Ndoa na malaika wa kifo (Hadithi ya kweli kuhusu mauaji

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,982
2,915
Littleton, Colorado

Ilikuwa tarehe 30, mwezi wa 12 mwaka 1978, ambapo kama kawaida uwa ni msimu wa saruji katika maeneo mengi nchini Marekani ambapo saruji inakua ikianguka, ikiwa ni siku ya kawaida kama zilivyo siku nyingine kwa wakazi wa mji mdogo wa Littleton ulioko katika jimbo la Colorado waliamka na kuendelea na ratiba zao kama kawaida.

Wakati huu huu mji mdogo wa Littleton ulikuwa una wakazi wanaokadiriwa kufikia kiasi cha 40,000. Ulikuwa na mji mdogo kwa kipindi hiki ukiwa umepangiliwa vizuri na wenye utulivu wa hali ya juu ambapo ulifaa zaidi kwa watu wenye familia na watoto kwa ajili ya kuishi kwa kuwa mji huu kipindi hicho ulikuwa kati ya miji yenye matukio machache sana ya uhalifu. Kwa mwaka huo wa 1978, Littleton ilikuwa imekubwa na mauaji ya watu wawili na matukio ya uvamiji na uporaji matatu tu, hivyo utaona kiasi gani mji huu ulikuwa ni mji ambao ulikuwa na matukio machache sana ya uhalifu kwa wakati huo.

Katika familia zilizokuwa zikiishi katika mji huo kulikuwa na familia ya watu wanne ambao ni Robert Splingler akiwa na mkewe aliyejulikana kama Nancy na watoto wao wawili ambaye wakiume alijulikana kama David akiwa na umri miaka 17 huku wa kike akijulikana kama Suzan alikuwa na umri wa miaka 15. Robert akiwa ameajiliwa katika mamlaka ya usambazaji maji, Nancy yeye alikuwa mama wa nyumbani akiwa na jukumu la kulea familia na kuhakikisha majukumu yote ya nyumbani kama usafi, kupika, kufua n.k yanafanyika kila siku.

David yeye alikuwa anapendelea sana mziki huku akiwa anapenda san kupiga gitaa, wakati Nancy yeye alikuwa katika kipindi cha balehe hivyo muda mwingi alikuwa akiutumia kuwa na mpenzi wake ukizingatia muda huo ulikuwa kipindi cha likizo ambapo shule zilikuwa zimefungwa. Kwa mtazamo wa watu wengi hii ilionekana ni familia yenye furaha na ilikuwa ni familia iliyokamilika.

Hiyo tarehe 30, mwezi wa 12 ikiwa ni asubuhi, majirani wa familia ya Splingler wakiwa wameondoka kwa ajili ya likizo ya kuadhimisha sikukuu ya mwaka mpya, mpenzi wa Suzan ajulikanaye Tim aliyekuwa na umri wa miaka 16, aliamua kuja nyumbani kwao Suzan kumtembelea kama alivyozoea kufanya kila siku. Kawaida yao ilikuwa akifika nyumbani kwa akina Suzan alikuwa akichukua saruji na kurusha dirishani kwa Suzan mara tatu na Suzan alikuwa akisikia anakuja kumpokea nje ambapo anamuingiza chumbani kwake.

Siku hiyo baada ya kufika alifanya hivyo hivyo, lakini Suzan hakutokea, hivyo aliamua kuingia ndani kabisa na alishangaa kukuta nyumba ikiwa kimya kama vile hakuna mtu , alihisi uenda watakuwa bado wamelala kwakuwa wazo la kuwa wanaweza kuwa wamesafiri hakuwa nalo kwakuwa jana yake alikuwa na Suzan hakumwambia kama watasafiri na pia walipanga kuonana siku hiyo, na pia kama wangesafiri basi mlango ungekuwa umefungwa kwa funguo.

Tim aliamua kupanda ghorofani moja kwa moja kwenye chumba cha Suzan, na alipoingia chumbani alimuona Suzan akiwa amelala kitandani. Alianza kumuita akiwa kasimama mlangoni lakini Suzan hakuitika jambo lililomfanya Tim avue gloves alizokuwa kava na kumrushia lakini bado Suzan hakuitika wla kujitikisa. Tim aliamua kusogea karibu na kitanda na kwa mshangao ndipo alipogundua kuwa mwili wa Suzan ulikuwa kwenye dimbwi la damu huku akiwa na tundu la risasi kifuani. Tim alitoka chumbani kwa Suzan mbio na kukimbilia kwenye chumba cha David ili kumtaarifu alichokiona kwenye chumba cha mdogo wake, lakini alipofika alimkuta David naye akiwa kitandani kwake kalala kwenye dimbwi la damu pia, huku uso ukiwa umefunikwa na mto na kifuani kukiwa na tundu la risasi.

Kuona hivyo Tim alitoka ndani mbio na kwenda kupiga namba ya dharura 911, kuwataarifu polisi ambao walifika mara moja kwenye eneo la tukio. Askari polisi kutoka katika kituo cha polisi cha Arapahoe wanafika eneo la tukio na kukutana na hali ya tukio la kutisha. Kwa mazingira ya awali ya uchunguzi wa polisi ilionekana Suzan alikuwa kapigwa risasi ya kifuani kutoka kwenye bunduki iliyokuwa mbali kidogo kwa inches kadhaa toka alipokuwa amelala nah ii ilimfanya akate roho kwa haraka sana. David pia naye alikuwa kapigwa risasi moja tu kifuani kwake, ambayo iliondoa uhai wake.
Katika kuzidi kupekuwa nyumba, polisi walielekea upande wa chumba cha chini cha nyumba hiyo ambapo walikuta mwili wa Nancy ukiwa umekaa kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza yenye type writer, huku kichwani kukiwa na tundu la risasi. Pembeni kidogo ya mwili wake, sakafuni kulikuwa na bunduki ndogo, na kwenye mashine ya type writer kulikuwa na karatasi, ambapo walipoichomoa waligundua ilikuwa ni barua iliyoonekana kuandikwa na Nancy akikiri juu ya kutenda mauaji hayo pamoja na sababu zilizomfanya kutekereza mauaji hayo kasha kujiua, na mwisho mwa hiyo barua ilikuwa imesainiwa kwa peni kwa kuewekewa herufi“n” ambapo polisi walihisi imetokana na herufi ya kwanza ya jina la Nancy.

