Ndiyo, Lowassa ni fisadi na hilo halina ubishi lakini ndani ya CCM yupi ni afadhali Urais 2015!

Kwamba CCM wote na mafisadi siyo kweli .hiyo ni lugha ya kuwasaidia kupata usingizi mnaoukukosa miaka yote mitano.fanyeni utafiti wa kutosha mtawajua wana CCM a
ambao si mafisadi na ambao wanafaa kuwa rais ingawa ninyi hamuwapendi.
 
Mzee Mwanakijiji, Dr. Shein ndio chaguo la JK, japo hata akisimamishwa yeye, bado tutapata mabadiliko ya kweli, tatizo vita vya udini vitakuwa vibaya kuliko vile vya 2010. Wakristu wa bara, hawatamchagua rais Muislamu for another term, hivyo mgombea Mkristo wa upinzani, atajipatia easy ride!. Sipendi tupate rais aliyepigiwa chapuo na kanisa! Tuendelee kupiga chapuo la Edward Lowassa tuu!, au hamtaki mabadiliko?.

Unavoandika kwa uhakika!Utafikiri ni great foreseer mithili ya the late wa magomeni!Amekurithisha nini?
 
Mzee Mwanakijiji, Dr. Shein ndio chaguo la JK, japo hata akisimamishwa yeye, bado tutapata mabadiliko ya kweli, tatizo vita vya udini vitakuwa vibaya kuliko vile vya 2010. Wakristu wa bara, hawatamchagua rais Muislamu for another term, hivyo mgombea Mkristo wa upinzani, atajipatia easy ride!. Sipendi tupate rais aliyepigiwa chapuo na kanisa! Tuendelee kupiga chapuo la Edward Lowassa tuu!, au hamtaki mabadiliko?.
Mkuu samahani sana...
Usiyoyapenda ndiyo yanafanyika, wewe unafikiri Lowassa anapendekezwa kwa sababu gani?..wenzako wengi wameisha jua sasa kama wewe unapendekeza tu bila kujua sababu basi ndio hivyo!... Nipe sifa za Lowassa hasa kustahili kura yako nitakusikiliza kinyume cha hapo wewe pia ni mpiga chapuo lile usolipenda..
 
Kama sii UFISADI nadhani wapo watu wengi wanaweza kuwa viongozi bora CCM...Tatizo unapokiuka msingi mkubwa wa uongozi bora ni vigumu kusema nani ana afadhali maana huna kipimo tena zaidi ya sura na longolongo...Kiongozi bora lazima awe visionary, sioni Lowassa akiwa na sifa hiyo hata chembe zaidi ya imani za Umimi, ...........!

Mkuu Bob...heshima mbele......Asante sana kwa maneno hayo hapo juu
 
Hivyo mgombea Mkristo wa upinzani, atajipatia easy ride!. Sipendi tupate rais aliyepigiwa chapuo na kanisa! Tuendelee kupiga chapuo la Edward Lowassa tuu!, au hamtaki mabadiliko?.[/QUOTE]

Mkuu hivi ulichokiandika hapo juu ni fikra zako sahihi au ni matokekeo ya kuingizwa kwenye payroll! Hivi EL anawalipa bei gani mpaka ufahamu wenu unafifishwa kiasi hicho.
Sikutegemea mtu kama Pasco kuja na bandiko jepesi kiasi hicho!
Shame on u broda!
Nalog-off
 
Mzee Mwanakijiji, Dr. Shein ndio chaguo la JK, japo hata akisimamishwa yeye, bado tutapata mabadiliko ya kweli, tatizo vita vya udini vitakuwa vibaya kuliko vile vya 2010. Wakristu wa bara, hawatamchagua rais Muislamu for another term, hivyo mgombea Mkristo wa upinzani, atajipatia easy ride!. Sipendi tupate rais aliyepigiwa chapuo na kanisa! Tuendelee kupiga chapuo la Edward Lowassa tuu!, au hamtaki mabadiliko?.

