Ndoa-je ni kawaida kuhisi hivi kuhusu ndoa?

Lizzy my dear, asante nimependa mchango wako.
Nimesema sina ujanja kwa kuwa ninataka kuingia kwenye ndoa na huyu mtu na kuanza familia,nimekuwa mgumu kutoa maamuzi kwa kuwa marafiki zangu wengi wanalalamika kuhusu ndoa zao, nina ndugu wenye matatizo na ndoa zao, na mbaya zaidi mimi binafsi nimekuwa kwenye familia yenye wazazi wote wawili wanaoishi nyumba moja lakini ni afadhali kila mmoja angechukua ustaarabu wake..nadhani nikifikiria hayo yote ndiyo yananifanya niwe mwoga nikidhani na mimi ya kwangu itakuwa hivyo.

ningependa kuwa kwenye ndoa ya mpaka kifo kitutenganishe hilo la mkataba limenijia tu kama solution baada ya kuona kwanini watu wang'ang'aniane matatizo siku zote 365 kesi kila leo!! Namuomba Mungu anisaidie kwa kweli.

Nimekuelewa mwaya. . . .
Ila sasa unatakiwa ujue kwamba hutakiwi kuruhusu hizo failure za watu wengine ziamue matokeo ya ndoa yako, usije ukawa unaona matatizo hata pale ambapo hamna matatizo.Wewe ni tofauti na wao kama alivyo mtarajiwa wako, kwahiyo hata ndoa yenu mnaweza mkaifanya ikawa tofauti kabisa na za wengine.Mnachohitaji ni determination, sio woga na hisia kwamba na nyie mtaishia kule kule.

Anza kuwa na mawazo chanya, hayo mengine futilia mbali kwasababu nyie hayawahusu labda mtake wenyewe.
 
this is very paradoxical - kabla mtu hajatangaza nia, kila siku anakumbushwa ndoa itakuwa lini...sasa jamaa yuko tayari kwa tukio, dada tumbo joto
 
Usiogope,ndoa ni utimilifu wa furaha(mapenzi)...(omba Mungu) jiulize/tafakari kwa kina (mapenzi hutangulia ndoa): unampenda?, anakupenda? ...fikiria kufanikiwa...jenga picha kuwa una kitu unaenda kutoa kama sehemu ya mafanikio ktk ndoa yenu...
 
Kila mtu na bahati yake kwenye ndoa, kwa hivyo na wewe jaribu yako na wala usiogope. Hakuna formula uta deal na issues zitakazojitokeza on case by case basis.

Kuna wanaume wengine ni wema sana na wanaheshimu ndoa zao, unaweza kubahatika ukapata mmoja wapo wa aina hiyo.

Kuna wanaume wengine hata ukiwaramba nyayo basi wao hawana fadhila wala shukurani kwa hivyo inabidi ustahmili ila usikubali kufikia stage ya kuhatarisha maisha yako kwa kuletewa ukimwi.

Vile vile usiwe tena kama mume anafanya hivi basi na wewe lazima ulipize kisasi.

Eeeeeh nisije kugeuza hii kuwa kitchen party
 
Back
Top Bottom