Katika maelezo yaliyokuwa kwenye hiyo barua Nancy alidai ya kwamba alipata hiyo bunduki ya mumewe kwa bahati mbaya na alipoipata aliamua kutenda jambo hilo kwakuwa walikuwa wanataka kutengana na walikuwa wakibishana ni nani hasa atakayebaki na watoto na Nancy anadai hakuwa tayari kuishi bila watoto wake hivyo aliamua bora awaue nay eye ajiue.

Barua yote ilikuwa imechpwa kwa mashine isipokuwa saini ya herufi “n”, na kwa kuitazama haraka haraka ile ule ujumbe ulikuwa unatosha kutumika kama ushahidi kuwa Nancy ndiye alitekereza mauaji hayo ni kasha kujiua mwenyewe kwa sababu alizozitoa kwenye hiyo barua. Lakini polisi hawakutaka kufikia tamati haraka kwa kuchukulia huo ushahidi kama ndicho kigezo tosha cha kukubari kuwa Nancy ndiye katekereza mauaji.

Jack Swanburg, aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi cha Arapohoe, anadai kwamba kosa kubwa ambalo polisi wengi hufanya ni kufikia hitimisho kwa kufanya maamuzi yao binafsi pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha au kutazama ushahidi wote uliopo. Anazidi kusema kwamba ukifanya upelelezi huku kichwani ukiwa tayari na hitimisho binafsi basi huo upelelezi lazima ukupe matokeo yasiyo sahihi.

Kutokana na polisi kutotaka kufikia hitimisho kwa kutumia tu ile barua waliyokuta kwenye type writer, waliendelea kukusanya ushahid wote ulionekana kuwa unaweza kusaidia katika kutatua kesi hiyo ambayo ilikuwa mbele yao. Mpiga picha wa polisi alianza zoezi la kupiga picha eneo lote la tukio na kama kawaida utaratibu wa upigaji picha uanza kwa kupiga picha eneo lote, kasha uendelea kwa kupunguza ukubwa wa eneo mpaka kufikia kupiga picha kitu kimoja kimoja mfano tundu la risasi peke yake, bunduki peke yake n.k.

Aina ya silaha iliyokutwa sakafuni pembeni ya Nancy ilikuwa bunduki ndogo ijulikanayo kama 38 caliber Smith Mansen, ambapo nayo ilipigwa picha na mpiga picha wa polisi. Bunduki ilikuwa kama foot sita kutoka mwili wa Nancy ulipokuwa umekaa pale nyuyma ya meza kwenye kiti. Hii ilikuwa siyo jambo la kawaida kwamba mtu ajipige risasi ya kichwa kasha bunduki idondoke umbali huo kutoka alipo.

Wakati wa mchana mara Robert ambaye hakuwa nyumbani anawasili na kukuta nyumba yake ikiwa imezungushiwa utepe wa njano kuashiria kwamba ni eneo ambalo limefungwa na polisi kwa ajili ya kuchukua ushahidi na kufanya upelelezi baada ya tukio la kiharifu kufanyika pale. Polisi wanamtaarifu juu ya mauaji yaliyotokea nyumbani kwake na anaonekana kusikitika sana huku akijawa na majonzi.

Pia anapoonyeshwa bunduki iliyotumika katika kutekereza mauaji hayo, anakubari kuwa ni bundukui yake na anadai kwamba hakuwa nyumbani wakati tukio hilo linatokea. Katika kuzidi kumhoji polisi wanapata picha tofauti juu ya familia ya Bwana Robert tofauti na ambavyo watu wanje hasa majirani walivyokuwa wakiiona. Majirani na watu waliokuwa wakimfahamu walikuwa wakidai kwamba Robert alikuwa mtu mzuri, mwenye roho nzuri, mpenda watu, mchangamfu, jirani mwema na baba mpenda familia. Lakini kiuhalisia polisi wanagundua hii ilikuwa tofauti na hali halisi katika familia hiyo baina ya Nancy na Robert. Hata wazazi wa nancy hawakuwa wakimkubari Robert walikuwa wanamuona kama siyo mtu sahihi kwa mtoto wao, pia ndani ya familia kulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara baina ya wazazi hawa.

Katika mahojiano kati ya polisi na Robert, Robert anakiri kuwa walikuwa wana ugomvi wa kindoa kwa muda mrefu kiasi kwamba walikuwa wametengana kwa muda na kurudiana hivi karibuni. Anaendelea kudai kwamba chanzo cha huo ugomvi ilikuwa kwasababu Robert alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzake kule ofisini alipokuwa akifanya kazi. Anazidi kudai kwamba japo Nancy alikuwa hapendi uhusiano huo, ila hakutegemea kama anaweza kuchukua maamuzi hayo hata yeye amestaajabu na kuogopa kwa tukioo hilo. Robert anaonekana kutoa ushirikiano wa kutosha kwa polisi na anaweza kueleza kila kitu alichofanya na wapi alipokuwa siku nzima.

Anadai kwamba yeye na Nancy waliingia kwenye ugomvi wa mabishano siku hiyo asubuhi, hivyo aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kuzurura kwa kuendesha gari mitaa mbalimbali ili kupunguza msongo wa mawazo na anadai alitumia kama saa moja au moja na nusu akiendesha gari, baada ya hapo aliamua kwenda sinema kutazama filamu. Kuthibitisha kuwa maelezo yake ni sahihi Robert anakubari kufanyiwa kipimo cha kupima uongo na ukweli. Majibu yanapotoka mtaalamu wa kusoma matokeo ya kipimo hicho anadai kuwa hayawezi kuwasaidia polisi maana hayaeleweki kabisa hivyo hawezi kusema kama alikuwa anongea ukweli au hapana.

Polisi wanaamua kumkagua Robert ili kuona kama wanaweza pata ushahidi wowote unaoweza kumfunga kwenye tukio hilo la mauaji, na kitu walichokuwa wanajaribu kujua ni kuchukua kipimo cha kuonyesha kama mwili wa Robert ulikuwa na mabaki ya mlipuka wa risasi (Gun Powder residue) nah ii ingedhirisha kuwa ni yeye aliyefyatua risasi, au alikuwa karibu wakati risasi inafyatuliwa au uenda aliishika ile bunduki baada tu ya kufyatua risasi.

