Ndoa isikose amani kwa sababu ya kukosa mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa isikose amani kwa sababu ya kukosa mtoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 12, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  [​IMG]Miongoni mwa matatizo mengi yanyozikumba ndoa nyingi ni kukosa mtoto. Ndoa ni neno lenye herufi nne ambalo ukilichambu kwa undani zaidi utakuta mambo mengi sana, katika ndoa kuna mume na mke, naweza kusema hakuna ndoa isiyo na mke au hakuna ndoa isiyo mume, ndio maana unaweza kusema ndoa ni ukamilifu wa makubaliano ya manaume na mwanamke kuishi pamoja kuwa ni mume na mke kidini, kisheria na kimila.

  Napenda kuweka mambo wazi kwamba ndoa nyingi mpaka leo zina migogoro au zimeshavinjika kutokana na kukosa subira au kujua nini cha kufanya wataki zinapokutana na tatizo la kukosa mtoto. Tatizo la kukosa mtoto linaweza kuwa la mwanaume au mwanamke, si vizuri swala la kukosa mtoto linapotokea katika ndoa mume kumsumbua mkewe kwa kumtaka yeye akapime au kumrushia matusi ya kumwita mgumba na pengine tatizo linawewza kuwa upande wa mwanaume, ni vizuri zaidi kwenda wote kumuona daktari atakaye wapima afya zenu.

  Tunaweza kuelimishana kidaktari katika magonjwa yanayoweza kusababisha mwanamke au mwanaume kushindwa kupata mtoto.

  Mwanamke.
  Magonjwa ya uzazi husababisha mwanamke ashindwe kupata Ujauzito, hasa Upevushaji wa mayai (Infetily) na kukomaa kwa mayai ( Imaturity) Kwamba mwanamke anaweza kupata Fertilizetion lakini mimba ikatoka. Unaweza kujiuliza kwanini inatokea mimba, mimba inaweza kutoka kutokana na magonjwa kama Fibroid ambayo ni misuli au nyama zinazokuwa katika tumbo la uzazi, misuli hii inakula lishe na damu ambayo inahitajika kulisha kiumbe nilichopo kwenye tumbo la uzazi.Hivyo kiumbe ninapokosa lishe na damu kinatoka chenyewe, ndio pale unasikia mimba imetoka.
  Tatizo hili mara nyingi huwa kubwa kwa mwanamke ambaye hajazaa, inaweza kumsababishia asiweze kupata mtoto, japo hata waliozaa wanaweza kupatwa na tatizo hili. Friboid haina tiba ya moja kwa moja kuwa unaweza kupona, lakini tatizo linapokuwa kubwa basi daktari huondoa tumbo la uzazi.

  Matatizo katika tumbo la uzazi, Ablution Placenta. Mimba inatunga lakini baadae inaachia kwenye kondo la uzazi, mtu mwenye tatizo hili akipata mimba haiwezi kukua na kutoa mtoto.
  Mtu mwenye tatizo hili anashauriwa mimba ikiwa changa apate muda mwingi wa kupumzika, asifanye kazi ngumu zitakazomsababishia mimba kuharibika, mpaka utakapofika wakati wa kujifungua.

  Mwanaume
  Mwanaume nae anaweza kukosa mbegu za kiume kutokana na matatizo ya toka utotoni, Inakuwa vipi? Kutokana na korodani kutokushuka kutoka tumboni kwenda sehemu zake za siri wakati anapozaliwa, huweza kusababisha ashindwe kupata mtoto.
  Tiba: Kutokushuka kwa korodani wakati wa kuzaliwa ni kufanyiwa upasuaji mapema mtoto angali akiwa mdogo, akichelewa kutokana na joto la mwili mbegu huharibika na kusababisha kutokupata mtoto.
  Tatizo lingine ni Uasili wa mbegu, (Nature of Sperms) ambao unatokana na umbile la mbegu. Kuna mbegu zenye kichwa butu, zinazoshindwa kupenya kwenye yai la kike. (Ovary).
  Tiba: Uasili wa mbegu hauna suluhisho la tiba maalumu
  2. Mbegu zisizo na mkia ambazo husababisha zishindwe kuogelea kuelekea tumbo la uzazi la mwanamke.
  3. Wingi wa Mbegu, (Sperm count) katika vipimo kwa mbegu idadi ya sperm katika kila mililiter zinatakiwa zaidi ya 25 x 10 per 6. Idadi ikiwa pungufu mara nyingi huwa vigumu Sperms kurutubisha yai.

  Tiba: Kuna dawa zitolewazo na wataalam katika hispitali, mtu mwenye tatizo hili anaweza kwenda hospitali za rufaa. Kuna dawa zake mfano Manix ambazo zinasemekana zinaongeza wingi wa mbegu.
  Napenda kuhitimisha kwa kusema wanandoa wasianze kulaumiana au kutalakia kwa sababu tu ya kuishi miaka mingi bila kupata mtoto, mtu unaweza kuishi miaka mingi bila kupata mtoto akatibiwa na kupata mtoto. Ingawa kweli kuna magonjwa mengine haya wezi kutibika kama nilivyoorodhesha. Mnapaswa wanandoa kuheshimu ndoa yenu na kumwomba Mungu awajaalie kwani tunapaswa kumshirikisha Mungu kwa kila kitu iliaweze kutusaidia shida zetu.
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtoto ni baraka toka kwa mungu.
   
 3. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  japokua sijasoma! thnx.
   
 4. z

  ze Sniper Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umetisha n tenx 4 that!
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Wewe ni aina ya watu wanatia sahihi mikataba bila kusoma. sredi hajaisoma lakini unatoa shukrani. Shauri yako mwenzio kamtukana mama yako mzazi.
   
 6. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hafai kabisa kupewa kazi yeyote labda ya ukinyozi kwani mtenda na mtendwa wanakuwa pamoja
   
 7. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Asante sana.Children are flowers.
   
Loading...