Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Black Rose, Dec 19, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
  1. Black Rose

    Black Rose JF-Expert Member

    #1
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 21, 2011
    Messages: 243
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0

    Usinchekeshe!
    Ina maana waislam watanzania wao hawajiwezi hadi kuchangiwa? Hebu usituangushe.
    Mtumai cha ndugu si hufa maskini?Mahakama ya kadhi tunachoionea mashaka ni kama itaweza kumaliza matatizo ya "kifikra' kwa wanaume wa kiislam hasa kwenye Ndoa.Huu umaskini uliokithiri utamalizwa vipi na hii mahakama? Tatizo ni umaskini wa fikra na mapato unaochangia wanawake wa kiislam kunyanyasika.Salma2015 kauliza maswali ya msingi na hakuna hata mmoja kaweza kujibu hizo hoja.Wanawake wa kiislam hawana tatizo na maagizo ya Kuran au ya Mtume.Wasiwasi ni utendaji kuanzia waumin wenyewe hadi watakaosimamia hizo mahakama.Enyi wanaume, mjue mnatuharibia ibada zetu kwa tabia zenu.Mnalazimisha wanawake wawe na tabia zisizoendana na Uislam kwa vile nyie hamtimizi maagizo.Mnabebesha wanawake mizigo mizito ya "hasira, wivu, chuki" ukiacha mingine ya familia . For you the intellectuals I would confidently say that
    Ndoa kwenye uislam ni ibada.Allah kamuumba "mwanamke" kwa "mwanaume" waishi kwenye ndoa kwa lengo la kuwepo amani, utulivu, raha na faraja.Hivyo basi ndoa inatakiwa izae AMANI NA RAHA.Hii itawezekana kupatikana kama tu wote wanatimiziana wajibu unaowapasa vinginevyo kutakuwa na magomvi yatakayoharibu amani, utulivuna hatimaye kuharibu ndoa (Rejea Kur.30.21).Wanaume mmepewa onyo mkaambia Muogopeni Allah kwa jinsi mtakavyoshi na wake zenu, kwa sababu mumewaoa kwa trust ya Allah! Sasa kama nyie hata hili Onyo hamlizingatii, mnaweza kuwa na uhalali kudai mahakama ya Kadhi ili ati iwaamulie mambo ya ndoa?

    Haya hili la Polygamy nalo ni suala lenye utata.
    Uislam umeweka msisistizo mkubwa kwa haki za watu - mume –mke, na pia zile za Muumba.Kufuatana na Uislam,mke ni life partner and not a robot or husband's property that can be put out of commission or replaced at any time without any consideration, concern, shame or feelings!Uislam haumpi mwanaume yeyote yule a right to have more than one wife nor considers it is an act of piety.
    Mtume mwenyewe alikuwa na mke mmoja tu for about twenty five years kabla ya kuoa wengine,na alimuoa huyu mke akimzidi mtume kwa miaka 15 years.Pigeni mahesabu ndipo mtambue "tamaa" haikuwa sababu ya msingi ya Mtume kuoa zaidi ya Bi Khadija. Hivyo basi kinyume na wanavyodhania wanaume wengi wa kiislam, monogamy is a norm and polygamy a rare exception in Islam. Kuhusisha dini na polygamy ni upotoshaji wa makusudi wa wale wenye kueneza huo utaratibu wa kuoa wake wengi.

    Dini ya Kiislam ni dini ya haki kwa wote na siyo a smoke screen to deceive anyone and or hide behind it to protect personal desires or lust. Wanaume wengi wa Kiislam wanajitafutia uhalali wa vitendo vyao kwa kutumia verses za Kuraan conveniently and selectively bila kusoma ayah kamili na kuwa na uelewa wa kutosha. Ayah inayozungumzia kuoa zaidi ya mke mmoja ina context na imeelezwa uzuri kabisa: Marrying more than one wife was revealed after a battle in which many Muslim men were killed leaving behind helpless widows and orphans. The entire ayah (verse) of Surah (chapter) An-Nisa (The women 4:3), where Allaah The Almighty says; "And if you fear that you shall not be able to deal justly with the orphan-girls, then marry other women of your choice, two or three, or four, but if you fear that you shall not be able to deal justly with them, then (marry) only one……."

    Sasa nyie wanaume wa Tanzania, miaka hii mna sababu gani zaidi ya tamaa zenu kuoa zaidi ya mke mmoja?


     
  2. mgen

    mgen JF-Expert Member

    #2
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 18, 2010
    Messages: 15,150
    Likes Received: 1,882
    Trophy Points: 280
    pande la muhogo litazama kwa uzuri leo! Thanks!
     
