Ndoa imeingia doa. Msaada wa mawazo unahitajika sana

Pole sana mkuu linavyokukuta jambo ni bora kusema ni wewe ili upate msaada vizuri usimsingizie kaka yako
 
Habarini!

Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga. Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.

Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.

Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yakepia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.

Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda. Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake.

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake.

Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.

Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.

Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa. Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!
Ushauri ni mdogo tu kitanda hakizai haramu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Asimwache!Bali amwambie awe huru akijisikia kuolewa aolewe au kua na mchepuko awe nae pia!!Lakini Jamaa aoe Mwanamke mwingine halafu huyu abaki tu kama mlezi wa watoto!!!yeye atoe huduma kwa watoto wake!!!
 
Haya haya wale wote wanaosema wakioa mwanamke bikra wala hawatachapiwa nyoosha mikono juudaa hii dunia ina mambo
 
Kuvunja ndoa sio suluhu
Kosa sio la mtoto

Asimnyanyase mtoto

Mke asimamie msamaha alioomba..ila nina shaka mke atarudiana na huyo mzazi mwenzie
Hii ndo huwa inafikirisha! Jamaa anaweza msamehe mkewe lakin mke mwenyewe asiache kabisa kuwa na jamaa
 
Hili nalo neno
Ndo maan lazma asitishe unyumba,kulala chumba kimoja na chakula km akil ale alichopakuliwa mtoto
Vya kutengewa sumu nje njeee

Ila kwa ajili ya watoto sio kosa lao
Aendelee kuwepo kwny huo mji
Mahitaji ya kiutu uzima atafte mchepuko ampime wakielewana amuoe

Nasisitiza asitoe talaka
Ili Wasigawane mali lakini
Ila haya mambo ya kugawana mali na mtu aliyenisaliti jaman syo fair kabisa!!
 
Habarini!

Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga. Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.

Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.

Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yakepia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.

Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda. Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake.

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake.

Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.

Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.

Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa. Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!
Hakuna dharau kubwa kwa mwanaume kama hiyo.

Ni Mwanaume ZOBA pekee ndiye anayeweza kusamehe huu Usaliti.

Hata kama tungekuwa na watoto 50 na mali nyingi.....
Hizo mali zote ningemwachia huyo mwanamke ili mimi niwe SALAMA.

Kama atakubali kuendelea kuishi naye MWAMBIE AANDAE JENEZA LAKE MAPEMA.
 
Hiv vitu havijaanza kwa kizaz hiki tu yalikuwepo toka zaman ndio maana walianzisha kamsemo kao "kitanda hakizai haramu" pia atambue yeye sio wa kwanza kulea watoto/mtoto ambaye sio wake. Hapo ndipo ulipo ukomavu wa akili na tatzo halitatuliwi kwa kukimbiwa.
Alinde ndoa yake apambane kuilinda familia yake ndio kitu pekee cha thamani alicho nacho ubinafsi usimfanye aipoteze.
Unalindaje familia ambayo kuna watoto zao la usaliti! Ujasiri wa kuvukilia haya unatoka wapi?
 
Unalindaje familia ambayo kuna watoto zao la usaliti! Ujasiri wa kuvukilia haya unatoka wapi?
Oa mke wapili (ila asihishi hapo) huyo abaki kama mzazi mwenzako tu humo ndani ila huduma zote za familia hakikisha unatoa ikiwepo na mda wa kukaa nayo
 
Mungu ampe hekima. Na iwe fundisho pia kwa wababa anavyoumia yeye ndivyo wanawake wanaoletewa wtt kti nje ya ndoa wanavyoumia. But mwisho wa siku wanawake wanawalea hao wtt so na yy alee. Ila ki ukweli mwanamke mwenzangu hajafanya poa hata kidogo unachepuka mpk kuzaa huko eti tukumbushie ibaki kumbukumbu ya mapenzi yetu ya tangu utotoni. Ujinga ujinga tuu.
 
Maabara gani hiyo TZ ambayo inatoa majibu ya mtoto sio wako?..nilisikia wanatoa majibu ya mtoto ni wako hata kama majibu ya kipimo yanaonyesha sio pale ambapo wanaona mume ataenda kutengana na mama na mtoto ataishia kuishi kwa mateso.
 
Back
Top Bottom