Kwa kipindi hicho matokeo ya kipimo hicho yalikuwa yanachukua muda kupataikana, ambapo ilikuwa inachukua zaidi ya wiki moja mpaka matokeo kutolewa. Kutokana na kutokuwa na ushahidi na sababu yoyote ya kumshikiria, polisi walimuachia Robert huru, huku wakingojea matokeo ya kipimo cha mabaki ya vumbi la mlipuko wa risasi kutoka katika maabara kinayomilikiwa na kitengo makosa ya jinai cha Colorado

Lakini nyumba ya Robert ilikuwa bado imefungwa polisi wakiendeleakuichunguza kwa ajili ya ushahidi zaidi hivyo hakuruhusiwa kukaa pale, na kutokana na sababu hiyo mkuu wa kituo cha polisi Bwana Jack Swanburg alijitolea kumpa hifadhi Robert ya muda pale nyumbani kwake,na anadai alistaajabu kumuona Robert akiwa ni mtu mwenye utulivu wa hali ya juu kama vile hakuwa kapatwa na tukio la kuogofya la kufiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili tena katika mauaji ya kutisha.

Tarehe 3 mwezi wa 1 mwaka 1979, polisi wanahitimisha kuwa lile tukio lilitekelezwa na Nancy, lakini baada ya siku kadhaa maotkeo ya kipimo cha mabaki ya mripuko wa risasi kutoka yanadhihirisha kwamba Robert anajua zaidi kuliko ambavyo amewambia polisi. Kipimo kinaonyesha kwamba Robert alikuwa na mabaki ya vumbi la mripuko wa risasi wakati Nancy binafsi hakuwa na vumbi hilo mkononi jambo ambalo linaashiria kuwa huenda Robert ndiye aliyefyatua risasi hiyo au alikuwa karibu wakati inafyatuliwa au aliishika bunduki pale baada ya risasi kufyatuliwa.

Polisi wanamwita Robert tena kwa ajili ya mahojiano na mara hii anabadirisha hadithi na maelezo yake ya awali. Anadai kwamba alirudi nyumbani na kukuta tayari mauaji yamekwishatokea, na alipoelekea chumba cha chini alimkuta nancy akiwa amekwishajiua huku bunduki ikiwa karibu na mwili wake. Anadai aliikota akarudi nyumba na kusema Mungu wangu kasha aliidondosha na kutoka ndani amekimbia akaingia kwenye gari lake na kuondoka.

Siku ya tukio wakati polsii wakiendelea na uchunguzi, waligundua uwepo wa alama za matairi ya gari eneo la nyumba ya Robert ambazo zilionekana kuwa zilikuwa zimeachwa na gari ambalo lilikuwa limetoka pale muda siyo mrefu sana kutokana na ukweli kwamba kwakuwa saruji ilikuwa inadondoka kama zilikuwa namuda mrefu zingekuwa zimefunikwa na saruji tayari. Alama hizo zilikuwa zinaonyesha kuwa gari lilikuja na kasha likaondoka hivyo kulikuwa na set mbili za alama ya matairi kwenye saruji, na alama hizo walikuja kugundua kuwa ni alama za matairi ya gari la Robert. Kutokana na maelezo yake mapya na uwepo wa hizo alama, zilithibitisha kuwa Robert alikuwa akisema ukweli kuhusu kuja nyumbani kwake na kuondoka.

Polisi walimuondoa Robert kama mshukiwa wa mauaji hayo na kuhitimisha kabisa kuwa mtendaji alikuwa Nancy, ila familia ya Nancy haikukubari kabisa hili jambo wao waliamimini kwamba Robert anajua ukweli kuliko kile anachowambia polisi. Na mbaya zaidi wakati wazishi Robert alikuja na mwanamke wake kwenye mazishi ambapo miili ya marehemu ilichomwa moto. Watu waliokuwepo walishangaa kwakuwa hakuonyesha dalili zozote za majonzi kama mtu ambaye kapoteza familia yake katika mauaji akiwemo mke na watoto wake wawili.

Pia kabla ya kifo cha Nancy alikuwa amemwandikia binamu yake barua akimwambia kuwa kwasasa yeye na Robert wanaelewana na wako vizuri akiwa anamwambia mipango yake ya baadae na maisha ya mbeleni, jambo ambalo familia ya Nancy inadai kwamba linaonyesha kuwa Nancy hakuwa na mpango wa kujiua ama kuua watoto ndiyo maana alikuwa akizungumzia mipango ya baadaye kweye barua ile.

Hivyo maneno ya chini chini yaliendelea kuzungumzwa na watu mbalimbali katika mji wa Littleton juu ye uhusika wa Robert katika mauaji hayo, lakini japo kuna watu walikuwa na mashaka akiwemo baadhi ya maafisa polisi juu ya Robert kuhsuika katika mauaji hayo, polisi waliamua kufunga kesi hiyo kwa kuhitimisha kwamba Nancy ndiye alitenda mauaji hayo. Bunduki na kila kitu kasoro ile barua ya Nancy vilirudishwa kwa Robert.

Robert hakuchukua muda mrefu alirudi na kuanza kuishi kwenye nyumba yake ambayo mauaji yale yalitekelezwa, jambo ambalo majirani waliona kama ni la ajabu kwakuwa siyo rahisi kwa mtu wa kawaida kuishi kwa amani bila wasiwasi kwenye nyumba ambayo familia yake nzima iliteketezwa. Na kwa mshangao zaidi Robert tarehe 14, mwezi wa 7 mwaka 1979 Robert anaoana na huyo mwanamke aliyekuwa mfanyakazi mwenzake ajulikanaye kama Sheron Cooper na wote wanaishi pamoja kwenye nyumba ya Robert. Robert anawambia polisi kuwa yeye siyo mtu wa kuishi kwenye mambo yaliyopita kwakuwa ni lazima maisha yaendelee hivyo ameamua kusahau mabaya yaliyopita.

