Ndiyo maana elimu yetu haina uwezo wa kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kujiajiri

FineForever

JF-Expert Member
Apr 12, 2017
1,777
2,353
502b63fdc19c3365c4ff641cf3d26dd5.jpg
Huu unaitwa ubunifu. Leo hii ukienda secondary ukamwambia mwl. akuletee mwanafunzi mwenye akili zaidi darasani, atakuletea yule ambae hupata "A" ya Mathematics, Physics au Chemistry.

Kamwe hatakuletea yule ambae anaweza kuchora, kuimba, kuchonga au kucheza mpira vizuri.

Elimu yetu itabaki kuwa ya kukaririshwa tu na kamwe haitamwezesha mhitimu kukabiliana na changamoto za maisha ktk mazingira yanayotuzunguka.

Ndiyo maana Leo hii kila mhitimu anafikiria zaidi kuajiriwa kuliko kujiajiri, hii ni kutokana na Mfumo wa Elimu Yetu Jinsi ulivyo.

Nawasilisha!
 
Kuna kaukweli kias,
Jwani viongozi na serikali za kiafrica wanaamini kwenye vyeti , na kusahau informal education ambayo unzalisha watu wabunifu , wenye vipaji mbalimbaki nje ya formal education
Mf kuna mafundi wengi wa ujenzi , magari, n.k ambao wanauwezo mkubwa kuzifi baadhi ya wasomi wa kada husika ambao wanajua theory lakini vitendo ni zero
 
Kila mtu ana akili. Hakuna asiye na akili hata kidogo. Kila mtu ana uwezo wa aina ya kwake. Muhimu ni kwamba mfumo wa elimu uzingatie uwezo na upendeleo wa mtu kujiendeleza kielimu.
 
Ungeanza na maneno nimecopy nakupaste kutoka kwa nikki wa pili...
Yeah Mkuu. Ndio maana kwenye Heading nimeonesha kuwa ni tetesi, ingawa pia kumbe mwishoni ningeandika cc/appreciation/source. Noted with thanks Mkuu.
 
502b63fdc19c3365c4ff641cf3d26dd5.jpg
Huu unaitwa ubunifu. Leo hii ukienda secondary ukamwambia mwl. akuletee mwanafunzi mwenye akili zaidi darasani, atakuletea yule ambae hupata "A" ya Mathematics, Physics au Chemistry.

Kamwe hatakuletea yule ambae anaweza kuchora, kuimba, kuchonga au kucheza mpira vizuri.

Elimu yetu itabaki kuwa ya kukaririshwa tu na kamwe haitamwezesha mhitimu kukabiliana na changamoto za maisha ktk mazingira yanayotuzunguka.

Ndiyo maana Leo hii kila mhitimu anafikiria zaidi kuajiriwa kuliko kujiajiri, hii ni kutokana na Mfumo wa Elimu Yetu Jinsi ulivyo.

Nawasilisha!
Ni kweli kabisa tunafundishwa kukariri zaidi ya utendaji
 
Kuna wakati kulaumu hakusaidii nadhani unge kuja mkakati namna ya kujiajri sasa unapo kuja na Uzi kama huu na hujatupa njia ya kulitatua tatizo ni kuendelea kututumaza tunao soma uzi huu
 
LA hasha! Hii inamana kubwa muno kwako, kwangu na yule. Kwanini? Kwa sababu, Uzi huu unatupatia mwanga (exposure) kwamba kwa kuwa mfumo wa elimu yetu unatuaminisha kwamba baada ya kuhitimu tutegemee kuajiriwa kuliko kujiajiri, sasa ni wakati wa mimi, wewe na yule kujitathimini na kutambua ni kitu gani cha ziada tulichonacho, tunachoweza kufanya nje ya kile tulichokaririshwa darasani ili tuweze kuvipa vipaumbele zaidi na kuviendeleza kwa vitendo.

Lakini cha kushangaza, mtu anamaliza la 7, fomu 4, fomu 6 au chuo lakini hawezi kutumia maarifa aliyoyapata kutumia fursa zilizopo kufanya mambo mbalimbali kama vile kulima bustani au kufungua biashara yoyote, badala yake anabaki kukaa vijiweni au kutembea huku na kule akisaka ajira bila mafanikio.
 
Mkuu asante kwa ufafanuzi mzuri hapa ndo umefafanua maana kwenye Uzi kuna mafumbo mengi sana

Sasa mkuu tusaidiane kujulishana fursa ambazo kama vijana na jamii ya watanzania inaweza kutusaidia katika maisha
 
Jaman system ya kuham Chuo kimoja kwenda kingne hukoje
Chuo Kikuu au hivi vya kati? Kama ni Chuo Kikuu, nafikiri TCU na Chuo unachohamia wanahusika moja kwa moja. Sina taarifa kamili kuhusu hiyo, ila kwa uchache is like hivo yaani.
 
Back
Top Bottom