Walikubaliana kuaona wakiwa hawana watoto kumbe mwanaume alikuwa na mtoto bila kujua, ndoa ikavunjika!

Crala kidoti

Member
May 18, 2023
48
140
Habari jf ni Crala Kidoti tena. Hii issue ilimtokea mdogo wangu mwaka 2019 upande wa baba mkubwa wangu.

Dogo alikuwa na mchumba wa kike aliyedumu nae kwa miaka miwili kwenye uchumba. Hatimaye wakafunga ndoa mwaka 2019 mwenzi wa 3, na mkewe alimpata na kuwa mchumba wake baada ya kuachana na mkaka mmoja hivi.

Na sababu ya kuachana na jamaa yule alikuwa na mtoto tayari aliyempata kabla ya kukutane nae. Yule binti alimchana tuu kwamba yeye hawezi olewa na mwanaume ambaye anamtoto tayari, anapenda kuwa na mwanaume ambaye anatengeneza watoto wao wenyewe.

Bond ikavunjika na mdogo wangu akaanza mahusiano na huyo dada, na walikubaliana kabisa mimi na wewe hatuna mtoto. Walienda hivyo mpaka kufunga ndoa ya kanisani. So, sababu moja wapo ya ndoa kufunga ni sote hatuna watoto.

Sasa ililofika mwezi wa 7 dada wa mdogo wangu huyo ambaye wamezaliwa tumbo moja alitembelea maeneo ambayo dogo alisoma chuo kule Mwanza ambapo alienda kikazi, katika kuzunguka zunguka akakutana na mdada mmoja ana mtoto kafanana sana na mdogo wake ambaye amefunga ndoa mwezi wa 3, na akiangalia yale maeneo mdogo wake ndipo alipokuwa anaishi na ni karibu na chuo.

Sasa dada mtu baada ya mshituko akaamua kwenda kwa dada mwenye mtoto ilikupata data, akamuuliza huyu mtoto baba yake yupo wapi, dada yule akamjibu kuwa kuwa alikuwa anasoma chuoni hapa. Alinipa mimba kipindi amemaliza chuo hapa sikukutanane tena baada ya kuondoka.

Dada akaamini ni mdogo wake kwa sababu kafanana naye kabisa. Akamwambia unaweza kunitajia jina akamtajia jina la mwanzo, likawa jina hilohilo, dada akachukua simu na kumuonyesha picha ya kaka yake, dada mwenye mtoto akasema ndio huyo huyo.

Dada mtu bila kuchelewa akapiga simu home na kuwaeleza kila kitu. Baada ya siku kumaliza kazi yake akaenda kwao na kuwaambia kila kitu na mama akaamua kuwasiliana na dada yule na kuongea naye. Walionyesha picha na dogo kweli walifanana hivyo hivyo.

Sasa familia wakaamua kumwambia dogo kuwa unajua mtoto sehemu fulani, dogo akasema yeye hana mtoto kabisa. Dada mtu akaamua kumwambia kila kitu, dogo alipata mshangao sana. Maana anaelewa makubaliano na mkewe.

Dada za jamaa wakawa wanang'ang'ania mtoto aje home ili wamjue vizuri mtoto. Baba mtu akasema mambo haya tufanye kwa utaratibu msikurupuke, maana kijana mdogo wenu ameshaoa ana mke, mama na dada zake walimpenda mtoto yule wakawa wanataka aje home. Huku kaka yao anazuia, mwishowe walimtumia nauli dada yule aje home.

Sasa kaka yao katika kuangaika kuangaika mkewe wake akajua kuna kitu hapa, kwani alimuuliza mbona kama hauko sawa shida ni nini, anakwepa kumwambia simu zilikuwa nyingi sana anapigiwa na dada zake aje home sababu dogo kashafika na unaweza usimwambie mkeo tutatafuta nmana ya kumwambia mkeo usijali.

Baada ya simu kuwa nyingi na maongezi mkewe si akasikia bwana mazungumzo. Case ikawa kubwa sana.

Kwa kifupi mkewe aliamini familia ilishirikiana kumficha yeye kuhusu kaka yao kuwa na mtoto. Kuanzia siku ile ndoa ilikosa amani kabisa, yule dada alikuwa analia kama kafiwa na mume vile tena mume aliyemtegemea. Dah, niliona huruma sana nikikumbuka.

Baba yao akasema niliwaambia case kama hizi inahitaji kuwa na hekima kuzisuluhisha. Dada zake kama mawifi si unajua, wakaanza kusema huyu ni damu yetu hatuwezi itupa. Sasa kuweka sawa ile kesi wazazi wa dogo wakamwambia kuwa wewe endelea na ndoa yenu mtoto hatakuja kuishi kwenye nyumba yenu.