Ndoa mpya baina ya Robert na Sheron

Kama ilivyo kawaida ya ndoa inapokuwa mpya, inakuwa imejaa bashasha ya mapenzi motomoto, Robert na Sheron walikuwa na kitu kimoja ambacho walipenda sana kufanya, wote walikuwa wpenzi wa kutembelea na kupanda miamba na milima ijulikanayo kama Grand Canyon (hiking) iliyopo katika jimbo la Colorado. Sheron alikuwa mwandishi wa kitabu maarufu sana kinachojulikana ka ON FOOT of the GRAND CANYON kinachohusiana na muongozo wa kutembelea na kupanda milima na mabonde ya Grand Canyon, hivyo alikuwa ni mtu maarufu katika jimbo la Colorado kutokana na ukweli kwamba watalii na watu wengi walikuwa wamesoma na kutumia mwongozo wa kitabu chake. Hiki kitabu uwapa muongozo wapandaji na watembeleaji wa milima hiyo juu ya hatari inayoweza kuwapata, sehemu za kujiepusha kupita, sehemu zenye miinuko na hatari zaidi pia uwaongoza kwa kuwaelekez sehemu salama za kupita ili kuepuka hatari ya kuanguka na kudondoka.

Robert akiwa na familia yake mpya ambapo alikuwa akiishi yeye mke wake mpya pamoja na mbwa wake wawili, alionekana kuwa ni mtu mwenye furaha kabisa na kuwa alikuwa kasahau yaliyopita na kuanza maisha mapya. Watu wengi wanadai kwamba Robert alikuwa akiwambia kuwa Sheron ndiye mwanamke wa maisha yake, na kuwambia kuwa wanaendana na wana tabia na haiba zinazofanana kwa kupenda vitu na mambo yanayofanana. Sheron alikuwa ni mwanamke anayependelea kwenda kwenye mitoko, mchangamfu na mzungumzaji tofauti kabisa na Nancy, nah ii ilikuwa ni haiba sawa sawa na aliyokuwa nayo Robert hivyo ni kweli walionekana kuendana kabisa.

Lakini baada ya miaka kadhaa ya kuishi Robert na Sheron, mambo yanaanza kwenda kombo na matatizo yanaanza kujitokeza katika ndoa yao. Baada ya baba mzazi wa Robert kufariki, Robert alibadirika kitabia sana kiasi ambacho Sheron alianza kuhisi Robert hakuwa mtu sahihi kwake kama ambavyo alikuwa amefikiria awali, jambo hili lilimfanya Sheron kuwa mtu wa mawazo na kufanya kuwe na kutoelewana katika ndoa yao ambapo mara kwa mara walijikuta wakigombana na kujibizana sana. Inaelekea Bwana Robert hakuwa na bahati na wanawake au huenda wanawake ndiyo hawakuwa na bahati na Bwana Robert.

Mwezi wa 12 mwaka 1986, polisi wanapokea simu kutoka kwa Sheron ambaye anadai kwamba mumewe anamtafuta anataka kumdhuru, hivyo polisi waliwahi na kwenda nyumbani kwa Robert ambapo walimkuta Sheron akiwa kajifungia kwenye kabati la nguo huku akiwa kapandwa presha hivyo ilibidi wamkimbize hospitali. Baada ya ya hili tukio ndoa yao inavunjika kwa kupeana taraka nah ii inakuwa ndoa ya pili ya Bwana Robert kuvunjika katika mazingira yasiyo ya kawaida. Sheron anaamua kuondoka kwenye nyumba ya Robert na kuhama mji wa Littleton.

Lakini taraka hii inamuumiza Robert kwakuwa inamlazimu kugharamia gharama za Sheron za kila mwezi kama mojawapo ya sharti la taraka, kutokana na hilo inambidi Robert arudi kufanya kazi maana kwa kipindi hicho alikuwa ameacha kazi. Kwa sasa Robert alikuwa na umri wa miaka 55, na alikuwa karudi kuwa mseja hivyo bila kupoteza muda anaanza kutafuta mke mpya kwa ajili ya ndoa.

Kutoka na haiba yake na muonekano wake mzuri, haikuwa shida sana kwake kupata mwanamke maana. Robert anaweka tangazo la kutafuta mpenzi kwenye gazeti na kati ya watu waliojibu tangazo lake alikuwa mwanamama Donna Sundlin, mkazi wa mji wa Eveline Colorado ambaye alikuwa kastaafu kazi ya maktaba. Donna na Robert baada ya kukutana wanaanzisha mahusiano moja kwa moja na wanaonekana kila mmoja kumkubari mwenzake.

Mwezi wa 8 mwaka 1990 wanafunga ndoa, na Robert anamshawishi Donna wahamie kwenye mji mdogo wa kitalii wa Durango. Durango ni mji mdogo uliozungukwa na milima na mabonde, watu wengi wanaoishi mji huo ni wapenzi wa kupanda milima na wanajishughulisha na shughuli za utalii. Pia ni mji ambao nao una kiwango kidogo cha uhalifu, umetulia una hali ya hewa nzuri japo umejitenga kwa kuzungukwan amilima lakini una madhari ya kuvutia.

Baada ya kuhamia mji mpya Robert akiwa amefunga ndoa kwa mara ya tatu, walijitahidi kwa kadri wawezavyo kukubarika kwenye jamii mpya, na haikuwa tatizo kutokana na haiba na ucheshi wa Robert aliweza kufahamika kwa kila mtu na alijihusisha kwenye masuala ya mpira wa miguu na kuwa refa katika mechi za kawaida za mji huo. Donna alifanikiwa kupata kazi katika klabu ya mpira ya Durango, wakati Robert naye alipata kazi kama mtangazaji na Dj wa kituo cha redio kidogo cha Durango ambapoa alikuwa akiendesha kipindi cha mziki wa Country, jambo ambalo lilimfanya awe maarufu katika mji wa Durango afahamike na kupendwa na watu wengi.