  3. Black Rose

    Black Rose JF-Expert Member

    #3
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 21, 2011
    Messages: 243
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Tuwasubiri hao maintelechuoz wenye kulazimisha bila ku cite authority yeyote waje wajibu hiyo niloweka hapo juu.
     
  4. mgen

    mgen JF-Expert Member

    #4
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 18, 2010
    Messages: 15,150
    Likes Received: 1,882
    Trophy Points: 280
    Huyu topicol kwa akili yake ilivyo finyu, hapo badala ya kujibu hoja, angeomba serkali impe ffu ili wakuzibiti!
     
  5. Black Rose

    Black Rose JF-Expert Member

    #5
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 21, 2011
    Messages: 243
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0

    Huwezi wewe ukataka serikali ikukabidhi vyombo vyake kwa matumizi binafsi.
    BAKWATA iliundwa na serikali kama chombo cha Waislam, lakini bado kuna wanaoipinga na kusema hawaitambui.Kibaya zaidi sasa wanataka serikali iingie kuanzisha chombo cha waislam. Ikiwa ndivyo, je hawatakujasema Serikali inaingilia mambo ya waislam?Mimi ningeunga mkono kama chombo hiki kingeundwa na wenyewe.Mwenye kutaka kukitumia akitumie, asiyetaka abaki na option a kutumia vyombo vingine vya serikali.Mpaka kesho mimi nitabaki kwa serikali na mahakama zake na uamuzi wa mtu kuamua anataka mambo yake yasimamiwe wapi.
    Wanataka mirathi nayo isimamiwe na Kadhi courts.Mbona hata sasa inafahamika kabisa ni vipi mali ya muislam itagawanywa. Mwanamke wa kiislam kama sharia ingefuatwa kuanzia mwanzo, angepaswa kuwezeshwa na mumewe wakati wa uhai wa mume kuwa na mali yake mwenyewe. Ina maana pale mume akifariki, mke atapata hicho kithumni au 1/8th ya mali ya mume ambyo ni kidogo kama token na ingetosha. Lakini unakuta mwanaume masikini.karundika wanawake 4, ana kinyumba kimoja, au pengine hana kitu! sasa hicho kithumni kitawasaidiaje wajane hao?

    Pendekezo kwa akina intelechuoz, boresheni hali zenu za kiuchumi kwanza, ili Kadhi courts zikianza, mue na hata kitu cha kuwarithisha watoto zenu na wake zenu.Pia mjue, kiislam watoto wa nje ya ndoa hawarithi kitu.Sasa mbona bado mnazaa kama mmetumwa? Mbona hamuikimbii zinaa kama inavyoagiza Kuran?
    Makatazo mengi bado hamsikii ila pale mnapoona panawapeni ahueni mnapawekea mkazo!
     
  6. mgen

    mgen JF-Expert Member

    #6
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 18, 2010
    Messages: 15,150
    Likes Received: 1,882
    Trophy Points: 280
    Nimeamini JF kweli mahali pa great thinkers kama wewe! nimeheshimu mawazo yako hadi rohoni! Wengi wameshindwa kuwa waislamu kwa sababu ya waislamu! Ukija huku kwetu uswazi utalia, badala ya kuwafanyia Insaafu wanawake wao ndio wanadai huduma! unamuachia mkeo mwenye watoto5 buku, eti afanye maarifa, jioni unarudi mikono mitupu unadai chenji, ukiwa huna basi mkwala wake nitaongeza jiko lingine! story, bao, kahawa, majungu, vijiweni! utasikia yule mwanamke ni laanatullah! kisa kamnyima.....
     
  7. Black Rose

    Black Rose JF-Expert Member

    #7
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 21, 2011
    Messages: 243
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Hii waje wabishe! Wanawasukuma wake zao kwenye zinaa tu halafu wanadai Kadhi courts.Wasafishe kwanza nyumba zao, watii maamrisho ya Uislam ndipo wadai Kadhi Courts.Wanafiki wakubwa! Kwanza wanaaibisha Uislam kwa maana Uislam unampa mwanamke staha kwa mapana yote.Uislam hautaki mwanamke aaibike kwa kujitembeza ovyo mitaani, sokoni na madukani kuombaomba.Mume apaswa kumtimizia mkewe na watoto.Fikiria mwanaume unamlazimisha mkeo kuvaa hijab, kisha unamuachoa buku afanyefanye! Hiyo fanyafanya maana yake nini? Huko sokoni unakotaka aende akajichekeshechekeshe kwa wauza nyanya, vitunguu na mchicha ili tu wewe ule ndio uislam?Halafu unataka kuoa rundo la wanawake - niliuliza utawalisha nini? Au ndio utumwa mamboleo?