Nitakuhakikisha jambo moja Shein atapata kura za Wakristu wengi kuliko Bilal kwa mfano japo wote ni Waislamu. Wakristu wengi na kwa kweli Watanzania wengi wameshaupitai huo udini. Shein anavyozidi kujipambanua huko Zanzibar ndivyo ambavyo anajionesha kuwa he was the reason behind the throne ya Kikwete. Watanzania wengi wanamchukulia Shein kama kiongozi aliyetulia kifikra, asiyependa makuu wala makundi. Lowassa hana temperance za kiongozi kama alivyo Shein. Kwa CCM hakuna mwanasiasa mjanja kama Lowassa lakini kama kwa kupima nafasi ya uongozi hakuna mtu anayeweza kuchukua madaraka ya nchi akiwa na uzoefu, hekima na nia ya kulinda Muungano na maslahi ya Watanzania wote kama Dr. Mohammed Shein.
 
Naona wengi wameshindwa kunielewa, wanadhani lengo langu ni kumpigia chapuo Edward Ngoyai Lowassa, la hasha hiyo si kweli. Ukweli ni kuwa mimi ni moja wa watu wenye msimamo usioyumba na ambaye anaamini kwa dhati kuwa kuwa adui mkubwa wa taifa letu ni CCM. Siwezi kumpigia chapuo mgombea yeyote wa CCM kwa sababu ninaamini ndani ya hiki chama hawezi kupatikana mtu safi asiye na doa. Kwa bahati nzuri wananchi wengi nao wameanza kuutambua ukweli huu kwamba CCM imeweza kudumu tu kwa kutegemea ukondoo na woga wa Watanzania kupambana na uovu wake.

Ni vigumu kumweleza mtu na akakuelewa kwa nini Jakaya Mrisho Kikwete alichaguliwa kwa kipindi kingine na ni vigumu zaidi kueleza kwa nini hadi leo bado ni Raisi wa taifa hili. Lakini huo ndio ukweli ingawa mchungu, baada ya kuboronga na kupata sufuri katika awamu yake ya kwanza, Jakaya Mrisho Kikwete anaendela kutanua Magogoni kama kiongozi wa taifa hili kwa awamu nyingine. Sasa kama haya yote yamefanyika na tumeyashuhudia mbele ya macho yetu na yaelekea tumeyakubali na kusalimu amri, kwa nini wengi tushangae na kuguna anapotajwa Edward Ngoyai Lowassa ?

Naomba niwape siri, CCM maji yako shingoni na kwa msingi huo kinachofanyika sasa na kama ilivyo kawaida yao ni kupanga mbinu na hila za kushinda uchaguzi 2015. CCM wanajua fika kuwa bila dola chama kitasambaratika na kufa na mafisadi ndani yake itabidi wawajibishwe na hivyo wanatumia kila hila kitabuni kuhakikisha wanabaki madarakani. Hivi vita vinavyodaiwa kufanyika ndani ya CCM ya kuwafukuza mafisadi si lolote si chochote kwani ni dhahiri ndani ya chama hiki hakuna anayeweza kumnyooshea mwingine kidole - kama sote tulivyoshuhudia katika kikao chao kilichopita, ni usanii tu uliotawala.

Wote tulishuhudia CCM wakimpigia magoti Rostamu awasaidie kwenye uchaguzi wa Igunga, sasa kama CCM wote si wapuuzi mbona hatukusikia sauti yoyote ikitoka kwa hao wasafi inaodaiwa wametapakaa humo ? Mbona hakuna mwanaCCM anayehoji tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mwenyekiti wao na je hali ingekuwaje kama mtoa tuhuma hizo hakuwa Lowassa mwenyewe ? Kwa nini tumekubali kufukia hizo tuhuma na badala yake tumejikita kumlaumu Lowassa kwa kutotoa hizi tuhuma mapema hadi akakubali kujiuzulu ili kumnusuru bosi wake, the real invisible figure behind Richmond ?

