Ndiyo kateuliwa lakini hapendwi na wengi

Mie nimefurahi rais hajasikiliza manenobya mitandaoni na wapinzani kumpangia watu...kawapiga low blow moja matata...
 
Jamaa anachukiwa kwa sababu ni wale watu wanaishi kijanja janja halafu hana uwezo wa kuongoza. Busara pia ziro.
Kumbuka huyu sio kilaza Mnyika wala kilaza Mbowe. Ame elimika vizuri sana, na ni mmoja ya watanzania waliofauli vizuri. Inawezekana nazungumza na mwana JF ambaye hajui nini maana ya kupata First Class katika ngazi ya Degree.

Alifanya vizuri kwa nafasi ya Ukkurugenzi, Benki Kuu na Naibu Waziri wa Fedha, hayo ya kumkomesha Rwakatare kama Mbunge wa Bukoba kupitia Chadema haiuondoi usomi wake, weredi wake haitufanyi Watanzania wote tusahau uwezo wake.

Hatushangai tunafahamu kuna watanzania wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii na hawana jema. Ukimtukana baba yako wana kusifia, ukimfanyia mazuri mzazi wako wanakuzomea.

Jamii gani hii ya Jamhuri ya JF. Ukiwa Mchaga utasakamwa Ukiwa Msukuma hafai, ukiwa kiliza uko Chadema wewe Msomi, ukiwa na akili puvu ukiwa CCM wewe mjinga. Taabu tupu.
 
Dr Mwigulu Nchemba kati ya WaTanzania 10 wanaolitaja jina lake ni wawili au watatu ndiyo wanamwona ni Kiongozi mzuri. Dr. Mwigulu alikuwa mzuri wakati upinzani ulipokuwa imara - yaani Waziri wa Vijembe Vijembe hivi.

Hata nafasi aliyopewa na JPM ndiyo ilikuwa inamfaa. Kwa sasa alipaswa kuwa ile ya Bashungwa sio sijui. Wizara ya Fedha Mwigulu hafai - mnaweza mkawa mnaogopa bure tu.

Bora hata Dr Mkenda au Dr Kimei ana PR nzuri kuliko Mwigulu. Kuna wengi wanafaa nafasi hiyo lakini sio Mwigulu ambaye ni Mwanasiasa mkorofi, mwenye visasi na mjanja mjanja hivi.

Mwigulu bora hata angepewa nafasi ya Mhagama halafu Mhagama akapewa TAMISEMI na Ummy akapewa Utalii au Kilimo. Kwa Mwigulu ambaye ni Mwanasiasa haswa ni hakika uchumi utadorora kwa sababu utakuwa wa kisiasa zaidi na hata usitegmee wafanyakazi kupata maslahi mazuri na hata wafanyabiashara itakuwa hovyo hovyo tu.

Kwa kifupi Mwigulu hafai pale - bora abadilishwe haraka.
You are not serious
 
Si kwamba namtetea, ila Mwigulu Nchemba anafaa katika wizara hii ya fedha

Tukumbuke alishawahi kuwa katika wizara hii na katika awamu yao hiyo ndio wizara ya fedha ilikuja na mifumo madhubuti ambayo kwa kiasi kikubwa ina control matumizi ya fedha za umma

Kubwa ninalokumbuka na alilofanya vizuri kipindi hicho ni mfumo wa ulipaji mishahara kwa watumishi wa umma "Lawson" (Sina hakika na spelling)

Huu mfumo kwa kiasi kikubwa ndio unaosaidia watumishi kupata mshahara kwa wakati na kwa pamoja kuliko ilivyokuwa zamani

Pia kwa kiasi kikubwa huu mfumo umedhibiti maafisa watumishi kulipa mshahara "account" fake na kwa kiasi kikubwa hakuna namna mtumishi wa umma atakosa mshahara kama yupo kwenye mfumo endapo yupo kazini Kama ilivyokuwa zamani

Pamoja na "ulimbukeni" wake aliouonyesha kipindi cha Magufuri, ila bado ni mtu makini pale anapokuwa na watu sahihi

Binafsi naamini alikuwa hivyo alivyo kwasababu ya kutaka kuendelea kubaki madarakani maana ndio aina ya Boss aliyekuwa nae

Bila kujipendekeza na kujifanya hazimo kulikuwa hamna namna ya kuendelea kula

Tumpe muda tuone Kama "sifa" zitaendelea ndio tumseme

Mtu ambaye naona ni "incompetent" mwanzo mwisho ni Jaffo

Huyu bwana ni Mzee wa makelele sijawahi ona utendaji wake tangu aanze kujulikana. Naamini huyu wanamstili tu lakini hana anachofanya
Hafai hafai
 
Mkuu, Mwigulu Nchemba ndiyo waziri wako wa fedha kwa sasa

Kama unawapenda kina Kimei na Mkenda waajili nyumbani kwenu.
 
Back
Top Bottom