Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Sababu mojawapo ni kumkosoa mwenza mbele za watu. Mkisha funga ndoa nyinyi ni mwili mmoja. Mume wako akichemka hadharani unaimeza aibu mpaka mfike chumbani ndiyo mnaongea. Mfano unajua mume wako Kimalkia hakipandi, akivunja mbele za watu meza.
Kumkumbatia mume wako asubuhi akiwa anakuaga ni muhimu. Kwa mila za Afrika ni ngumu kufanya haya kama mpo na wazazi au wakwe. Mkumbatie chumbani na busu hata akirudi kutoka kazini.
Jiepushe na marafiki wasio mkubali mke/mume wako. Maneno yao yatakua sumu katika penzi lenu.
Jifunze kuomba msamaha kwa mke/mume wako. Kiburi ni sumu ya mapenzi.
Kuwa muwazi kwa mwenza wako. Mfano Haya mambo ya kuja kufahamu ulizaa kabla ya ndoa mkiwa tayari kwenye ndoa yana leta hatari sana.
Wengine neno niache au tuachane limekaa mdomoni kila mkikwaruzana kidogo tu.
Kila ukipata nafasi weka manjonjo kwenye ndoa yenu. Hata kutumia weekend hotelini kubadilisha mazingira na kuwa na nafasi yenu.