Ila yule dada still aliamini kuwa familia ilimficha kuhusu ilo na aliwaambia hana imani tena na familia yenu na hata kwa mume wake, Walijaribu kumshawishi hata kutumia wazazi wake na viongozi wa dini na walimwambia kuwa unandoa ya kanisani, Lakini still alikataa katakata, yule dada alikuwa analia mpaka huruma.

Wazazi wake walimshauri basi aendela na ndoa yenu tu, haina shida, mtoto hana shida yoyote ila dada alisema hawezi ishi na mtu ambaye kampa maumivu makali kwenye maisha yake na dada yule kutokana na maumivu na vilio mimba ilitoka ilikuwa na 2 month hivi, kutokana na situation ile.

Mwishowe dogo aligombana sana dada yake akiona kama kamuharibia ndoa yake, tena ngumi kama ngumi na maneno, mpaka leo hawapatani na dada yake. Dada mtu alijaribu kuomba msamaha ila wala.
Kwa kifupi ndoa ilivunjika.

Kama ungekuwa wewe mtu mzima case kama hii unasuluhisha vipi?

Karibuni jamani.
 
Kifupi binti yuko sahihi kwasabubu hayo ni makubaliano yao kabla hta ya ndoa na ikumbukwe aliacha mahusiano yake ya mwanzo kwasababu hyo ya mwenzie yule kuwa na mtt na busara kutumika kw binti sio sheria ila ni uamuzi wake kuamua kukubaliana na hyo hali au laa kifupi yuko sahihi ila upande wa pili wa familia ya jamaa wangekuwa tu wavumilivu angalau wangesubir hta Bibie ajifungue kwnza pengine ingesaidia
 
The young wife is okay . Yupo sawa . You can’t just bring the kid to the family . We all agree it’s nil -nil
 
Watoto wadogo wa chekechea ndo wataamini hii story!!
Tena chekechea za zamani. Siku hizi wana akili na hawawezi kuamini. Uvamie tu mtu njiani eti huyu mtoto kafanana na fulani na uamue kufuatilia! Tena mtoto mdogo! Umri ambao unaweza kuhisi ni mtu anapokuwa mtu mzima. Kwenye age ya utoto siyo rahisi uone mtoto ambae hata humjui eti anafanana na ndugu yako na uchukuwe uamuzi wa kupeleleza!
 
Kiufupi huyo Dada yake Hana akili Wala busara anaendeshwa na hisia badala ya kufikiria matokeo ya atakachokifanya.

Kulikuwa na haja gani ya kukimbilia kutoa hizo taarifa mapema ilhali anajua mke wa mdogo wake ana MIMBA.

Na kulikuwa na umuhimu gani wa kutoa taarifa kuhusu mambo yasiyomhusu pasipo kuwa tayari kujua namna ya kulitatua tatizo.
 
Kila mtu ana uamuzi wake. Walikua na makubaliano yao wenyewe. Lakini kuna muda katika haya maisha makubaliano huwa yanavunjwa au yanakuwa modified. Na kwa imani yangu, rehema ina umuhimu mkubwa sana kwenye ndoa. Ndoa bila rehema ni ngumu sana.

Kuna muda mume/mke wako anaweza fanya kitu, na kwa akili za kawaida hutaweza kubeba. Lakini Kristo akijaa kwa wingi ndani yako, akaachilia neno likuumbe upya, kuna vitu utaweza kuvibeba hutaamini. Wengi wetu baba/mama zetu washapiga matukio tukiwa tunakuwa, lakini still, they chose to press on. Its never a bed of roses anyways.

Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, roho yako yote, nguvu zako zote na Akili zako zote. Hii itatusaidia sana katika trials mbalimbali. Pia tujifunze kutafuta hekima kwa wazee wa vijijini. Kuna shauri hautazipata kwenye mitandao ila wanazo. Very sad outcome.
 
In short kama ni hadith ya kweli, jamaa aachane na huyo mwanamke atafute watoto mpaka idadi anayopenda aachane na mambo ya kuoa au ataoa mwingine halafu mwambie dada arudi sokoni asubiri mteja mwingine wa ndoa.
 
Tena chekechea za zamani. Siku hizi wana akili na hawawezi kuamini. Uvamie tu mtu njiani eti huyu mtoto kafanana na fulani na uamue kufuatilia! Tena mtoto mdogo! Umri ambao unaweza kuhisi ni mtu anapokuwa mtu mzima. Kwenye age ya utoto siyo rahisi uone mtoto ambae hata humjui eti anafanana na ndugu yako na uchukuwe uamuzi wa kupeleleza!
Jf siku hizi utoto mwingi!!
 
Back
Top Bottom