Lakini Robert mara zote alikuwa hapedi kuzungumzia maisha yake, na ilipomlazimu kujibu maswali juu ya familia yake ya awali, Robert alikuwa akitoa hadithi tofauti tofauti kuhusu ni nini kiliikuta familia yake. Kuna wakati aliwambia watu kuwa mwanaye wa kiume yani David, alikuwa natumia dawa za kulevya na zilimfanya amuue mama yake na dada yake kasha kujipiga risasi mwenyewe, na kuna wakati aliwambia watu kuwa familia yake ilipata ajali ya gari huku yeye ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo na kwamba familia yake yote ilikufa kwenye hiyo ajali isipokuwa yeye tu japo naye aliumia na pia aliwahi wambia baadhi ya watu kuwa mkewe ndiye aliwaua watoto nay eye kasha kujiua.

Inaendelea kwenye comment number 6.
Pia unaweza kusoma makala nyingine kwa kubonyeza link hii Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st kisha subiri kwa sekunde 5 halafu utaona neno next upande wa juu kulia bonyeza hapo ili kusoma
 
Attachments

  • m1.jpg
    m1.jpg
    5.3 KB · Views: 96
  • m2.jpg
    m2.jpg
    13.6 KB · Views: 107
  • m4.jpg
    m4.jpg
    10.5 KB · Views: 104
  • m23.jpg
    m23.jpg
    22.1 KB · Views: 113
Story tamu.. Kwa wale wavivu wa kusoma vitabu najua hapa si mahala kwao.. Nasubiri mwendelezo mkuu.
 
Robert na Donna wanaonekana kufurahia maisha pia wanatumia muda wao wa ziada katika kutembea na kupanda milima, na Robert anaamua kubadirisha mapenzi yake ya kupanda milima kuwa kazi yake ya ziada kwa kuwatembeza na kuwaongoza watalii katika upandaji wa milima na mabonde ya Grand Canyon. Lakini tofauti na Sheron, Donna hakuwa mpenzi wa kupanda milima na kutembela mabonde kwakuwa alikuwa ana tatizo la uoga wa kupanda majengo marefu, milima mirefu hata alikuwa pia muoga wa kuendesha gari kwenye barabra inayopanda milima mirefu au kama barabara ingekuwa inapita sehemu ambapo pembeni kuna maporomoko kama Kasindaga, Donna alikuwa hawezi kupita hapo kwa uoga. Jambo hili liliwafanya Donna na Robert wakati wakiwa wanatembelea milima kuwa wanajiepusha kupanda sehemu za miinuko sana.

Baadae Donna anaamua kuacha kwenda milimani, hivyo Robert anakuwa akienda peke yake, jambo hili linafanya ndoa yao kuyumba kwa maana wanakuwa hawako pamoja muda mwingi Robert anakuwa kazini na akitoka anaenda peke yake milimani. Kutokana na utengano huu, Donna anagundua asipofanya kitu basi huenda ndoa yao itavunjika, hivyo mwaka 1993, Robert anamwambia Donna waende kutembelea milima kwa mara ya mwisho ili wakiwa huko wazungumzo kuhusu mahusiano yao. Donna anakubari japokuwa alikuwa ni muoga ila anaona ndiyo njia pekee ya kuokoa mahusiano yao ambayo anaona kuwa yanayumba. Na siku hiyo walikuwa wanaenda peke yao hawakuwa na watu au mtu wa ziada.

Asubuhi na mapema ya tarehe 11, mwezi wa 4 mwaka 1993 ambayo ilikuwa ni Jumapili ya Pasaka, wanandoahao wanaondoka na kuelekea aktika milima na mabonde ya Grand Canyon, huku Donna akitaraji ya kwamba matembezi hayo ndiyo yatakuwa mwarubaini wa kutibu utengano uliojitokeza kwenye ndoa yao siku za karibuni na kusabbisha matatizo. Jambo ambalo Donna hakuja ni kwamba matatizo ya kindoa kwa Robert yanaweza kuleta matokeo mabaya sana kwa mwanamke. Wakiwa huku Robert anampeleka Donna sehemu ya juu kabisa ya Grand canyon, japo Donna alikuwa anaogopa lakini mara hii aliamua kupandana na uoga wake akiwa na lengo la kuokoa ndoa yake.

Mida ya join Robert anaingia kituo cha polisi akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa na kuwataarifu polisi kwamba kumetokea ajali, ambapo mke wake kaanguka kutoka juu yam lima. Anawaambia polisi kuwa alikuwa akiandaa kamera yake kwa ajili ya kumpiga picha Donna aliyekuwa kasimama kwenye kingo yam lima na alipomaliza kuandaa kamera ile anataka kupiga picha hakumuona Donna na aliposogea na kutazama chini yam lima aliona Donna akiwa ameanguka na kaamua vibaya sana.

Askari na vyombo vya kuokoa wanakimbia kuelekea milimani ambapo mwili wa Donna ulikuwa, mwili wa Donna ulikuwa umeumia vibaya sana na ilionyesha ulijigonga mara kadhaa kwenye miamba wakati akianguka kuelekea chini ya mlima. Na mbaya zaidi hakukuwa na ushahidi wa kujitosheleza kwa ajili ya askari kuchukua. Jambo la kushangaza ni kwamba Robert anawambia polisi kuwa baada ya mkewe kuanguanguka aliteremka chini yam lima akamuosha uso wake uliokuwa umejaa damu kasha akaufunika mwili wake kwa shuka na ndipo akakimbia polisi kuita mdaada.

Kutokana na kutokuwa na shahidi ambaye alishuhudia wakati Donna akianguka maana Robert hakumuona wakati anaanguka, na kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha pale mwili wa Donna ulipokuwa umelala, polisi hawakuwa na jisni zaidi ya kuchukua maelezo aliyokuwa akiyatoa Robert kama ndiyo ushahidi. Baada ya kumhoji Robert kuhusu mambo waliyofanya na Donna siku nzima polisi waliafikia hitimisho kuwa Donna alianguka bahati mbaya. Donna alikuwa kafariki akiwa na umri wa miaka 58, akiacha watoto 5 na wajukuu 5 kutoka kwenye ndoa yake ya awali.

Habari za kifo chake zilisambaa kwa haraka sana kupitia vyombo vya habari, na watu waliona mazingira ya kifo chake hayakuwa sawa walihisi uenda Robert anahusika wengi wakiamini kwamba Robert atakuwa alimsukuma. Na jambo la kusikitisha zaidi Robert anaamuru mabaki ya mwili wa Donna yachomwe moto hata kabla ya ndugu na jamaa zake kufika kuhudhuria mazishi katika mji wa Colorado. Pia watu waliokuwa wakijua kuwa mke wa kwanza wa Robert na watoto wake walifariki katika mazingira ya kutatanisha walizidi kupata mashaka juu ya vifo vya wake wa Robert.