Mimi siipendi na naichukia CCM na lengo langu kuu ni kushiriki katika harakati za kuchochea kusambaratika kwa hiki chama cha mafisadi na turufu yangu kuu ni Edward Ngoyai Lowassa. Naamini kwamba hata leo Lowassa akiondoka CCM, ufisadi utabaki pale pale, uchafu utabaki pale pale na uovu wote utabaki pale pale - tatizo ndani CCM ni zaidi ya watu wawili, watu mia au hata watu elfu, ni mfumo. Wanaharakati, ugonjwa ndani ya CCM hautibiki kirahisi kama wengi wanavyofikiria na tukitaka kuliokoa taifa kutoka mikononi mwa CCM, lazima tuwe wabunifu, silaha kuu tuliyo nayo ya kuisambaratisha CCM ni CCM.
 
Patali.... why?? unauhakika sana na maisha yako na kila kitu eh??? haya bhana, wansema Mungu wa sasa kijana, unaweza ukabadnika vineno vyako hapa ghafla puuu.... na wewe mzinga
If this country has to change for better...people who do evil things, support evil deeds or having evil spirits like pasco and others of his kind they only deserve to die and burn in hell as early as possible!!!
 
Nitakuhakikisha jambo moja Shein atapata kura za Wakristu wengi kuliko Bilal kwa mfano japo wote ni Waislamu. Wakristu wengi na kwa kweli Watanzania wengi wameshaupitai huo udini. Shein anavyozidi kujipambanua huko Zanzibar ndivyo ambavyo anajionesha kuwa he was the reason behind the throne ya Kikwete. Watanzania wengi wanamchukulia Shein kama kiongozi aliyetulia kifikra, asiyependa makuu wala makundi. Lowassa hana temperance za kiongozi kama alivyo Shein. Kwa CCM hakuna mwanasiasa mjanja kama Lowassa lakini kama kwa kupima nafasi ya uongozi hakuna mtu anayeweza kuchukua madaraka ya nchi akiwa na uzoefu, hekima na nia ya kulinda Muungano na maslahi ya Watanzania wote kama Dr. Mohammed Shein.

Mzee MKJJ, watanzania wengi tunatarajia Rais ajaye ashughulike na matatizo mengi ambayo maraisi waliomtangulia wameshindwa, mojawapo ikiwa ni ufisadi. Unafikiri Shein ataliweza hilo?
 
Mag3 miye nimekupata vizuri kabisa ndio maana miye nawapatia wana CCM Shein vile vile. Yeyote atakayesimamishwa na CCM ni wa kupinga kwa sababu hatuna tatizo na watu tuna tatizo na chama. CCM ndio tatizo siyo Kikwete au Lowassa au Shein. As long as wanakuja na vazi lile bani ni wale wale.
 
Hivihaiwezekana kumpendekeza Hayati Horace Kolimba kupeperusha bendera la chamakubwa ccm. Huyu aliweza kusema kile kilichokuwa ndani ya shina la moyo wake, naki-kiakisi hali halisi. Hawa wengine kama vinyonga vile!
 
Naona wengi wameshindwa kunielewa, wanadhani lengo langu ni kumpigia chapuo Edward Ngoyai Lowassa, la hasha hiyo si kweli. Ukweli ni kuwa mimi ni moja wa watu wenye msimamo usioyumba na ambaye anaamini kwa dhati kuwa kuwa adui mkubwa wa taifa letu ni CCM. Siwezi kumpigia chapuo mgombea yeyote wa CCM kwa sababu ninaamini ndani ya hiki chama hawezi kupatikana mtu safi asiye na doa. Kwa bahati nzuri wananchi wengi nao wameanza kuutambua ukweli huu kwamba CCM imeweza kudumu tu kwa kutegemea ukondoo na woga wa Watanzania kupambana na uovu wake.

