Ndio wasomi wenyewe hawa.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndio wasomi wenyewe hawa..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 13, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hussein Kauli (Mwananchi)


  CHAMA Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu(THTU) kimesema hakiungi mkono mgomo uliotangazwa na Shirikisho la Vyma vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa madai kuwa kinaangalia maslahi ya taifa.

  Katibu mkuu wa chama hicho, Kulu Maswanya alisema kuwa kuwa nia ya Tucta ni kupata sulahu ya matatizo sugu yanayowakabili, lakinin akaongeza kuwa njia bora ni majadiliano ya kina yatakayofanya upembuzi yakinifu.


  Maswanya alisema silaha ya mgomo itakuwa na maana tu iwapo majadiliano hayo yatakayowezesha kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu, hayatafikia malengo.


  Naye mwenyekiti wa chama hicho, Dk Elifuraha Mtalo alisema wameamua kutounga mkono mgomo ulioitishwa na Tucta kwa kuwa hawakushirikishwa katika kuupanga.


  Alishangazwa na uamuzi wa mgomo huo uliopangwa kuanza Mei 5 mwaka huu kwa kuwa Tucta imekuwa ikishirikishwa kwenye vyombo vya maamuzi na serikali na kuleta matunda kwa wafanyakazi, ikiwemo kuundwa kwa bodi ya mishahara.


  “Hali hii ya ushiriki wa Tucta katika vyombo vya maamuzi na nia ya TUCTA kuandaa mgomo inaashiria kuwa kuna tatizo la msingi; ama la mfumo wa ushirikishwaji wa wafanyakazi au ushiriki dhaifu wa TUCTA katika vyombo vya maamuzi,” alisema Maswanya.


  Alisema kama tatizo ni mfumo, vyama vya wafanyakazi viwe tayari kukataa mfumo huo kwa dhamira ya wazi kwa kujiondoa kwenye vyombo vya maamuzi ili kutoa fundisho kwa serikali.


  "Iwapo tatizo ni udhaifu wa ushiriki wa vyama katika vyombo hivyo, ni vyema vyama vijitathmini upya ili kuwa na ushiriki bora utakaoleta tija kwa wafanyakazi,"alisema Maswanya.


  Maswanya alisema pamoja na kufikia maamuzi hayo, anakubali kuwa matatizo yaliyotolewa na Tucta ni ya msingi na yanagusa maslahi ya wafanyakazi wote na pia ni ya muda mrefu.  My Take:
  yaani.. wasomi wenyewe ndio wanapata shida ya kujua kama wagome.. sitoshangaa maprofesa wa vyuo vikuu wakiandamana kuunga mkono serikali!
   
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lakini kwani kuwa wasomi ni kugoma? Vipi kama hawaridhiki na sababu au jitihada zilizofanywa na chama cha wafanyakazi.
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nafikiri wana point.............ushiriki wa TUCTA kwenye maamuzi wa maslahi ya wafanyakazi Tanzania.......unahitaji kuangaliwa tena.........

  Mkuu Mwanakijiji......unaelewa nguvu ya vyama vya wafanyakazi inavyokuwa........lakini nyumbani........kwa kweli inasikitisha.....ni ukondoo tu

  .........Kama ni kweli kuwa THTU hawakushirikishwa......ni vema position yao ikawa clear...........ku-join vita usiyoifahamu you are likely to be shot first...........
   
 4. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kuridhika na jitihada zinazofanywa na chama cha wafanyakazi ni suala moja, lakini kuridhika na hali iliyopo na mwenendo wa serikali kwa wafanyakazi wake ni suala lingine. Inahitaji kuwa na moyo wa ajabu sana kama wa hawa wasomi wetu kuona kuwa mgomo si njia muafaka wa kutatua matatizo ya wafanyakazi na majadiliano na serikali ya aina ya JK yanaweza kuzaa matunda.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Mar 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kuwa Maswanya na Mtalo wana point, yaani viongozi wa TUCTA wanataka kuwaendesha wafanyakazi puta. Kama kweli viongozi wa TUCTA walishirikishwa katika maamuzi ya serikali na wakapitisha maamuzi yasiyokuwa na maslahi kwa wafanyakazi basi viongozi hao ndio wa kulalumiwa. Mgomo ungekuwa na maana tu kama serikali ilijiamulia mabo kimya kimya bila kuwashirikisha TUCTA.
   
