Ndoa imekua ni vita nife nalo au niwaambie wakwe?

Ndio 85% ya jinsia Jirani ilivyo. .... kupata hiyo 15% ni zari la mentali

Ushauri
_________
Jaribu kupunguza muda wa kuwa naye i.e ji - keep bize na mambo yako nje ya nyumbani

Usirumbane naye kwa chochote kwani kujibu making it worse..akianza kuongea wewe komaa na Lap/tab/smart etc

Upo kwa NGO , tengeneza safari ndogo ndogo ambazo zitakufanya usiwe home

CHEPUKA. .. hii mambo ya mke mmoja + pingu ya maisha inatukosti sana hasa sisi wa dhehebu la.... ... kumbuka italeta mtafaruko for sometime but will not last forever

Lastly. .. BE A MAN.
Binafsi nimekuelewa
 
Kwa maono yangu hapo kaka bado wampenda huyo. Hapo huwezi shaurika ni wwe mwenyewe uamue mkuu. Ila angalia kaka samaki mkunje. Kama hujawahi kumwonya kwa vitendo hawezi tikisika hata kidogo. Ila kama ni mimi kaka kutoka tu nyumbani bila taarifa ni kosa la jinai sembuse kulala nje. Jaribu kufikiri baadae itakuaje kabla hujafanya maamuzi coz linaweza kuja kukuumiza mwenyewe. Kwan mnawatoto?
mtoto 1
 
Kwa maono yangu hapo kaka bado wampenda huyo. Hapo huwezi shaurika ni wwe mwenyewe uamue mkuu. Ila angalia kaka samaki mkunje. Kama hujawahi kumwonya kwa vitendo hawezi tikisika hata kidogo. Ila kama ni mimi kaka kutoka tu nyumbani bila taarifa ni kosa la jinai sembuse kulala nje. Jaribu kufikiri baadae itakuaje kabla hujafanya maamuzi coz linaweza kuja kukuumiza mwenyewe. Kwan mnawatoto?
mtoto 1
 
nikimfokea anasema kuwa namnyanyasa kiufupi ameingia katika ndoa akiwa na brain washing ya mfumo dume upo na akienda kwenye msiba akisikia stori za mwanaume ametelekeza familia bas hasira zinakuja kwangu sasa napata wakat mgumu sana
 
Nisiwachoshe,

Ni miaka miwili toka nioe bint toka Tanga,nilijuana nae nikiwa Mwanza yeye yupo chuo fulani cha ualimu mm nikiwa kwenye shughuli zangu ktk NGO,S moja jijini hapo, alionesha ni mcha Mungu tulianzisha mahusiano lakini sikua na lengo nae lakini kadri tulivyoendelea na mahusiano alikua ameficha makucha huku akilalamikia wanaume huwa ni waongo mara hapendi kuchezewa basi nikaona ni malaika wa kuishi nae tukaenda kupima nikawa nakula kama kawaida tulipozoeana alianza kubadilika anakua mkali,mtu wa commanding nikajua atajirekebisha akatulia mwaka 2014 tukafunga ndoa hapo ndipo nilipoanza kuona rangi ya huyu binti ana rangi gani.

Amekua mtu wa kulalamika mlalamishi hata mambo ya kawaida,wivu wa kijinga hata nikiongea na mtu anajudge hata kanisani,katika maisha ya kawaida anapenda kujibizana na mm,akikosea hawezi kuomba msamaha,anapenda kususa hovyo, amekua mtu wa commanding,anachokitaka kifanyike,majibu ya hovyo mbele wa dada wa kazi, tukidiscuss jambo ambalo linatakiwa tufanye maamuz ananiambia wewe si ndio baba fanya utakavyo halaf sasa nikiwasiliana na mzazi wa kike mama akinishauri jambo basi hununa sana na kusema ndoa inaongozwa na mama ,yaani ni mtu wa hasira hasira mda wote mara nikirud kanuna tu,nikiumwa hatilii maanani.

Juzi nimerudi kichwa kinauma nina mawazo mambo yangu ya chuo na mengine anayoniletea yeye akaanza mara mbona nimemkasirikia nikamwambia sijamkasirikia ila nina msongo wa mawazo akasema hawezi kuishi maisha ya hapa mara anahisi nina mwanamke na akasema anaondoka na leo jion kaondoka nimemuuliza dada wa kazi ameniambia amesema anaenda mjini
sasa naombeni ushauri mm huyu nimechoka nimeongea habadiliki kwa chochote anataka kuwa na sauti kunizidi mm,

Je niwape taarifa nyumbani kwa huyu bint niwasimulie yote
au niwaambie na nyumbani kwetu habari zake naombeni ushauri wenu na je kama ameamua kulala nje kuna haja ya kumkaribisha tena kuwa mke?au nikae kimya moja kwa moja au nimpe displine gani itakayo mfanya atambue thamani ya mume tafadhalini ushauri wenu ni muhimu sana

BACKGROUND
Amelelewa katika maisha ambayo hakuoneshwa upendo sana na bibi yake alikua mshirikina na amekua akiwachezea toka mdogo na hata kwenye ufungaji ndoa bibi yule alifanya vimbwanga ili ndoa isifungwe lkn ilishindikana hapo ni sendoff kwanza baadae alifatilia harusi itafungwa wapi akaharibu kumkomoa
Mpaka hapo umetuchosha! Kwa sababu unasoma mshika mbili moja usepa af bado uko naye acha urijar wa ivo...
 