     
  8. Black Rose

    Black Rose JF-Expert Member

    #8
    Dec 19, 2011
    Joined: Nov 21, 2011
    Messages: 243
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0

    Sasa wewe skikiza:
    Kasome Surah 4 Ayah 19 uone kwanza Allah katika Uislam hapendi Talaka na anataka talaka iwe ni last resort.Lakini nyinyi wanaume mnapenda kuikimbilia kama kumtishia na kumkomoa mwanamke!Surah 4 Ayah 35 inasema pale ambapo itashindikana kupata muafaka wa matatizo ya ndoa na badala yake kukatawala chuki na uvumilivu ukashindikana, basi talaka yaweza kutolewa.Kadhalika hata mwanamke anaweza kutaka talaka itolewe pale anapoona kashindwa kuvumilia ndoa hiyo yaani mwaname ni mkatili, mume kashindwa kumkidhi financially au mwanamme ni *******. Hebu niambie, pamoja na Quaran kutoa possibilities hizi, utelekelezaji wa haya maagizo kwa wanaume wa kiislam ukoje?

    Talaka ndani ya Uislam ziko tatu
    1.Talak raj'i - hii ndio huitwa talaka rejea
    2.Talak baynounah soghra - huu ni utengano wa muda
    3.Talak baynouna kobra - utengano mkubwa
    Utaratibu unapaswa kufuatwa na ndio maana kama Kadhi courts zitakuwepo, huenda zitasaidia kusimamia kuona hizi talaka zinatolewa ipasavyo na siyo kiholela kama inavyoendelea sasa.Kibaya zaidi wanawake wanakuwa kwenye upande mbaya wa kupokea talaka na jamii inaamini kwamba mwanamke hana haki kutaka talaka.Kumbe wanawake nao wana haki kudai talaka rejea Surat IV Nisa'a -, Ayah 128
    Wanawake na jamii wanahitaji kubadilika kifikra na kupanua uelewa wao wa matakwa ya dini ya Kiislam.Nilitoa mfano wa ndugu yangu aliyepewa talaka mbili - Khul ambapo kulikuwa na uwezekano wa kurudiana na mumewe.Mume yule kwa akili yake mwenyewe, alitoa "talaka 2" akiweka uwezekano wa kumrudia mkewe, ili ati huyu mwanamke asubiri edah na kipindi hicho hakuwa na uhuru wowote.Mkewe naye alikereka sana kukaa edah kisa kumsubiri mume afanye uamuzi.Mke alitaka kuendelea mbele na maisha yake na ndio maana akaenda mahakama za serikali apewe haki yake.
    Nitarudi
    Blackie
     
  9. Safety last

    Safety last JF-Expert Member

    #9
    Dec 19, 2011
    Joined: Mar 24, 2011
    Messages: 4,224
    Likes Received: 164
    Trophy Points: 160
    hawa ndio wanawake wa kiislam tunaowataka wanajibu hoja kwa akili.
     
  10. s

    semako Senior Member

    #10
    Dec 20, 2011
    Joined: Nov 10, 2011
    Messages: 102
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Miongoni mwa watu wanaoishi maisha magumu duniani waarabu ni miongoni mwao,mafuta yanamilikiwa na watu wachache tu sasa wewe muislam mlalahoi wa TZ unategemea kupata msaada acha ushama,nchi ngapi za kiarabu zinataaaabu hayo mafuta kwanini yasitumike?sawa nchi hii ina makafili kama ulivyosema lkn kumbuka hujafa hujaumbika,ulapo jua tumboni mwako kuna........................................like this
     
  11. Memo

    Memo JF-Expert Member

    #11
    Dec 20, 2011
    Joined: Jan 17, 2011
    Messages: 2,147
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 135
    hii thread ya kufungia mwaka.
    Niliomba na kujaribu kuuliza sana, yuko wapi mwanamke wa kiislam anayeongelea hili swala katika ukweli wa moyo wake?
    Tumemuona mwanamke mmoja akiongelea swala la kadhi katika angle ya 'serikali inatuonea' na sio undani wa kiimani na msimamo wake kama mwanamke.

    Hatimae sasa amekuja mwanamke wa shoka, anasema kile ambacho tulikuw tunafichwa....haiwezekani mahakama inayotakiwa kuhukumu mambo yawahusuyo wanawake, mjadala wake usiwahusu wala wasijihusishe kabisa.