 6. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kichuguu,
  Mzizi wa fitina hapo haujaelezwa na kina bwana Maswanya na Mtalo. Kwa kifupi, TUCTA inaundwa na vyama huru 14 vya wafanyakazi, na RAAWU (cha kina Maswanya na Mtalo) si kimojawapo kati ya vyama hivyo 14 vinavyounda TUCTA. Hivyo basi kwa maelezo hayo, mgomo huu hauwahusu period!! kama watapenda kuwa sehemu ya mgomo kwa kuu-suport or otherwise hilo ni suala lingine, lakini kuupinga kwa madai waliyoyatoa kuwa hawakushirikishwa ni upuuzi kwa kuwa wao si sehemu inayounda TUCTA .
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Unajua hivi karibuni wafanyakazi/wahadhiri walikuwa wakilalamikia mafao yao ya kustaafu kuwa kidogo kulinganisha na wafanyakazi wengi wa sekta nyingine na wakiomba kuangaliwa upya ukokotoaji wa mafao.
  Cha ajabu ni kwamba nguvu ya TUCTA ilikuwa ndogo au haikuwepo kabisa. Nadhani TUCTA inatakiwa ifanye jitihada ya kuwaunganisha wafanyakazi maana wanaonekana si msaada kwa baadhi ya sekta. Mfano mwingine ni miaka kadhaa iliyopita ambapo wafanyakazi wa Mahospitalini (Dr) waligoma kuwaunga mkono sababu ikiwa ni ile ya ushiriki wao mdogo katika kutatua matatizo.
  Nadhani kabla hawajaanza jitihada za kupambana na serikali wangejitazama na wao. Wafanyakazi wengi hulalamika pesa wanazokatwa kwa ajili ya vyama vyao maana jitihada ambazo ni balanced hazionekani.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wakati mwingine mtu anahitaji kuongeza.. vikao baadaya vikao.. majadiliano baaday a majadiliano.. at the end somebody need to take a stand. Ambao wanasema hawatashiriki kwa sababu "hatukushirikishwa" wanatakiwa waachwe pembeni.

  Sisi hapa tunazao UAW na tunaamini uongozi wa UAW kitaifa unahitaji kuonesha maamuzi na kuongoza na vyama vyetu vya sehemu mbalimbali vinakaa na aidha kuunga mkono hoja za UAW au la. Hilo linafanywa kwa kutuita wafanyakazi kama tunakubaliana na mgomo ulioitwa na UAW kwenye tawi letu.. karibu mara zote tunakubali na kuwapa nguvu viongozi wetu kutekeleza maagizo ya UAW.

  Sasa huo uongozi wa wafanyakazi wa elimu uliwapa wanaowawakilisha haki ya kuamua kushiriki au la au wao kwa vile ni viongozi wameamua kutoshiriki kwa sababu hawakushrikishwa? As a matter of fact kwenye migomo ya wafanyakazi vile vyama vingine vinajiunga na mgomo kwa sababu vinakubaliana na malengo ya mgomo huo siyo kwa sababu vilishirikishwa kwenye vikao.

  Leo hii walimu wa Chuo Kikuu cha Houston wakianza kugoma kwa sababu ya unyanyasaji na serikali kupinga na jumuiya ya wafanyakazi wa elimu kitaifa ikaitisha mgomo, usidhani kiila vyuo vikuu vitataka vishirikishwe kwenye maamuzi. Kitakachofanyika ni kuwa vyuo vingine vitaamua kushiriki (kwa sababu wanakubaliana na mgomo) au la.

  Ndio utasikia "Chama cha Wafanyakazi chuo kikuu cha michigan kimetangaza kuunga mkono mgomo wa wafanyakazi huko Houston mpaka matatizo ya wenzao yametatauliwa"..

  Ndio maaana kauli ya vyama vya wafanyakazi duniani ni kuwa "Workers of the World Unite!".. sasa hawa wapuuzi (i mean that) wanapoamua kutoshiriki mgomo kwa sababu hawakushirikishwa wanatakiwa watimuliwe na wanachama wao mara moja kwa sababu wameweka ujiko wao mbele kuliko kanuni za msimamo wa pamoja katika kudai maslahi. Ni watu wa hatari katika kuendeleza maslahi ya wafanyakazi..

  Don't even get me started kwenye haya ya wafanyakazi...
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji,
  1. Hiko chama cha wasomi mbona mambo yao ni mswano!. Wanataaluma take home yao inaanzia Six figure, wagomee nini?. Naamini wafanyakazi wa taasisi za elmu ya juu ambao sio wanataaluma, waawishi uunga mkono mgono, labda kama viongozi wao watawasaliti kuegemea kwa wanataaluma.

  2. Wafanyakazi wa Tanzania ni waoga na wanafiki, kaa walivyo waanchi wa Tanzaia a kuichagua CCM. Hata kaa TUCTA itaorganize vipi, momo hautafanikiwa wa sababu at the end of the day, seriali itapata court injuction itakaodeclare mgomo ni illegal, watatoa tangazo atakayegoma, amejifukuzisha kazi, mgomo utafutwa.

  3. Kama inavyohitajika kuwaelimisha watu kuwa CCM haina hati miliki ya utawala wa nchi hii, baadhi ya watu wanaichagua CCM kwa uoga na ignorance tuu, lakini wakielimishwa wataamka, ndivyo wafanyakazi wa Tanzania, wanavyotakiwa kueimishwa kuwa mgomo ni haki yao, na mwajiri, hana uwezo wa kumtimua kazi mfanyakazi aliyegoma kwa mujibu wa sheria.