  1. tumekua tukitofautiana amenifanya kuwa mtu wa hasira lkn mkono wangu mzito kumpiga mwanamke but huwa naignore mapenzi najifariji hata akiondoka nitaoa mwingine mara kwa mara hunitishia kuondoka huwa namwambia sijamwambia aondoke ila akiondoka sitamtafuta nitatoa taarifa kwao tu hisia kwake zimeanza kupotea kabisa gubu imepoteza hisia kwake najilaumu kila siku kwa nini nimemuoa ndoa ya kikristo inawaletea kiburi sana wanawake
 
reality
M/Mungu kawaumba wanawake na kuwajaalia akili za utulivu.Wanauwezo mkubwa sana wa kumsoma mwanamume kama ambavyo mama mzazi anavyoweza kumsoma mwanae wa kumzaa. Uwezo wako na mihemuko yako mwanamke atakusoma bila kukubakishia akiba. Ukiona kila unaloliamua kama mwanaume kichwa cha familia, linakuwa baya kwake ama hakutii na mijadala na mikakati ya kimaendeleo unayopanga ama kuomba ushauri wake inagonga mwamba, elewa kunatatizo kubwa.
Fanya yafuatayo; tafuta wazee unaowaamini wewe,uwasimulie kisanga kizima, ili wawasuluhishe. Ukiona kashindikana, suala hilo lipeleke kwa wazee wake ili wawasuluhishe. Ukiona kashindikana na haoneshi dalili zozote za kujutia, elewa alishausoma ubongo wako unapoanzia hadi unapoishia na haumuwezi.
Vipaji vyenu itakuwa vimetofautiana hamuwezi kuishi maisha ya staha na upendo hadi uzeeni. Inawezekana alishakufanya mlishi wake bila wewe kujua, wakati ana mambo mengine kichwani mwake na hana mapenzi na wewe.
Ukitafuta usuluhishi ukaona mwenzio haheshimu, achana nae mapema.
Jinsi ya kumuacha. Hakikisha unatumia njia za talaka za kisheria na uwe radhi kugawana vyote mlivyochuma nae bila upendeleo wala dhuluma.
Ukifanikisha hayo, usije ukakurupuka tena kuoa hawara yako.
Suala la kuoa halitakiwi kukurupuka wala kushinikizwa na mtu yeyote. Tuliza akili zako na umshirikishe Mwenyezi Mungu atakubariki utapata mke mwema na utafurahia maisha ya ndoa. Hatua madhubuti na uamzi sahihi unatakiwa kuyachukua sasa. Utakavyoendelea kuishinae kishingo upande, utazeeka kwa matatizo yasiyo na tija wakati umri wako bado ni mdogo kubeba "mizigo".
 
Kawaida mahusiano ktk ndoa hutofautiana toka mtu m1 hadi mwingine. Kwa maana nyingine ni kwamba hakuna formula ya kuishi kwa wamandoa.

Hivyo kwa tabia kama hizo za mke kutaka kunizidi sauti nikimkanya asikanyike kwangu mm ndiyo mwisho wa ndoa.

Lakini pia aondoke nyumbani bila kunijulisha anakoenda na bado asirudi nyumbani kwa utandawazi huu pasiponijulisha alikolala harudi kwangu.

Lakini kumbuka unasema bibi yake ni mchawi na ana mtimanyongo kuhusiana na ndoa yenu. Huenda bibi kafanya yake na anamwendesha huyo bibie kwa remote ya kichawi.

Hata hivyo bibi kamlea ana sababu gani ya msingi ya kunuonea wivu wa kuolewa? Hii sentence yako haijanikaa vizuri akilini kwangu.
 
sasa wewe kuhusu huyo Bibi wa mke wako ulimfanyia assessment gani mpaka ukagundua kua alitaka kuiharibu ndoa yenu au ndio ulikua unajazwa ujinga na huyo mke wako kua Bibi yake anataka kuiharibu ndoa yenu japokua inawezakana kabisa juu ya hayo mambo lakini ulitakiwa kumfanyia analysis historia yake ya huko nyuma alikua anaishi ktk style gani sio anakujaza maneno Bibi yupo hivi' kwa kukuaminisha na wewe unamini tu" ukizingatia unasema umemfuma zaidi ya mara moja bado tu unataka ushauriwe binafsi yangu namueleza aondoke akigoma mimi naondoka namuachia nyumba naenda kuanza maisha upya na Kila kitu na muachia na beba nguo zangu na vyeti vyangu nikaishi kwa amani
 
Inasikitisha sana kuwa mwanaume lakini unashindwa na maamuzi ya kifamilia. Umelipa Mahari,Unamlisha,Unamvisha,Unaampa raha ya mgegedo na bado analeta jeuri??
 
Back
Top Bottom