Mwezi wa saba mwaka 1994, Robert akiwa nyumbani anapokea mgeni ambaye ni aliyekuwa mke wake wa pili Sheron. Sheron alikuwa akipitia kwenye wakati mgumu hasa kifedha kutokana na kuachana na aliyekuwa mpenzi wake kwa wakati huo na pia alikuwa ana tatizo la msongo wa mawazo hivyo alirudi kwenye nyumba ya Robert huko Durango na Robert alimpokea na kumpa chumba kwenye nyumba yake. Sheron hakujua uamuzi wake wa kurudi nyumbani kwa Robert utamtokea puani.

Tarehe 2, mwezi wa 10 mwaka 1992 miezi mitatu baadaya ya Sheron kuhamia kwa Robert, Robert anarudi nyumbani na kumkuta Sheron akiwa kaanguka chini hajitambui amelala sakafuni huku pembeni yake kukiwa na karatasi iliyokuwa na ujumbe aliouandika kuelezea sababu zake za kuamua kujiua. Robert anamkimbiza haraka hospitali lakini alikuwa kachelewa na baada ya masaa kadhaa, Sheron anatangazwa kuwa kaaga dunia. Kabla ya kuaga dunia Sheron aliweza kurudiwa fahamu na aliwambia madaktari kuwa alimeza vidonge vingi zaidi ya kiwango kinachohitajika kwa lengo la kujiua.

Hivyo kutokana na hilo, kifo chake kinachukuliwa kama kimetokana na Sheron kuji overdose hivyo hakuna upelelezi wowote unaofanyika kwakuwa alithibitisha mwenyewe kabla ya kufariki kuwa ndiye aliyeamua kumeza vidonge hivyo. Iwe kwa bahati mbaya au kwa kupangwa, kifo cha Sheron ilikuwa ni faida kwa Robert kwakuwa hakuhitajika kuendelea kulipa gharama za Sheron kama ilivyotakiwa na mahakama siku walipotarakiana.

Habari juu ya kifo cha Sheron inapoifikia familia ya Donna, wanaamua kuwasiliana na polisi mara moja. Kutokana na kwamba walikwishakusikia kuwa familia ya Robert ya awali iliteketea katika mazingira ya kutatnisha, na Donna alikufa kwa ajali ambayo pia inastaajabisha kwa kuanguka kutoka juu ya kilima na sasa wanasikia mke mwingine wa Robert kafa katika mazingira ya kutatanisha pia, wao walikuwa wana mashaka ya kwamba kuna jambo lisilo la kwaida linaendelea. Waliendela kupiga simu mara kwa mara wakiwasiliana na polisi na maafisa mbalimbali jambo ambalo liliwalazimu polisi wa Arapahoe kufungua tena faili la kesi ya vifo vya familia ya Robert ya mwaka 1978.

Afisa polisi wa Arapahoe ajulikanaye kama Paul Goodman ndiye anapewa jukuma la kuongoza uchunguzi wa kuchunguza tena vifo vya familia hiyo, ambayo ilikuwa imepotea miaka 15 iliyopita. Lakini katika uchunguzi wao Paul na wenzake wanagundua ushahidi mbalimbali unaoashiria kuwa huenda kile kilichokuwa kimehitimishwa na polisi kipindi kile hakikuwa kweli bali ni tukio la tofauti lililotokea siku ya Jumapili ile ya mwaka 1978.

Kwanza ule ujumbe uilioachwa na Nancy ulikuwa umeeleza kinagaubaga sababu za Nancy kuua watoto wake na kujiua mwenyewe, kitu abacho hakikukuwa kawaida maana jumbenyingi za watu wanaojiua uwa hawatoi sababu kwa kinani kwanini wamechukua maamuzi hayo. Pia ujumbe huo ulikuwa umechapwa kwa mashini ya kuchapia na kusainiwa kwa peni kwa herufi moja tu ya “n” jambo ambalo Robert alidai lilikuwa kawaida kwa Nancy kwakuwa alikuwa na ugonjwa wa Neurones hivyo alikuwa hawezi kushika kalamu kwa muda mrefu na kuandika. Lakini polisi walistaajabu kukuta cheki za benki ambazo Nancy alikuwa kazijaza kwa mkono wake na kusisaini bila tatizo lolote na zilikuwa ni cheki nyingi tu jambo ambalo lilipingana na maelezo ya Robert. Pia polisi walistaajabu kama ikiwa Nancy alikuwa na tatizo hilo basi asingeweza kushika bastora na kulenga mtu kwa usahihi.

Pia tundu la jeraha la risasi ambayo ilipenya kwenye kichwa cha Nancy lilikuwa ni tundu ambalo kwa majibu ya majaribio ya kimaabara kuhusu ukubwa wa tundu la risasi kutoka kwenye bunduki iliyotumiwa kumuua Nancy inapofyatuliwa kutoka katikaumbali mbalimbali kutoka kwa mtu, lile tundu la risasi alilokuwa nalo Nancy lilionyesha kuwa bunduki ilikuwa kati ya inches 6 mpaka nane kutoka kwenye kichwa chake jambo ambalo linapingana na ukweli kwamba mtu anayejipiga risasi husogeza mdomo wa bunduki na kugusa kichwa chake kabisa. Hakuna mtu anayejipiga risasi kwa kushikiria bunduki umbali huo kutoka kwenye kichwa chake.

Kutokana na mambo haya polisi walianza kuhisi kuwa Nancy hakujiua bali aliuawa na hadithi ya Robert ilikuwa ni ya kutengeneza kuficha tukio halisi. Wakati huo huo Goodman alikuw akishirikiana na FBI ambao walikuwa wakichunguza kifo cha Donna kutokana na ukweli kwmaba japo polisi walihitimisha kuwa ilikuwa ni ajali kuwa Donna alianguka kutoka juu ya kilima, ila FBI walikuwa hawakukubariana na ripoti ya polisi hivyo waliamua kufanya uchunguzi wao kimya kimya.

