Ndizi Tiba ya Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndizi Tiba ya Ukimwi

Discussion in 'JF Doctor' started by Iga, Mar 22, 2010.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WANASAYANSI wamegundua protini maalum iliyomo kwenye ndizi ambayo inazuia wanawake wasiambukizwe ukimwi wakati wa tendo la ngono.

  Wanasayansi hao toka Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani wanaamini kwamba ugunduzi huo utasaidia kutengenezwa na kuuzwa dawa za bei nafuu zitakazozuia kuenea kwa ukimwi duniani.

  Protini iliyomo katika ndizi huitwa kwa jina la Kitaalamu lectins na kiasili huwemo katika ndizi wakati inapoanza na kuendelea kukua tayari kukomaa na kutumika na walaji. Kemikali zilizomo katika protini hiyo inasemekana husaidia kuzuia mgonjwa kukumbwa na maradhi mengi kufuatia kuambukizwa ukimwi.

  Katika maabara protini hiyo iliyosilimishwa kwa jina la BanLec imekutwa ina nguvu sawasawa na dawa mbili zilizopo madukani leo dhidi ya ukimwi.

  Kufuatia kuchapishwa kwa matokeo ya utafiti huu katika jarida la 'Journal of Biological Chemistry,' BanLec ina uwezekano mkubwa wa kuwa kinga nafuu na salama zaidi kutumika katika sehemu nyeti za wanawake ili kujikinga na ukimwi.

  Ingawa kondomu zinasaidia sana kuzuia ukimwi lakini wanasayansi hao wanasema huwa zinafaa zaidi katika kuzuia maambukizi pale tu zinapotumika bila kuacha na zikatumika kwa namna inayotakikana kitu ambacho sio rahisi kufanywa na wanawake katika nchi zinazoendelea maana hawana sauti sana wakati wa tendo la ngono kama wenzao wa nchi zilizoendelea.

  David Marvovitz kiongozi na mwandishi wa taarifa ya utafiti huu anasema kwamba dawa itakayotokana na ndizi itakuwa ni ya muda mrefu na inayotumiwa na mwanamke mwenyewe toauti na ilivyo kondomu ambayo budi ivaliwe na mwanamme pale anapotaka.

  Utafiti huo unaelezea kwa kirefu jinsi ambavyo protini ya lectin ilivyo na uwezo wa kushinda VVU. Lectin ni protini inayobeba sukari na ina uwezo wa kugundua wavamizi katika mwili kama vile virusi na kuambatanisha na pathogen.

  Watafiti hao wamegundua kwamba BenLec, lectin iliyomo kwenye ndizi inazuia maambukizi ya VVU kwa kuambatana na sukari iliyojaa katika bahasha ya protini ya gp120 kwenye HIV-1 na hivyo kuizuia kuingia kwenye mwili.

  Tiba itakayotumia ndizi wanadai wanasayansi hao itakuwa ni ya gharama za chini zaidi kulinganisha na tiba za kupunguza makali ya ukimwi za sasa ambazo hutumia malighafi ambayo si asili. Isitoshe tiba hiyo mpya inaweza kuja na mambo mengine ya ziada kuliko hii ya sasa, wanasema watafiti hao.

  'Tatizo la baadhi ya madawa ya ukimwi ya sasa ni kuwa virusi vya ukimwi vinaweza kujizalisha vyenyewe na ksuambaa mwilini zaidi kisha kuwa virusi sugu kutibika,' ansema Michael Swanson mmojawapo wa watafiti hao, ' lakini mbele ya lectin vidudu hivyo haviwezi kufurukuta na husalimu amri na hivyo muathirika kuwa salama kwa muda mrefu na pengine kupona kabisa kama atafuata masharti ya madaktari wake.' {Source: Afrol News }
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mmmh, kaaazi kweli kweli.
  lakini maeneo wanayokula ndizi sana hasa mikoa ya Mbeya na Kagera plus nnchi ya Uganda ni maeneo wanayokula ndizi sana...lakini maambukizi ya UKIMwI ni nooma.
  acha nirudia tena kusoma maelezo ya hiki kinachoitwa utafiti.
   
 3. a

  akili Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli nimesikia haya kwenye sauti ya BBC Jumamosi iliyopita..Sisi walima ndizi basi tuangalie jinsi ya kutengeneza misosi mbalimbali ambayo itakuwa ni kama vile lishe bora dhidi ya maambukizi ya ukimwi! !!!
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nguvumali nafikiri kama nimesoma vizuri ni kuwa hiyo protein inayopatikana kwenye ndizi itakuwa enhanced na sukari ndo inafanya iwe tiba!!

  Otherwise tuwaachie wataalam wakamilishe final product ili tuone ......tatizo (kwa wagonjwa) la tafiti za kisayansi ni muda wanaochukua baada ya kupata preliminary results kama hizi mpaka watakapojiridhisha na kutupa product sokoni...si chini ya miaka 12 ijayo!! By then, tayari kusini mwa jangwa la sahara tutakuwa tumepoteza nguvu kazi kubwa sana!!
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hebu wana Food Science and Nutrition nifahamisheni kama ndizi ni protein!!!?? Kuna aina ngapi za makundi ya vyakula (protein, vitamins, carbohydrates, fats and oil or lipids) zilizopo katika ndizi mbichi na mbivu??? Du nimechoka!!
   
 6. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkuu mie siyo food scientist ila nilivyoelewa si kuwa ndizi yote imejengwa na protein hapana ila kama sikosei amino acid ambayo itakuwa extracted na kuwa enhanced ndo hapo itafanya hiyo kazi ila si ndizi kama ndizi.General concept hapa ni kama vile transgenic organisms just a small thing which is extracted and modified.Usitegemee kupika na kula ndizi ndo itakuwa kinga utakuwa unajidanganya.
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hapa tuwaache wataalamu wamalize kazi yao kabla atujaumizana vichwa hapa
   
Loading...