Ni vigumu kumweleza mtu na akakuelewa kwa nini Jakaya Mrisho Kikwete alichaguliwa kwa kipindi kingine na ni vigumu zaidi kueleza kwa nini hadi leo bado ni Raisi wa taifa hili. Lakini huo ndio ukweli ingawa mchungu, baada ya kuboronga na kupata sufuri katika awamu yake ya kwanza, Jakaya Mrisho Kikwete anaendela kutanua Magogoni kama kiongozi wa taifa hili kwa awamu nyingine. Sasa kama haya yote yamefanyika na tumeyashuhudia mbele ya macho yetu na yaelekea tumeyakubali na kusalimu amri, kwa nini wengi tushangae na kuguna anapotajwa Edward Ngoyai Lowassa ?

Naomba niwape siri, CCM maji yako shingoni na kwa msingi huo kinachofanyika sasa na kama ilivyo kawaida yao ni kupanga mbinu na hila za kushinda uchaguzi 2015. CCM wanajua fika kuwa bila dola chama kitasambaratika na kufa na mafisadi ndani yake itabidi wawajibishwe na hivyo wanatumia kila hila kitabuni kuhakikisha wanabaki madarakani. Hivi vita vinavyodaiwa kufanyika ndani ya CCM ya kuwafukuza mafisadi si lolote si chochote kwani ni dhahiri ndani ya chama hiki hakuna anayeweza kumnyooshea mwingine kidole - kama sote tulivyoshuhudia katika kikao chao kilichopita, ni usanii tu uliotawala.

Wote tulishuhudia CCM wakimpigia magoti Rostamu awasaidie kwenye uchaguzi wa Igunga, sasa kama CCM wote si wapuuzi mbona hatukusikia sauti yoyote ikitoka kwa hao wasafi inaodaiwa wametapakaa humo ? Mbona hakuna mwanaCCM anayehoji tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mwenyekiti wao na je hali ingekuwaje kama mtoa tuhuma hizo hakuwa Lowassa mwenyewe ? Kwa nini tumekubali kufukia hizo tuhuma na badala yake tumejikita kumlaumu Lowassa kwa kutotoa hizi tuhuma mapema hadi akakubali kujiuzulu ili kumnusuru bosi wake, the real invisible figure behind Richmond ?

Mimi siipendi na naichukia CCM na lengo langu kuu ni kushiriki katika harakati za kuchochea kusambaratika kwa hiki chama cha mafisadi na turufu yangu kuu ni Edward Ngoyai Lowassa. Naamini kwamba hata leo Lowassa akiondoka CCM, ufisadi utabaki pale pale, uchafu utabaki pale pale na uovu wote utabaki pale pale - tatizo ndani CCM ni zaidi ya watu wawili, watu mia au hata watu elfu, ni mfumo. Wanaharakati ugonjwa ndani ya CCM hautibiki kirahisi kama wengi wanavyofikiria na tukitaka kuliokoa taifa kutoka mikononi mwa CCM, lazima tuwe wabunifu, silaha tuliyo nayo ya kuisambaratisha CCM ni CCM.
Mkuu wangu sio swla la kutokukusoma vizuri bali ndivyo ulivyopendekeza.. hakuna mtu hapa anaweza pendekeza JK arudie Urais na wala hakuna mtu alopenda JK ashinke awamu ya pili kati yetu ila wapo waliopendekeza hivyo na tulibanan kwa maswali vile vile...
Kwa hiyo hujafanya kosa kuwa na pendekezo lako na ndio maana tumedai vigezo uilivyotumia maana sifa zote alizopata Lowassa ni usimamizi ktk serikali ya Mubarak kuendesha mambo ya Mubarak sasa kuna uzuri upi?...
 
