi halina maana yoyote ila ukiwa kwenye ndoa acha masiahara wewe..Hakuna ndoa yenye furaha bila mtoto nenda kulia kushoto juu chini hapa tunajifurahisha tu..
Najaribu kujiuliza kama tunaochangia hii mada kama tupo ndani ya ndoa au tunazini..
 
watoto ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu, amini hivyo. Mkuu naona unavyotujibu humu sisi tunaotoa hoja humu ni kama vile una msimamo wako Fulani ktk suala hili na sio km ulivyodai kuwa UNAJIULIZA.....maana ungekuwa unajiuliza ungechukua mawazo ya wadau humu na kuonesha kuwa sasa unaanza kupata majibu....ila ok naona UNA MSIMAMO wako Fulani ambao mimi wala wachangiaji wengine humu hatuwezi kukubadilisha. KILA LA KHERI.
acheni siasa na utandawazi lengo la ndoa zote duniani moja ni kuwa na familia ..definition ya familia ni baba,mama,na watoto..hakuna familia ya mama na baba ..hivyo hakuna ndoa yenye maelewano bila watoto.mlivyozaliwa vivyohivyo mwahitaji kuacha watoto duniani kama wazazi wenu walivyowaweka duniani mpaka mkakutana..ndoa bila mtoto ni dalili ya danguro hata mkiwa na kila kitu hakika bila mtoto hamtakuwa na amani wala nini..fuatilieni na furaha ya ndoa pande zote mbili ni matunda ambayo ni watoto.
 
Ninaamini hakuna hata mmoja ambaye yuko kwenye ndoa miaka zaidi ya 4 na hana mtoto aliyetoa comment yoyote humu. Tunaongea tu ambao hayatuhusu.
 
Inategemea na dhumuni la ndoa yenu kabla yakufunga..
Kama mm nimefunga ndoa kupata watoto na kama ningekosa ningehangaika kwa namna yeyote ile sasa sijui kama wengine mnafunga kwa kugegedana ama vipi!"!"?
 
ndoa ni lazima kupata watoto. ndoa bila watoto ni jehanum, ila unachotakiwa kuelewa ni kwamba watoto ni zawadi toka kwa Mungu, kama Mungu hajakujalia watoto, mdai Mungu usiku na mchana atakupatia hata kama wewe ni tasa au mgumba Mungu atakuponya na kukupatia watoto. Mungu awasaidie.
 
Nitampigia magoti mungu anitoe duniani..Usiombe kukutwa na balaa hili lisikie tu hasa ukiwa kwenye ndoa nazungumzia ukiwa kwenye ndoa ila ukiwa kwenye uzinzi halina maana yoyote ila ukiwa kwenye ndoa acha masiahara wewe..Hakuna ndoa yenye furaha bila mtoto nenda kulia kushoto juu chini hapa tunajifurahisha tu..
Najaribu kujiuliza kama tunaochangia hii mada kama tupo ndani ya ndoa au tunazini..


soma hii signature yako kisha uniambie kama mtoto yupo hapo,,To every successful man, there is a very complicated woman who is causing a headache behind!. Bobi Wine,, hahaha ila asante bro nalijua hilo pia katika ndoa kuna ile kitu kuchokana sema mnapokuwa hamna watoto ni rahisi sana kutupana na kutokuwa na watoto kinaweza kuwa kigezo kikubwa, nipo ndani ya ndoa mwaka wa kumi na tano sasa changamoto tunazopeana wakati mwingine tunajuta kwanini tunao hawa watoto ambao ndiyo imekuwa sababu kubwa ya kutotupana.
 
Ndoa ni mpango wa Mungu tangu mwanzo, na kuzaa na kuongezeka pia ni agizo la Mungu lakini mtoto ni zawadi ya Mungu katika ndoa. Kutoka na kutafuta mtoto nje ya ndoa ni kosa, si tu kisheria bali pia ni uvunjaji wa Amri za Mungu. Imeandikwa usizini.

Mkuu Naomba kuelimishwa kidogo....hili jambo lipo katika sharia ipi ya mwaka gani?
 
Sio lazima inategemea makubaliano yenu,jiulize kwanin mme akiwa na mke ambae hazai mme hutoka na kuzaa kwingine! !
Ndio ujiulize watoto wana umuhimu gan??
 
Kwa tunaoamini ndoa ni kutoka kwa Mungu tunaamini pia kila jema ndani ya hiyo taasisi ni kwa mapenzi ya Mungu,Wapo wachache ambao wameumbwa wagumba lakini kwa walio wengi inaweza kuwa ni sababu ama za kujitakia ama za kupachikwa lakini yooote hayo ndoa iwe ndoa na watoto yawe ni matokeo kama ilivyo kwenye mpira kuna kushinda,sare ama kushindwa

Kama hamjapangiwa mpate watoto hata mfanyeje na ukijifanya kutoka nje ya ndoa tayari wewe umeharibu maana ya ndoa kwani umeiasi kwa kuzini na asiyekuwa wako.
 
Mkuu Naomba kuelimishwa kidogo....hili jambo lipo katika sharia ipi ya mwaka gani?
Sheria ya ndoa Tanzania ya Mwaka1972. Kwa upande wa Dini ipo katika kitabu cha Sheria cha Musa/Moses (Totati/Taurat: Cap 5 Sec.18).
 
Back
Top Bottom