Ndizi dawa ya Ukimwi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndizi dawa ya Ukimwi!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Kimey, Mar 18, 2010.

 1. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  VIPIMO vya kimaabara vya wanasayansi nchini Marekani vimebaini kuwa ndizi zina virutubisho maalumu viitwavyo BanLec ambavyo viko sawa na aina mbili za dawa zinazotumika katika kuzuia kuenea kwa virusi vya ukimwi.

  Wanasayansi hao wamesema wanaamini virutubisho hivyo vya BanLec ni muhimu na vinaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

  Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo ambayo yameripotiwa katika jarida la Biological Chemistry la Michigan, virutubisho hivyo vinatokana na kemikali ambayo inazalishwa kiasili katika mimea ijulikanayo kama ‘lectin’ ambayo inapambana na magonjwa yanayoikumba mimea.

  Watafiti hao wamegundua kuwa lectin iliyo ndani ya ndizi inaweza kukabiliana na madhara ya HIV kwa kuzuia virusi kuingia katika mwili wa binadamu.

  BanLec hutumika kama bahasha maalumu ya kuhifadhia protini ambayo hudhibiti kubadilika kwa vinasaba vya vijidudu vya HIV.
  Msimamizi mkuu wa jarida la kisayansi kutoka Chuo Kikuu cha Michigan, Michael Swanson alisema: “Tatizo la baadhi ya dawa za kudhibiti HIV ni kuwa zinaweza kuzidiwa nguvu, lakini inakuwa vigumu zaidi zinapokuwa na lectin.
  “Lectin hujiunga na sukari inayopatikana katika nukta tofauti za bahasha za HIV-1, na inadhaniwa kuwa inaweza kuwa na nguvu zaidi ya kuzuia virusi kuikaribia.”
  Source: Mwananchi
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,690
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  zisije tu zikapanda bei
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii thread si imerudiwa? Jumatatu wiki hili sikumbuki, lakini niliichangia hii!
   
 4. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,556
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ni kweli au kuadimika kabisa.
   
 5. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ha ha ha kweli kabsaa!!
  nimecheck kuanzia tarehe tano March kweye hii Jukwaa sikuona ndo maana nikapost hii! may be iliwekwa jukwaa lingine!!
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,554
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  Ajabu hapa Tanzania sehemu ambazo ndizi ndio chakula kikuu ndiko Ukimwi unaongoza,nenda mkoa wa Mbeya na Kagera,huko ndizi ndio menu kubwa lakini gonjwa kwa saaana,hizi tafiti zingine bana ni uchuro mtupu
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,586
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nashangaa, labda watuelimishe namna ya kuzitumia. pengine inatakiwa ziliwe zikiwa mbichi.
   
 8. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Labda kwa ngozi nyeusi ni Vise-versa!!
   
 9. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kutokana na utafiti huu kinachozuiwa ni HIV-1, Afrika na hasa Tanzania kuna HIV-1 na HIV-2 na anayeshambulia sana na kumaliza wengi ni HIV-2. Huenda huko Mbeya na Kagera kuna HIV-2 ambaye hazuiliki kwa ndizi
   
 10. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hawa watafiti wasipokua makini kututangazia majaribio yao katika vyakula, watazidisha maambukizi mapya kwani watu watadhani kula ndizi ndio umemaliza ukimwi kumbe unamaliza watu.
  Siku zijazo watatwambia mchele, mahindi, ulezi yaani vyakula vinavyoliwa na wengi ndio dawa kumbe siyo dawa. Hatari sana!!!! tafiti hizi.
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,586
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Sishangai matunda mengine wanaiogopa ndizi.
   

  Attached Files:

 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  ndizi mbivu sio ndizi mbichi au ndizi mbichi zilizopikwa.
  sio Plantin, ni banana
   
 14. m

  muhanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  na mie nashanga sana, ingekuwa ni kweli basi huko kagera na mbeya wasingeyumbishwa na virus, au ni mpaka zifanyiwe 'modification' kabla ya kuwa kinga/dawa ya ukimwi???
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Dose yake ikoje ..??
   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Kula ndizi mbivu kumi kila baada ya ngono zembe moja.
   
 17. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,270
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona kilimanjaro na kagera ndiko kunapoongoza kwa maambukizi?
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Hii Adhabu unaweza kumaliza ndizi kumi Bigirita ?
   
 19. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,556
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dah!!! hii kali.
   
 20. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,715
  Trophy Points: 280
  au atufafanulie ni ndizi kisukari, mzuzu, mshale, matoke au zipi
   
Loading...