Mag3 miye nimekupata vizuri kabisa ndio maana miye nawapatia wana CCM Shein vile vile. Yeyote atakayesimamishwa na CCM ni wa kupinga kwa sababu hatuna tatizo na watu tuna tatizo na chama. CCM ndio tatizo siyo Kikwete au Lowassa au Shein. As long as wanakuja na vazi lile bani ni wale wale.

Hakuna mbadala wa CCM at least in terms of personalities hasa kutoka upinzani..

Kuuikataa ccm kwa sasa ni sawa na biashara ya "SHAURI YAKO"
 
Mkuu wangu sio swla la kutokukusoma vizuri bali ndivyo ulivyopendekeza.. hakuna mtu hapa anaweza pendekeza JK arudie Urais na wala hakuna mtu alopenda JK ashinke awamu ya pili kati yetu ila wapo waliopendekeza hivyo na tulibanan kwa maswali vile vile...
Kwa hiyo hujafanya kosa kuwa na pendekezo lako na ndio maana tumedai vigezo uilivyotumia maana sifa zote alizopata Lowassa ni usimamizi ktk serikali ya Mubarak kuendesha mambo ya Mubaraka sasa kuna uzuri upi?...

Hata usimamizi siyo mzuri ila "media attention seeker" hafanyi kitu kwa nia njema kwa watu ila masifa tuuu...

Pili katika vitu ambavyo watu wengi hawatamsamehe EL katika CCM ni kwamba ana roho mbaya na anaonea hata wapishi nyumbani kwake he so arrogant and stupid ..akiwekwa tutafuta mbinu mbadala, trust me..
 
Kama hakuna mwenye nafuu zaidi ya Lowasa je Mkapa kipiindi kile alichomolewa kutoka wapi? Walipomchomoa mkapa watafute na wengine watawapata amba japo watatumia miaka mitatu kufanya kazi na sio kulazimisha eti hakuna mwenye nafuu zaidi ya RICH man of MONDULI
 
To be frank hata mimi namkubali sana Lowasa kwani niambie mbona aliweza kuvunja mkataba wa city water na kesi tukashinda ndani ya muda mfupi? The man is intelligent and hard working. Kumbuka alivyoisafisha Posta , alivyomchukulia hatua mhandisi wa wilaya ya Temeke etc. Mangapi tumeshaona kwa mtoto wa mkulima ambaye anaonekana ni msafii? Watanzania tusiote hata hawa wapinzani kuwa wakiingia tutaona makubwa kama wanavyosema. Kikubwa ni kwamba watu wameichoka CCM lakini kama watajitazama kwa upya bado wanaweza kabisa kuchukua dola. Mtabisha lakini huo ndio ukweli!!!
 
Aliweza kuwafukuza Citywater halafu akafanya nini? tatizo la maji limekwisha nchini ama Dar limekwisha maaana nijuavyo mimi hadi kesho tunakunywa maji ya chupa..matanki ya Mchina ndio yanazidi kupanda bei.. Amefanya nini kwa kuliwezesha Taifa kwenda mbele.. Kiongozi mbunifu unafukuza Citywater kwa sababu za kisheria na una mpango wa kuboresha na sio kulitokomeza zaidi taifa. bado naomba mazuri ya Lowassa pengine hamumjui vizuri mnasikia tu habari za matangazo...
 
Mkuu wangu sio swla la kutokukusoma vizuri bali ndivyo ulivyopendekeza.. hakuna mtu hapa anaweza pendekeza JK arudie Urais na wala hakuna mtu alopenda JK ashinke awamu ya pili kati yetu ila wapo waliopendekeza hivyo na tulibanan kwa maswali vile vile...
Kwa hiyo hujafanya kosa kuwa na pendekezo lako na ndio maana tumedai vigezo uilivyotumia maana sifa zote alizopata Lowassa ni usimamizi ktk serikali ya Mubarak kuendesha mambo ya Mubaraka sasa kuna uzuri upi?...