    Tunataka na wanawake waliojipambanua kama waislam hapa jf...AshaDii, uko wapi mama, njoo tukisikie.
     
  12. shizukan

    shizukan JF-Expert Member

    #12
    Dec 20, 2011
    Joined: Jan 16, 2011
    Messages: 1,158
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 0
    Ule wakati wa kuwa-rank watu kwa jinsia umeshapita. Wakati Malaria Sugu, Ally Kombo na Topical wanajibu hoja kwa kulazimisha waaminio, leo tunaye MAMA mwenye akili na ufahamu anayejibu hoja kwa vifungu vya kitabu kinachohusu. Kama Waislamu wanataka mtu wa kuwawakilisha mwenye majukwaa ni heri kumchukua mtu mwenye akili zake kama Black Rose. Ila for the way nawajua hawa simple minded people, sasa hivi watasema 'huyu sio muislamu', kisa; anapinga mambo yao.

    Siku zote mtu mwenye busara hujiangalia mwenyewe kwanza kabla hajatoka nje. Mama anasisitiza maadili jamani. Anadai tuboreshe familia zetu na tuondokane na maisha duni. (huku mwanaume mzima bila aibu anasifia waarabu kuwa watamsaidia wakati na wenyewe wana shida zao).

    Waislamu wote wa Tanzania wangekuwa na uelewa wa namna hii, tusingekuwa na jamii duni kama tuzionazo buguruni, tandale na maeneo mengine yenye population kubwa.
     
  13. Z

    Zion Daughter JF-Expert Member

    #13
    Dec 20, 2011
    Joined: Jul 9, 2009
    Messages: 8,936
    Likes Received: 58
    Trophy Points: 145
    Akima topical,MM na wenziwe hawana hoja.Utawaona wakija hapa watavoporomosha maneno yasiyofaa na kuchafua hewa...
     
  14. Safety last

    Safety last JF-Expert Member

    #14
    Dec 20, 2011
    Joined: Mar 24, 2011
    Messages: 4,224
    Likes Received: 164
    Trophy Points: 160
    Huyu black Rose ndio muislam safi ,wale wengine wamekariri kuruan mpaka wamelewa wanalipukalipu tu.
     
  15. Cha Moto

    Cha Moto JF-Expert Member

    #15
    Dec 20, 2011
    Joined: Jul 2, 2011
    Messages: 945
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 35
    we tamaam wallah, mia mia binti!!!!!!!!!
    TOBOA TOBOoooooo.
     
  16. Buchanan

    Buchanan JF Diamond Member

    #16
    Dec 20, 2011
    Joined: May 19, 2009
    Messages: 13,203
    Likes Received: 371
    Trophy Points: 180
    Waislamu cha msingi kwao ni Mahakama ya Kadhi tu hakuna kingine? Hivi huyo Kadhi atatuondolea umaskini tulio nao au atatusaidiaje?
     
  17. s

    sweke34 JF-Expert Member

    #17
    Dec 20, 2011
    Joined: Sep 28, 2010
    Messages: 2,533
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 135
    Mimi hii kitu ya watoto nje ya ndoa kutotambulika kwenye mirathi inanitia huzuni maana ndiyo inasababisha sana uduni wa maisha ya watu wengi. Lakini mwisho wa siku utasikia ni 'mfumo kristo' ndiyo unaleta ufukara ...kumbe ukweli ni kuwa ufukara unasababishwa na viidume vingi vilivyokosa maadili na kujaa zinaa.
     
  18. BADILI TABIA

    BADILI TABIA JF-Expert Member

    #18
    Dec 20, 2011
    Joined: Jun 13, 2011
    Messages: 30,873
    Likes Received: 6,224
    Trophy Points: 280
    dada i salute you. Hawata kuja kujibu hoja hapa. Wamezoea kuleta ubishani usokuwa na tija. Ubarikiwe
     
  19. s

    sweke34 JF-Expert Member

    #19
    Dec 20, 2011
    Joined: Sep 28, 2010
    Messages: 2,533
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 135
    Topical and Co wapo likizo ya Xmas nini?
     
  20. FaizaFoxy

    FaizaFoxy JF-Expert Member

    #20
    Dec 20, 2011
    Joined: Apr 13, 2011
    Messages: 58,103
    Likes Received: 22,143
    Trophy Points: 280
    Nashangaa mpaka sasa Black Rose hujaitwa FF in disguise.
     
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...