Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,782
Kauli za navumilia kwa sababu ya wanangu na nyingine kama hizi zimeua nafsi na mili ya wanawake wengi.. Infact wanawake ni wahanga wa ndoa kuliko wanaume
Kulinda heshima: Ni utamaduni wa kurithi na mazoea ya kijamii kwamba mwanamke akiwa kwenye ndoa anaheshimika zaidi kuliko ambaye hana ndoa
Kutojiamini.: Wengi hudhani hawawezi kusimama wenyewe bila mwenza rasmi.. Kile kitendo cha kuwa na mwanaume ndani ya nyumba hata kama ni jinga fulani lisilojitambua kwake inatosha kabisa
Kuonesha uwezo wa kumiliki: Wengi huingia kwenye mtego wa kuolewa na watu wa ajabu kisa tu ana sifa fulani ambazo anaweza kutambia wengine kuwa naye anamiliki mwanaume mwenye sifa Fulani
Wengi hawafunguki lakini mioyoni wamejawa na maumivu makali mno.. Wameolewa, wamezalishwa.. Lakini mwanaume hana mbele hana nyuma yupo yupo
Hahudumii familia chakula, nguo na mahitaji mengine muhimu
Halipi ada za shule wala chochote
Pesa yake ni yake
Akiishiwa atamuomba mkewe na ole wake mke amnyime
Wengi ni watu wa kuchelewa kurudi nyumbani kwa visingizio mbalimbali.. Na wakirudi wanataka wakute chakula kizuri nk
Wengine wanajifanya hawana kazi na kazi ni ngumu kupatikana lakini kumbe ni wachagua kazi sana..
Mama anatoka asubuhi kwenda kazini baba ndio kwanza anavuta shuka.. Kisha akiamka anataka akute chai nzuri na hata kiporo cha wali ndondo ama chapati za kusukuma na nauli ya kuendea kwenye mishe
Hawezi hata kutandika kitanda wala walau kufua boxer zake.. Na kama ndani ya nyumba kuna beki tatu ama ndugu wa kike hao ni asusa yake. Ukatili mkubwa sana huu
Huko kwenye mishe akipata anatumia na michepuko na marafiki wasio na faida na sometimes akiishiwa atampigia mkewe amtumie
Wanawake wengi wanaishi kwenye hili gereza .. Wamegeuzwa chuma ulete na watumwa wa kuwatumikia wanaume wasiojitambua na wanaishi na haya maumivu kisa kulinda ndoa
Ndani ya nyumba hakuna kujadiliana kitu ni mwendo wa amri, hakuna upendo hakuna ucheshi, akimhitaji chakula cha ndoa atampanda kama mbwa na akimaliza atamuacha hapo bila kujali hisia za mwenzake!
Simu ya baba ni ya baba ole wake mama aiguse ataporomoshewa zigo la kashfa na matusi.. Lakini simu ya mama ni halali baba kuishika na kuipekua hata kupokea na kusoma msg zisizomhusu
Siku baba katoa 50 kampa mama... Hiyo ndio itakuwa wimbo wa masimango kila mama atapoongelea upungufu wa mahitaji nyumbani.... Lakini bado wanagumumia haya machungu wakitumaini waume zao watabadilika na kutambua hisia zao na majukumu yao..!
Wanawake wengi wameamua kuchepuka kutafuta unafuu wa kihisia
Wengine kwa ajili ya kipato
Wengine wameamua kuingia kwenye ulevi kutafuta nafuu ya usongo wa mawazo
Wengine hawana hisia za mapenzi tena na hawajirhamini tena
Wengine wameingia kwenye kundi la kujichukia na kujenga chuki mbaya kwa wenza wao..!
Ndoa jambo jema lililotarajiwa kuleta heshima, upendo, masikilizano, furaha maendeleo nk imegeuka kuwa jehanum ya mateso makubwa na gereza la utumwa mbaya kabisa..!
NDOA ! NDOANO.. RIP MAUNDA..! (Haihusiani na hii mada)