Mkuu Mkandara, pamoja na kunisoma lakini nilichoongelea ni kile kinachoitwa "worst case scenario" na nilisema hivi;
Ukweli ni kuwa kama Raisi 2015 atatoka CCM (na hilo Mungu atupishilie mbali !), basi ndani ya hiki Chama cha Mafisadi, kwa sasa hakuna kama Lowassa kama taifa linataka kujinasua kwenye dimbwi la utawala legelege uliojaa usanii. Uwajibikaji, uvumilivu na ujasiri aliouonyesha ni dalili nzuri katika Uongozi kama hazitasukumwa na ulafi na tamaa, vitu ambavyo hata hivyo vimemganda kama kupe na kumwandama kama kivuli chake !
Ombi langu ni kuwa Raisi asitoke CCM, tumaini langu ni kuwa Raisi hatatoka CCM na ndoto yangu ni kuwa Tanzania itawezekana bila CCM.
 
We have a myriad of problems, tafadhalini sana tuwekeni misingi ya kuchagua viongozi based on standards, principles and records, not personalities.

Leo hii tuna shida kibao. Uchumi wote uko hovyo, elimu ndio kabisa, afya, ajira, miundombinu.. Matatizo ni mengi. Katika majadiliano yetu hapa hakuna anayeyataja, wala kuja na suluhisho la haya yote. Huyu anasema Lowassa afadhali, mwingine Membe.. Afadhali kivipi? Tutajuaje wanafaa wakati hata hawaongelei ni njia zipi watazitumia kutatua matatizo yetu?

Kwa nini tusiweke standards, principles na kuhoji their past records na iwe ndiyo blueprint yetu ya kupata viongozi.

Mfano, rasimali ya kwanza ambayo tunatakiwa kuwa nayo si uranium wala tanzanite bali "akili/brains". Hivyo kwa nini tusiweke priority katika elimu (formal and informal) kuwa ndio vision yetu kama nchi. Twende mbali zaidi na kusema kuwa elimu hii kwa asilimia kubwa iendane na matumizi ya rasimali tulizonazo, hivyo kwamba miaka ya baadae tumiliki rasimali zetu na tushikilie uchumi wetu. Maswali yanakuja, hiyo elimu tutaipataje? Gharama zake? Professions gani zipewe priority? Wapi zinapatikana? Tuna vyuo vingapi? Tuna walimu? Kuna fedha ya kulipa walimu? Vyuo vyetu vinaproduce kitu kweli au ndio ujinga in ujinga out hivyo tuvi-reform?

Then tunaenda kwenye afya, miundombinu nk.. Kote huko tukiwa na priorities na standards zetu. That's how it should be done.

Haya mambo ya kusema huyu kijana mwenzetu apite, mara huyu nyerere alisema hafai/anafaa, mara huyu alilala na huyu na yule, dini yake ni hii, mara huyu ni mtoto wa fulani.. Bila standards tutaendelea kuongozwa na wapumbavu waliowekeza kwa wapambe na washabiki huku wenye uwezo wakikaa pembeni kuogopa fedheha wakiogopa hoja zao kutojadiliwa bali personalities zao..

Back to the thread, kama Lowasa ni mwizi na kuna ushahidi kwa nini hayuko jela? Serikali ni ya CCM. Kwa nini wasimfukuze uanachama kwa sababu chama ni chao na wao ni wasafi? Chama ni chao. Kama mwenyekiti anaogopa kumfukuza, kwa nini mwenyekiti asifukuzwe then Lowassa afukuzwe? Hapo ndipo naconclude CCM wote wezi, wanafki na/au waoga. On top of that, it's evidently they have failed us big time.
 
If this country has to change for better...people who do evil things, support evil deeds or having evil spirits like pasco and others of his kind they only deserve to die and burn in hell as early as possible!!!
what you pray for is as evil as what you are condemning... just look in the mirror and ask yourself who is more devilish!! SICK
 
Back
Top Bottom