Kutokana na kukosekana kwa mashahidi na ushahid wa kujitosheleza kwenye kesi ya Donna, FBI waligundua kuwa njia pekee ya kupata ukweli ni kwa Robwert mwenye kukiri. Ila walijua siyo jambo rahisi kupata ukweli kutoka kwa mtu kama Robert ambaye kwa zaidi ya miaka 20, amekuwa akikana kuhsuika kwake kwenye kifo chochote kilichotokea. Afisa wa FBI Lenald Jones anaamua kuomba msaada kwa mtaalamu wa tabia za binadamu kutoka katika kitengo cha kuchunguza tabia za binadamu cha FBI.

Mtaalamu huyo anawashauri kwanza wanachotakiwa kufanya ni kufanya uchunguzi wa kina kuhusu Robert wapate kumjua ni mtu wa namna gani, anapendelea nini tabia yake yani watafute na kujua kila kitu wanachoweza kupata kinachomhusu Robert kuhusu tabia na utu wake. Katika uchunguzi wao waligundua kwamba Robert alikuwa mtu anayejiamini, alikuwa ni mtu ambaye alikuwa ana ushawishi na alikuwa ni mtu anayefanikiwa katika kila alichofanya na aliweza kufanya jambo lolote baya na kuepusha kukamatwa kwa kutengeneza mazingira ambayo asingeweza kuhsishwa moja kwa moja na jambo hilo.

Goodman aliendele kufanya kazi kw uakribu na mtaalamu huyo wa tabia za binadamu ili kuweza kupata njia ambayo itawasaidia kuweza kumkamata Robert. Vyombo vya usalama vilikuwa vikimfuatilia Robert bila yeye kujau ambaye kwa sasa alikwua akiishi kwenye mji wa Grand Junction huko huko Colorado, amapo ni mwendo wa saa tatu toka Durango kwa usafiri wa gari.

Grand Junction ni mji mdogo ambao kwa kipindi hicho ulikuwa na watu 50,000 hivyo kutokana na kuwa na idadi ya watu wachache watu wengi walifahamiana na Robert alipohamia hapo alianza kujihusisha na michezo ya kuigiza kwenye majukwaa na hilo lilimfanya awe mashuhuri na watu wengi kumfahamu. Hii ilidhihirisha kuwa mojawapo ya tabia ya Robert ni kupenda kujulikana na kuonekana ni mtu muhimu katika jamii na polisi walichukua hii kama moja ya weakness yake.

Wakati Robert akiwa anaigiza mchezo mmoja wapo jukwaani anagundua kwamba ana tatizo la kukumbuka maneno ambayo anatakiwa azungumze. Anaamua kwneda kwa daktari kupimwa ili tatizo alilo nalo lijulikane na baada ya vipimo kutoka inagundulika kwamba Robert ana ugonjwa wa Kansa. Robert anaiandikia familia yake iliyoko Ufaransa kuwataarifu juu ya hali yake. Hii habari baada ya kuwafikia polisi na FBI wanagundua ya kwamba wana muda mchache inabidi wafanye hima kama wanataka kuhakikisha Robert anakamatwa na kupelekwa kwenye mkono wa sheria.

Mwezi wa 9 mwaka 2000, vyombo vya usalama vinamfuata Robert nyumbani kwek huko Grand Junction, na kwa mshangao wanakuta Robert kaoa mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka 53 ajulikanaye kama Judith. Hii inazidi kuwapa moraari askari kufanya kazi haraka kabla bahati mbaya ya Robert kwa wanawake haijampata Judith. Wanaomba Robert kama atakuwayuko tayari wangependa kumfanyia mahojiano na Robert anakubari kuongozana nao.
tarehe 14, mwezi wa 9 mwaka 2000, Robert anakaa na Goodman na kachero kutoka FBI katika chumba cha mahojiano ambapo wanamfanyia Robert mahojiano lakini hakuna jambomla maana walilopata kutoka kwake. Baada ya masaa kadhaa Goodman anamuuliza Robert kama kuna jambo lolote ambalo angependa kuwambia na jibu lake lilikuwa hapana. Walimaliza mahojiano kwa kumwambia kuwa Robert tungependa kuzngumza na wewe tena na jibu lake lilikuwa ndiyo najua mtazungumza na mimi tena.

Siku iliyofuata asubuhi walipokea sdimu kutoka kwa Robert akawambia kuwa angependa kuzungumza nao tena. Mara hii Goodman anaamua kuhusisha njia ambazo alifunzwa kutoka kwa mtaalamu wa tabia kutoka kitengo cha FBI. Kutokana na kwamba Robert alikuwa na tabia ya kupenda kuonekana ya kwamba ni mtu muhimu ambaye kila mtu anamtazama yeye, siku hiyo polisi waliandaa chumba cha mahojiano ambacho picha zake kadhaa zilizochorwa chorwa kwa kalamu zilibandikwa kulikuwa na maafisa wanne wakiw na kompyuta, kulikuwa na ubao umeandikwa majina yake kulikuwa na videos kamera kadhaa, yani waliandaa chumba ionekane kwamba mahojiano yale ni muhimu sana kuna maafisa wengi na wote wako makini na busy kwa ajili ya kumsikiliza yeye, kulikuwa na mafaili mengi mezani, picha ya Raisi ukutani, alama za nembo ya FBI, maafisa kadhaa wakiwa kwenye simu n.k.

Pia walimwambia kuwa mahojiano yale ni muhimu na polisi wanamengi ya kujifunza kutoka kwake kwa kumfanyia research na kumstudy, na kwamba Goodman alikuwa ni afisamzoefuwa FBI na alikuwa amechunguza kesi kadhaa za maujai ila hakuwahi kukutana na kesi ngumu na ambayo alishindwa kuendelea nayo kama kesi ya matukio ya Robert. Alimwambia kuwa kama angeweza kuzungumzia kuhusu mauaji yale angekuwa kawasaidia sana FBI na polisi maana wangejifunza jinsi gani wangeweza kutatua kesi nyingi.