  4. Last week wafanyakazi wa Umma wa Uingereza wamefanya one day strike, Wizara ya ne ya Uingereza, FCO, ikawaomba wanabalozi wake wasigome, ili wasiwatese maelfu ya wategemea huduma za wanabalozi hao, kama viza, hivyo hawakugoma, japo stand still ilikuwepo kwa sababu clearance, inatoka London kwenye mgomo. Hivyo chama hicho ama kweli hakikushirikishwa na kinaona mgomo huo hauna tija kwa maslahi ya chama chao, then its their right kutounga mkono. Hapa issue sio umoja ni nguvu, hapa ni vita vya maslahi.

  5. Kusema kweli nikimkumbua Leach Walessa wa Poland miaka hiyo, Tanzania bado hatuna chama cha wafanyakazi, vilivyopo ni mfano vyama tuu
  kama jinsi tusivyo na chama cha upinzani ukiondoa mifano vyama vilivyopo!.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Naona tatizo la complacency Tanzania. Everywhere I look.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  i remember Bruno Mpangala.. sijui aliishie wapi.. wajifunze kutoka kwa Morgan kule Zimbabwe au Lula wa Brazil.. bado hatujapata Rais anayetoka kwenye vyama vya wafanyakazi.. angalau tuliwahi kuwa na kina RMK..
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Mar 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Bila kukubaliana na Maswanya + Mtalo, bado nina mashaka sana na uongozi wa TUCTU kwa vile walishiriki katika kupitisha maamuzi ya serikali wanayotaka kugomea sasa.
   
 13. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimefurahia neno "upuuzi"

  Ni upuuzi kama huu mara zote unarudisha nyuma harakati za kupambana na maovu nchini mwetu. Hivi wangekaa kimya na siku hiyo wao wakaenda kazini ingeathiri nini? kwa kuwa yeye na watoto wake wanashiba basi haoni mantiki nzima kwenye hoja ya mgomo?

  hii haina tofauti sana na ile ya kuwa " nilitaka kufukuzwa uanachama" Kwani maalimu Seif alipofukuzwa alipoteza nini ambacho hana leo?

  Mantiki ni masilahi ya walio wengi, period. Mengine yanakuja baadae.

  Na huo ndio USHUJAA.

  Naitamani forum ambayo naweza kutukana na kupoteza kidogo hekima yangu. Bahati yao haipo.
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni walewale tu wanajiandaa kugombea ubunge na kuacha kazi zao za sasa so ni namna tu ya kutafuta kaangwa mkono na viongozi wa Chama Changu Mie!
   
 15. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji,
  Bruno Mpangala hakuwa na bahati ya Mama Sita, yeye alitumika kuwalaghai wafanyakazi wenzake akiahidiwa ubunge wa Mbeya mjini, bahati haikuwa yake, ubunge aliukosa kwa kushindwa kupita kwenye kura za maoni na kule kwa wafanyakazi akashindwa kurudi baada ya kujionyesha kuwa yeye ni mtu wa CCM, hivyo ikala kwake.
   
 16. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nia na dhamira zao ni tofauti kabisa na wanayotoa vinywani mwao, Kwa kuwa wasomi ni wengi humu, hawa wanatakiwa kufukuzwa uongozi haraka sana.

  Uharaka wa kauli zao, ni dhahiri kuwa hawakuwasiliana na wanachama wao. hivyo kimsingi hawajawashirikisha wanachama wao, na hii ndiyo msingi wa hoja yao. SOPENDI UPUUZ:(
   
 17. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pasko umesema,
  Sikuona ajabu na nilikuwa nategemea hali kama hii kutokea. Hii siyo kwa vyama vya elimu ya juu tu ila kwenye taasisi zote zilizo na wanaojiita wasomi (wenye masters na PhDs). You know why, divide them and rule them. Watanzania tunabaki na nyimbo tu lakini vitendo hakuna. By the way, hata yanapotokea maswala ya maslahi yanayowahusu wasomi, wanapenda kushiriki kivyao kwa utaratibu ule ule wa tugawe tutawale.
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  watafuata madaktari , then wafanyakazi wa serikali kuu. then watabaki walimu na wafanyakazi wachache wa sekta binafsi.

  Serikali na sisi wananchi tuna bahati sana .huwa najiuliza wakulima wangekuwa na uwezo na njia ya kufanya mgomoooo.

  Kwa kweli katika kundi la wafanyakazi linanyonywa sana ni wakulima
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ukweli huo hapo juu si vema ukawa ignored..........kwenye harakati za namna hiyo...........

  .........ni vema pia kujifunza kutokana na experience............ya hizi nia za migomo....
   
 20. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #20
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nakwambia, inatia kinyaa. In Tanzania, wasomi are the worst enemy of the people. We are the most coward and hypocritic of all the groups. This explains why the opposition gets the least support in cities where the so called 'wasomi' are residents!! Ukombozi wa nchi yetu utaletwa na mwananchi, the common man in Kantalamba, Mgela, Nzega,etc.
   
Loading...