Ndoa imekua ni vita nife nalo au niwaambie wakwe?

M/Mungu kawaumba wanawake na kuwajaalia akili za utulivu.Wanauwezo mkubwa sana wa kumsoma mwanamume kama ambavyo mama mzazi anavyoweza kumsoma mwanae wa kumzaa. Uwezo wako na mihemuko yako mwanamke atakusoma bila kukubakishia akiba. Ukiona kila unaloliamua kama mwanaume kichwa cha familia, linakuwa baya kwake ama hakutii na mijadala na mikakati ya kimaendeleo unayopanga ama kuomba ushauri wake inagonga mwamba, elewa kunatatizo kubwa.
Fanya yafuatayo; tafuta wazee unaowaamini wewe,uwasimulie kisanga kizima, ili wawasuluhishe. Ukiona kashindikana, suala hilo lipeleke kwa wazee wake ili wawasuluhishe. Ukiona kashindikana na haoneshi dalili zozote za kujutia, elewa alishausoma ubongo wako unapoanzia hadi unapoishia na haumuwezi.
Vipaji vyenu itakuwa vimetofautiana hamuwezi kuishi maisha ya staha na upendo hadi uzeeni. Inawezekana alishakufanya mlishi wake bila wewe kujua, wakati ana mambo mengine kichwani mwake na hana mapenzi na wewe.
Ukitafuta usuluhishi ukaona mwenzio haheshimu, achana nae mapema.
Jinsi ya kumuacha. Hakikisha unatumia njia za talaka za kisheria na uwe radhi kugawana vyote mlivyochuma nae bila upendeleo wala dhuluma.
Ukifanikisha hayo, usije ukakurupuka tena kuoa hawara yako.
Suala la kuoa halitakiwi kukurupuka wala kushinikizwa na mtu yeyote. Tuliza akili zako na umshirikishe Mwenyezi Mungu atakubariki utapata mke mwema na utafurahia maisha ya ndoa. Hatua madhubuti na uamzi sahihi unatakiwa kuyachukua sasa. Utakavyoendelea kuishinae kishingo upande, utazeeka kwa matatizo yasiyo na tija wakati umri wako bado ni mdogo kubeba "mizigo".
 
Hujasimulia hata mimba kuharibika achilia mbali kulea!!!?
Au ume skip somewhere
 
Kuishi na mwanamke kunahitaji u-loffa na unafiki kwa pamoja. Don't take it serious Bro. Jifanye mpuuzi ili mambo yaendelee. Komaa umalize shule. Uongeze kipato kelele zitaisha.
NB: Wakati wa mechi achana na kuchat kwenye magroup whatsapp,PIGA KAZI TU mpaka afike kileleni.
 
Ngoja na mie niweke udhoefu wangu.
Tabia ya sasa ya mkeo ni matokeo na kama sio matokeo basi ndivyo alivyo na hafai kua mke. Chanzo cha tabia hizo ni zile siku 90 za mwanzo tangu muanze kuishi wote, katika siku hizi mkeo alianza tabia kama hizi kwa kukujaribu kuona wewe uta react vipi lakini wewe ulikua unachukulia poa na sasa yamekomaa.

Fanya hivi, hakikisha unakua mwanaume kwa mke wako. Fanya na amua mambo kiume. Usiwe muongeaji sana au mlalamishi, ukiona amekukosea na yeye anajua kua hili alilofanya ni kosa wewe kaa kimya na onyesha kuchukia, hapa usimlalamikie wala kumfokea.
 
Mkuu pole sana.....Allah alikuonesha mapema kuwa hakufai ww ukampa nafasi ya kujirekebisha ...Hapo ndipo ulipoanziasha janga kubwa moyoni kwako.Kuna kauli moja inasema KAMA MWANAFUNZI WA FIELD ANAONESHA UTOVU WA NIDHAM HAPASWI KUMPA NAFASI YA KUMUAJIRI.maana akiajiliwa atakuwa mtumishi mbaya ktk tasisi yako....Kaka ww umemuajiri mtu ambaye hafai kuwa mtumishi ktk ofisi yako....Imani yako ingefanaa na mimi ningekushauri ongeza mke wa pili au muache uowe mwingine.....Pole sana kwa kumaliza mwaka 2016 kwa tabu na kuanza mwaka 2017 kwa majonzi....
 
Fanya haraka mrudishe kwao alafu ndo uwape hayo maelezo. Kwa vile unapenda akijirekebisha mrudishe. Otherwise muache kwao ili atie akili.
 
kwa mujibu wa maelezo yako, umri wa ndoa yenu umefikia mahala ambapo huwa ni hatari zaidi.
Vumilia mshauliane mtafika tu maana ujue ndoa ndoano! i atka moyo, hata ukimwacha unaweza kuoa mwenye matatizo zaidi ya hayo.

(Gori kipa kaacha namba 3)
 
Uyo ana wivu sana n dawa yake mtom...... Kwa fujo n ni kila siku baada ya apo nipe majibu kwa pm
 
Twanga kihuni huni yaani kisela. Ikibidi hata nipe contacts zake tusaidiane atatulizwa tu. Tupo pamoja kaka undugu ni kufanana.
 
Ni mapito ya ndoa, akikua ataacha.. hata usiumize kichwa au kama vp omba uamisho wa kazi hata mwaka mmoja atakumisi tu.
 
b9e3f9b2f17e398dc7cd1ee6dccbd9d4.jpg
tuangalie ninini wanachokisema wazee wetu kuhusu haya maisha.pole sana bro binafsi hapa siwezi kutia neno watakushauri wenzangu.
 
Back
Top Bottom