Ndio! Mazingira magumu ya kufanya kazi; Ndio! Malipo ya chini; Ndio! Hata hivyo sio kisingizio cha kubaka na kushambulia wagonjwa na wanafunzi

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Wafanyakazi wa Afya na Walimu ni waajiriwa wakuu serikalini. Mshahara wao na hali yao ya kazi ni duni sana . Na tunapaswa kuwahurumia na kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha hili swala.

Walakini, katika siku za hivi karibuni tumesikia visa kadhaa vya kushambuliwa na ubakaji wa wagonjwa na wanafunzi. Kesi mbili zimenishangaza: jaribio la waalimu wawili wa kiume kumtoa mimba mwanafunzi wa miaka 16 baada ya kubaka(kisheria ni ubakaji kwani ni chini ya 18); na Muuguzi / Mkunga aliyesajiliwa kumpiga kofi mjamzito.

Kesi zote mbili ni za kutisha na hazina kisingizio licha ya umati wa mtandao ambao umejaribu kuwatetea wahutuhumiwa.

eti: "hatujui mazingira mazuri ya labour" ,"Nurse alijaribu kumzuia mjamzito kuua mtoto".

Taaluma hizi, ualimu na Uuguzi, ni za hiari: Hakuna mtu anayelazimishwa kujiunga. Kwa kuongeza, wana viwango vyao vya wazi ambavyo vinawatofautisha na kazi zingine (naongea kama mwana taaluma wa afya).

Huruma, kuaminika, na weledi ndio hufautisha Muuguzi kutoka kwa mtu wa nasibu anayejali mgonjwa
. Ndo maana mtu analipwa! Ndiyo sababu muuguzi amethibitishwa. Muuguzi anatarajiwa kufanya kazi yake kinyume na mihemko ya mtu wa kawaida ya hasira au fustration.

hivyo hivyo unaweza kusema kuhusu waalimu.

Kwa hivyo kwa wale wanaokiuka uaminifu huu, hawanastahili kutambuliwa kama wataalamu kwani hawana tofauti na mjinga wa karakana ambaye anafundisha au kumtunza mgonjwa.

Serikali inapaswa kuhitaji bodi za wataalam kuwa kali zaidi katika utekelezaji wa viwango vya kitaalam
 
Back
Top Bottom