Jambo hilo lilimfurahisha sana Robert na kujionakweli yeye ni mtu muhimu alieyshindikana hadi polisi wanataka kupata mafunzo kutoka kwake na alipenda kwa jisni gani alivyoonekana kuwa kivutio cha askari polisi wengi na FBI mpaka wametengeneza kikosi kazi kwa ajili yake. Jambo ambalo hakujua ni kwamba huu ulikuwa ni mtego kwake. Wanamwambia ili awasaidie itakuwa vizuri kama atawaeleza ni jinsi gani aliua familia yake na kuweza kuficha ukweli pasipo kaucha ushahidi na pia kuweza kuua wengine wawili hadi kutimiza idadi ya watu watano.

Alipoambiwa hivyo, anamtazama Goodman anamwambia mbona unanipa sifa za mauaji zaidi, mimi nimeua wanne tu na siyo watano kama unavyodai. Robert anakiri kuwa yeye ndiye alihusika na mauaji ya mke wake Nancy na watoto wao wawili David na Suzan. Robert akadai kwamba asubuhi ya tarehe 30, mwezi wa 12, mwaka 1978 aliamka akiwa amekwisha chukua uamuzi wa kumuua mke wake na alimraghai mke wake kwa kumtaka asaini karatasi tupu ambayo aliitumia kuchapa ujumbe wa mauaji polisi walioukuta kwenye mashini ya kuchapa.

Alizidi kueleza kuwa alimfuata mkewe akamwambia kuwa ana surprise kwa ajili yake na alimuoongoza hadi chumba cha chini ya nyumba na kumwambia akae kwenye kiti nyumba ya meza yenye mashini ya kuchapa kasha akamwambia afumbe macho ambapo alitoa bunduki na kumpiga risasi ya kichwa. Na baada ya hapo alielekea ghorofani akiwa na hakika kuwa watoto wake watakuwa wamelala ambapo aliingia kwenye chumba cha Suzan ambaye alikuwa kalala bado na kumpiga risasi kasha alitoka na kuelekea kwenye chumba cha David ambapo alimkuta David alisikia mlio wa risasi na alikuwa kaamka kaka kitandani, naye alimpiga risasi moja na alipomuangalia aligundua bado David hajafa na kwakuwa risasi zilizkuwa zimekwisha aliamua kuchukua mto na kumfunika uso ili kummalizia kabisa.

Polisi walipomuuliza kwanini aliua familia yake alidai kwamba Nancy alikuwa mtu mchoyo sana na mwenye roho mbaya hivyo ilikuwa nibora kumuua kuliko kumpa taraka na kuwa mpenzi wake mpya hakuwa napenda watoto wake hivyo aliona ili aweze kuishi vizuri na Sheron ni bora na watoto awaue.

Polisi walitaka akiri mauaji ya watu wote wanne, hivyo walizidi kumchimba pia awambie ukweli wa hasa ni nini kilitokea kwenye kifo cha mkewe mwaka 1993, yani Donna. Robert aliwambia polisi kwamba hatozungumzia kifo cha Donna kwakuwa ana watoto wakubwa ambao anaogopa kwamba wanaweza vamia na kuharibu mali zake iwapo ataongelea kuhusu kifo cha mama yao. Walijaribu kumshawishi kwa njia mbalimbali na walimwambia kwamba inaonekana angependa kujulikana kama serial killer lakini kwa kukiri kwake kuua familia yake ya mwanzo basi hakumanyi kuwa serial killer.

Hii kauli ilimfanya akubari kuzungumzia kifo cha Donna, alikubari kuwa yeye ndiye alimpeleka milimani makusudi kwa lengo la kumuua kwakuwa alikuwa kamchoka na walikuwa hawaendani tena hivyo kumuondoa maishani mwake bila kuhitaji kugawana mali na kulipia gharama za taraka aliona njia sahihi na rahisi ni kumuua kwa kumsukuma kutoka juu yam lima.

Baada ya mahojiano na kukiri kwake, habari hizi zilisambaa haraka kuanzia Grand Junction mpaka Durango hadi katika mji wa mwanzo alipokuwa akiishi wa Littleton. Kila mtu alitishika na ilikuwa ni habari kubwa kwa miezi kadhaa na watu wengi waliomfahamu walistaajabu maana mebele ya macho ya watu wengi Robert alikuwa mtu safi mstaraabu na mtaratibu hakuna maybe aliwahi kushuhudi upande wa pili wa tabia yake.

Tarehe 5, mwezi wa 11 mwaka 2000, alikamatwa na kuwekwa kuzuizini huku kukiwa na ushahidi wa kukiri kwake juu ya kutekereza mauaji hayo, hakukuwa na haja ya kufungua kesi kwakuwa alikiri kuwa alipanga na kutekereza mauaji ya mke wake wa kwanza na watoto wawili pia alikiri kupanga na kutekereza mauaji ya Donna. Katika siku ya kwanza ya kusikiliza shauri lake, waandishi walijaa sana kwenye chumba cha mahakama na watu wengi na wanafamilia na mke wake wan ne Judith pia alihudhuria. Robert alipoletwa alikuwa akionekana kama yuko kwenye jukwaa la maigizo kwakuwa alikuwa akitabasamu na kumnyia jicho mke wake, na wala hakuonekana kusikitika wala kutazama wanafamilia wa wathirika wa mauaji aliyoyatekereza.

Robert alipewa kifungo cha maisha gerezani bila nafasi yyeote ya parole tarehe 5 mwezi wwa 8 mwakaq 2001. Hii haikuwa adhabu pekee aliyopata Robert, maana miezi tisa tu baad aya kufungwa Robert alifariki akiwa gerezani na huu ndiyo ukawa mwisho wake japo kwa familia ya wale aliowaua hawajawahi kusahau matukio aliyoyafanya.

Mwisho………………….
Pia unaweza kusoma makala nyingine kwa kubonyeza link hii Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st kisha subiri kwa sekunde 5 halafu utaona neno next upande wa juu kulia bonyeza hapo ili kusoma
 
Marekani kununua silaha ni sawa na kununua maji dukani. Mara mwanafunzi anaua wenzie shule. Ukiangalia murder investigation unashangaa
 
Amekamatwa kizembe saaana hakuweza kushtukia mtego na yeye akamwaga mchele wote. Kweli duniani kuna wapelelezi hatari
 
Back
Top Bottom